Showing posts with label prof mwandosya. Show all posts
Showing posts with label prof mwandosya. Show all posts

Profesa Mwandosya kurejea Novemba 8




Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya


Na Mussa Juma, Arusha 

WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kurejea nchini Novemba 8, mwaka huu baada ya hali ya afya yake kuimarika nchini India anakopatiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa kimataifa wa wadau wa Rabobank's mjini hapa jana, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, alisema aliwasiliana na Profesa Mwandosya juzi na kumweleza kuwa, afya yake inaimarika tofauti na uvumi ambao unaendelea.

"Kuna maneno mengi kuhusiana na Profesa Mwandosya na Dk Mwakyembe kutokana na kupata maradhi, lakini kikubwa hapa afya zao zimeimarika na nimewasiliana na Profesa Mwandosya atarejea Novemba 8, kabla ya kurejea tena kwenye matibabu Januari mwakani," alisema Sitta.

Sitta alikuwa akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari kuhusiana na kuonekana kuanza kupungua nguvu kundi la wanachama wa CCM ambao wanapiga vita ufisadi.

Hata hivyo, Waziri Sitta alisema hivi sasa vita dhidi ya ufisadi haipiganwi na viongozi wachache pekee, bali kuna wananchi wengi wakiwamo wanaoishi vijijini.

"Vita hii ya ufisadi hatupigani peke yetu, wapo wengi. Tunawasiliana na ingekuwa tupo wachache tusingefika hapa," alisema Waziri Sitta.

Alisema haiwezekani nchi kuachwa mikononi mwa watu wachache waendelee kubomoa urithi wa taifa kutokana na kutaka kuhodhi utajiri na mamlaka.

Waziri Sitta alisema kama ambavyo amekuwa akunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari, vita dhidi ya ufisadi ni endelevu na itakoma pale watuhumiwa watakapowajibika kwa makosa yao.


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WANANCHI WA JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI WAFANYA IBADA YA MAOMBI KUMWOMBEA WAZIRI PROF MWANDOSYA APONE MAPEMA



Prof Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa maji na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.
*****
Na mwandishi wetu
Wananchi wa Jimbo la Rungwe Mashariki wamefanya ibada maalum ya kumwombea Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni  Waziri wa maji Profesa. Mark Mwandosya ili apone haraka.

Baada ya ibada hiyo maalumu mmoja wa wakazi wa jimbo hilo Njwaba Mwakambinda amesema wananchi wa Kijiji hicho wanafarijika wanaposikia taarifa njema kuhusu hali ya afya ya Mbunge wao.

Naye mwenyekiti wa wataalamu mkoa wa Mbeya Prince Mwaihojo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa itikadi zao za kisiasa katika kuleta maendeleo katika Jimbo hilo na kuombeana mema badala ya kutumia siasa kuzushiana vifo.

Akijibu baadhi ya masuala yaliyojitokeza eneo hilo, Msaidizi wa Prof. Mark Mwandosya, Ndigwako Mwasandungila ambaye pia ni diwani wa kata ya Lwangwa amesema mbunge wao anaendelea vizuri na anaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi zake akiwa kwenye matibabu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WANAHABARI WAMTEMBELEA PROFESA MWANDOSYA HOSPITALINI INDIA


Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya akiwa mwenye furaha baada ya kutembelewa na wanahabari kutoka Tanzania walioko India kikazi. Shoto ni Bw. Mike Mande wa gazeti la East African na Bw Gabriel Nderumaki Mhariri wa habari za biashara wa gazeti la Daily News ( wa pili kulia) na kiongozi wa hospitali ya Apollo alikolazwa Prof Mwandosya baada ya kufanyiwa upasuaji wiki kadhaa zilizo
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»