Showing posts with label Makamu Wa Rais. Show all posts
Showing posts with label Makamu Wa Rais. Show all posts

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR MH BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA BALOZI MPYA WA JAPAN NCHINI

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR,BALOZI SEIF ALI IDDI AKIZUNGUMZA NA BALOZI MPYA WA JAPANI NCHINI TANZANIA,BW. MASAKI OKADA ALIYEFIKA OFISINI KWAKE VUGA KUMTEMBELEA.


Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameihakikishia Japan kwamba misaada inayotowa kwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla itaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.

Balozi Seif ametoa kauli hiyo hapo Ofisini kwake Vuga wakati wa Mazungumzo yake na Balozi Mpya wa Japan Nchini Tanzania Bwana Masaki Okada.

Alisema Misaada ya Nchi hiyo ukiwemo ule mkubwa wa Maji Safi ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi utawawezesha Wananachi na hata Wawekezaji kutumia huduma hiyo kwa ufanisi.

Balozi Seif alimueleza Balozi Masaki kwamba Japan bado ina nafasi kubwa ya kusaidia Maendeleo ya Kilimo, Maji na hata Mafunzo katika Fani tofauti.

Hatua hii itaziwezesha pande hizo mbili kuendeleza kushirikiana katika ile dhana na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Japan.

“ Japan imepiga hatua kubwa ya Kitaalamu katika sekta za Kilimo na Taaluma ya Teknolojia ya Kisasa. Hivyo Taaluma hiyo inaweza kusaidia Nchi nyingi hasa za Bara l;a Afrika ambazo zinategemea zaidi Kilimo ”. Alisisitiza Balozi Seif.

Akizungumzia Uwekezaji Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanziba inahitaji Wawekezaji Kutoka Nchini Japan katika kuimarisha uchumi wake.

Alisema ni vyema kwa Makampuni na Taasisi za Uwekezaji Nchini Japan zikaangalia uwezekano wa kufungua Miradi yao Zanzibar hasa katika Sekta ya Utalii ambayo hivi sasa ina wawekezaji wengi zaidi kutoka Nchi za Bara la Ulaya.

Kuhusu suala la Usafiri wa Baharini Balozi Seif aliiomba Japan kuangalia uwezekano wa kusaidia mpango wa SMZ wa Upatikanaji wa Meli kwa ajili usafirishaji Wananchi kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Balozi Seif alisema Zanzibar inahitaji Meli mpya kwa ajili ya kutoa huduma za uhakika zitakazoondoa hofu za wananchi ambao kwa sasa wanategemea usafiri wa Boti.

“ Zanzibar inahitaji kuwa na Meli Mpya hivi sasa kwa vile zile zilizonunuwa katika miaka ya 70 zimeshapitwa na wakati ingawa moja ya M.V Mapinduzi tayari imeshauzwa kutokana na uchakavu wake ”. Alifafanua Balozi Seif.

Naye Balozi wa Japan Nchini Tanzania Bwana Masaki Okada alielezea matumaini yake kwamba Makampuni mengi na hata Taaasisi za Huduma Nchini mwake zimeonyesha nia ya kuwekeza Hapa Zanzibar kwa vile Tanzania ni Miongoni mwa Nchi zilizopewa kipaumbele na Japan katika kushajiisha miradi ya Maendeleo.

Balozi Masaki alisema Japani inaiangalia Zanzibar kama mahala pazuri kwa uwekezaji na ni kituo muhimu zaidi kwa Biashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Bwana Masaki alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba ombi la Zanzibar la upatikanaji wa Usafiri wa Baharini ataliwasilisha kwa Waziri wa Fedha wa Nchi hiyo kwa ajili ya ufumbuzi unaostahiki
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA WIZARA ZA MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU, JIJINI ARUSHA JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu , uliofunguliwa leo Nov 4, katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa AICC, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo eliofunguliwa leo Nov 4, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wanawake na Watoto Zanzibar, Zainab Omar, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu, ulioanza leo Novemba 4, katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo Magesa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Balozi Liberata Mulamula, wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC Mkoani Arusha kufungua mkutano wa wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu. Mkutano huo umefunguliwa leo Novemba 4.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

ZANZIBAR YATIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YAKE NA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA NCHINI MAREKANI

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI NA RAIS WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA NCHINI MAREKANI DK.JAMES H. AMMONS WAKITIA SAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO KATI YA CHUO KIKUU CHA FLORIDA ( FAMU ) NA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR ( SUZA ).

MKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA ( FAMU ) DR. LEONARD PERRY AKIMUONYESHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI MOJA YA INJINI ILIYOBUNIWA NA WATAALAMU WA CHUO HICHO.


DR. SUBRAMANIAN RAMAKRISHNAN AKIMTEMBEZA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI KATIKA MOJA YA MAABARA KUU YA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA ( FAMU ).



Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Mashirikiano kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini marekani.

Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.

Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hicho cha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha { FAMU } Dr. James ammons.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.

Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.

“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.

Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida

{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida { FAMU -FSU }.

Mkuu wa Kitengom hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.

Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.




[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAKAMU WA RAIS DK GHALIB BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAZINGIRA, MAANDALIZI YA MKUTANO WA DURBAN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo, kuzungumzia maandalizi ya Mkutano wa 17 wa Nchi zilizoridhia mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Durban Afrika ya Kusini. Kushoto ni, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia mabadiliko ya Tabianchi, Richard Muyungi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WAKURUGENZI WA TPDC NA TIC OFISINI KWAKE IKULU JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta nchini (TPDC), Yona Killagane, wakati walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Masoko na Uwekezaji wa Shirika hilo, Dismas Fuko.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Nyaraka za kujisomea kuhusu Uwekezaji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Gondwe, wakati alipofika yeye na ujumbe wake kumtembelea Makamu wa Rais kwa mazungumzo ofisini kwa Makamu, Ikulu Dar es Salaam leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati walipofika ofisini kwake jijini Ikulu Dar es Salaam leo. Picha na muhidin Sufiani-OMR.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WANAHARAKATI, VIONGOZI WA DINI:Wahofu Rais ajaye atakuwa dikteta

WAUNGANA KUMDHIBITI 

Habari na Leon Bahati

VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini na wanaharakati wameonya kuwa kuna kila dalili kwamba mtu atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete atakuwa na hulka za kidikteta, hivyo wakataka Watanzania kuandaa mbinu za kumdhibiti mapema.Angalizo hilo lililotolewa na viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Chama cha Wanataaluma Katoliki (PCT), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Jumuiya ya Ahmadiya Tanzania, Makanisa ya Kipentekoste Budha na Wabahai, limekuja kipindi ambacho joto la urais wa 2015 linazidi kuongezeka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mjadala wa siku mbili wa viongozi wa taasisi za dini nchini wakiongozwa na wanaharakati wa mabadiliko ya katiba nchini uliofanyika Dar es Salaam jana, viongozi hao walisema njia moja kuu ya kumdhibiti kiongozi wa aina hiyo ni kutungwa kwa Katiba Mpya ambayo itambana Rais kwa kupunguza mrundikano wa madaraka aliyonayo kwa sasa.

Kwa upande wa wanaharakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga alisema: “Rais mwingine akija, (kabla ya Katiba Mpya), hatakubali mabadiliko yafanyike. Hivyo jambo linaweza likavutwa tena kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ijayo.”
Kiwanga ambaye alikuwa akifafanua mambo mbalimbali baada ya mada yake aliyowasilisha juu ya ukweli kuhusu mabadiliko ya katiba nchini, alisema kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye akatumia udikteta unaotokana na katiba ya sasa kumrundikia madaraka kukwamisha mabadiliko hayo.

Alisema wanaharakati wengi wa kisiasa nchini tayari wameweka ajenda ya kuhakikisha katiba ijayo inapunguza madaraka hayo, jambo ambalo wanaamini ni mwiba mchungu kwa Rais ajaye.Katika kufanikisha mkakati huo, aliwataka viongozi hao wa dini kushiriki katika kuhamasisha mpango wa katiba mpya ili ukamilike kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Alisema uzoefu unaonyesha kuwa viongozi wengi barani Afrika huzubaisha mabadiliko ya katiba, ili kulinda maslahi yao wawapo madarakani.
Mwanaharakati mwingine, kutoka Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu Rais Jakaya Kikwete tayari amewaahidi Watanzania kuwa Katiba Mpya, itakuwa tayari mwaka 2014.
Kibamba aliwataka viongozi hao wa dini kuongeza nguvu katika kuchochea shinikizo la mabadiliko hayo, ili yasije kukwamishwa na wanasiasa wenye uchu wa madaraka.

“Ingawa vuguvugu la kudai Katiba Mpya lilianza mara baada ya uhuru, mchakato wa maandalizi yake ulipata msukumo mpya kwa tamko la Rais kuridhia madai ya Katiba Mpya mwishoni mwa mwaka 2010,” alisema Kibamba na kuongeza:
“Kwa sababu hiyo, Watanzania wengi, akiwamo Mheshimiwa Rais (Kikwete) wamependekeza kuwa mchakato huo uchukue miaka minne, yaani kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.”

Ingawa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikwishasema kwamba Katiba Mpya itakuwa tayari ifikapo Aprili 26, 2014, Kibamba aliwataka viongozi hao wa taasisi za dini kuongeza nguvu katika harakati hizo za katiba kutokana na ukweli kwamba wanasiasa ni vigeugeu na wanaweza kuzorotesha mchakato.
Kibamba alionyesha picha ya jumba la kifahari ambalo linamilikiwa na aliyekuwa Rais wa Misri, Hosni Mubarak kama kielelezo cha matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma.

Alisema mali za namna hiyo huwafanya viongozi kutaka kung’ang’ania madaraka au kukataa mabadiliko ya katiba, kwa kuwa wanahofia ni kuhojiwa na umma juu ya uhalali wa utajiri huo.

Alieleza mbinu nyingine ambazo zinatumiwa na viongozi kuwanyonya wananchi kuwa ni kuweka kwenye katiba vipengele ambavyo vinawalinda wasihojiwe juu ya mali na utajiri waliojipatia kwa njia zisizo halali walipokuwa madarakani.Alisema Katiba ya sasa inamrundikia Rais madaraka makubwa yakiwamo ya kuteua watu kwenye nyadhifa mbalimbali pasi na kuwapo chombo chochote cha kuhoji hata kama wanaoteuliwa wana historia chafu.

Lakini alisema yeye pamoja na wanaharakati wengine wamekusudia kuhakikisha moja ya mambo yatakayokuwapo kwenye katiba hiyo mpya ni kupunguza madaraka ya Rais.

Katika mchakato wa kuelekea kupata Katiba Mpya, Kibamba alitaja masuala muhimu yanayopigiwa debe na wanaharakati mbali na kupunguza madaraka ya Rais kuwa ni pamoja na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na maadili ya taifa.

Mengine ni kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, muundo wa tawala kuanzia Serikali Kuu, Mikoa na Wilaya, suala la Muungano na adhabu ya kifo.Kibamba alisema mchakato wa Katiba Mpya ukifanikiwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Watanzania kushirikishwa.
Alisema licha ya Katiba ya sasa kuwa na viraka zaidi ya 10 tangu uhuru, wananchi hawakushirikishwa na badala yake kazi hiyo ilifanywa na kikundi cha watu wachache walioteuliwa ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Kibamba alisema hata Tume ya Jaji Kisanga ilipoishauri Serikali mwaka 1998 kuwashirikisha wananchi kwenye mabadiliko ya Katiba, ilionekana ni ushauri usiofaa.

Bunge lanyooshewa kidole
Mjadala huo pia uliligusa Bunge la 10 likidaiwa kwamba limekuwa halitekelezi kazi zake za kutunga sheria za nchi, kama katiba inavyosema.Mjumbe wa PCT, Dk Paul Shemsanga alisema uchunguzi wao umebaini kwamba Bunge limekuwa halitungi sheria, bali ni kupitisha sheria zinazotungwa na Serikali.

“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa Bunge halijawahi kutunga sheria. Serikali ndiyo imekuwa ikitengeneza miswada yote. Kinachofanyika ni wabunge kuhojiwa kwa kusema ndiyo au hapana, mwishowe hupitishwa kwa kauli waliosema ndiyo wameshinda kwa hivyo, umepita,” alisema Dk Shemsanga.
Akielezea juu ya malengo ya mjadala huo, Katibu wa TEC, Padre Antony Makunde alisema ni moja ya mkakati wa kuwaunganisha viongozi wa dini katika kufanikisha mpango wa kuundwa kwa Katiba Mpya nchini.

CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA MAWASILIANO WA KIMATAIFA GENEVA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa, uliofanyika Geneva, Switzerland, Oktoba 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihojiwa na mtangazaji wa Televisheni ya CNN, Becky Underson, baada ya kuhudhuria katika mkutano wa Mawasiliano wa kimataifa uliofanyika Geneva, Switzerland, Oktoba 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano wa India, Kapil Jibal, wakati walipokutana katika ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa, uliofanyika Oktoba 25, Geneva, Switzerland.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa, uliofanyika Oktoba 25, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa, uliofanyika Oktoba 25, Geneva Switzerland, ambapo Tanzania ilikuwa ni moja kati ya nchi zilizoshiriki katika maonyesho ya mkutano huo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KILELE CHA MIAKA 50 YA KITIVO CHA SHERIA/ CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu kilipoanzishwa mwaka 1961. Sherehe hizo zimefanyika leo Oktoba 22, katika Ukumbi wa Nkrumah  Chuo Kikuu jijini. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Naibu Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asharose Migiro, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam leo

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa kwanza wa kike wa Taaluma ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Julie Manning, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam leo
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kitivo cha Sheria, baada ya kutoa tuzo kwa baadhi ya wanafunzi wa zamani wa Taaluma ya Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kitivo cha Sheria, baada ya kutoa tuzo kwa baadhi ya wanafunzi wa zamani wa Taaluma ya Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tuzo mmoja wa wanafunzi wa kwanza wa Taaluma ya Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Miruka Owuor, kutoka nchini Kenya, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1961, zilizofanyika Chuoni hapo
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»