Showing posts with label uvccm. Show all posts
Showing posts with label uvccm. Show all posts

UVCCM waandamana Arusha


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha, James Ole Millya (katikati) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Monduli, Julius Kalanga (kushoto) walipoungana na vijana wa jumuiya hiyo katika maandamano kutoka Makao Makuu ya Polisi mkoani humo kuelekea ofisi ya UVCCM mkoa, jana. Picha na Filbert Rweyemamu

Moses Mashalla, Arusha

KUNDI la wafuasi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha, jana lilizingira uzio wa Makao Makuu ya Polisi mkoani hapa ambako mwenyekiti wa umoja huo, James Milya alikwenda kujisalimisha.Wakati Milya akihojiwa, wafuasi hao wa CCM walibaki nje wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu kiongozi wao huyo.

Wafuasi hao walifika hapo wakimsindikiza Milya kwa maandamano maalumu hali iliyowalazimisha polisi kuwazuia kuingia kwenye lango kuu. Walibaki huku kuendelea kuimba.

Milya aliwasili katika Ofisi Polisi Mkoa wa Arusha saa 6:30 mchana akiwa ndani ya gari aina ya Lexus. Mbali ya kusindikizwa na wafuasi wake hao, pia alikuwapo wakili wake, Moses Mahuna.

Baada ya kushuka kwenye gari hilo akiwa na wakili wake na baadhi ya viongozi wa UVCCM, aliekea moja kwa moja katika ofisi ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa ambako alikaa huko kwa takriban dakika 15 kabla ya kutoka nje na kupokewa kwa shangwe na wapambe wake.

Baada ya Milya kutoka, maandamano makubwa ya kumsindikiza kiongozi huyo yaliyoongozwa kwa magari, pikipiki na baiskeli yalianza. Yalipita kwenye Barabara ya Makongoro kuelekea Makao Makuu ya UVCCM mkoani hapa.

Hata hivyo, kabla ya kufika katika ofisi hizo, wakiwa katika eneo la mzunguko wa Mnara wa Azimio la Arusha, msafara huo ulikutana na gari la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo lililokuwa likitoka katika ofisi hizo za UVCCM. Lilisimama ghafla na kisha mkuu huyo wa mkoa kufungua dirisha kushuhudia maandamano hayo.

Kitendo hicho cha Mkuu wa Mkoa kilikuwa kama kimewazindua waandamanaji hao ambao walilipuka kwa sauti za juu na mmoja wao akisema: “Haturudi nyuma msimamo wetu uko palepale hata viongozi wa Serikali mkituingilia.”

Baada ya kuwasili katika ofisi za UVCCM Mkoa, waandamanaji hao walipigwa butwaa baada ya kukuta ofisi hizo zimefungwa huku katibu wake, Abdallah Mpokwa akionekana kuondoka kimyakimya. Wapambe wa Milya walipiga kelele kutaka ofisi hizo zifunguliwe ili kiongozi wao aingie ndani bila ya mafanikio.
Mpokwa alipohojiwa kuhusu kufungwa kwa ofisi za jumuiya hiyo, alikataa kuzungumza lolote na kutaka aachwe.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi hizo, Milya alisema alijisalimisha polisi baada ya kupata taarifa za kusakwa tangu wiki iliyopita.

Alisema baada ya kufika kituoni hapo, alitakiwa afike tena leo asubuhi kwa kuwa hakuhojiwa kutokana na viongozi wa jeshi hilo kuwa katika shughuli za mwenge wa Uhuru.“Nilipofika pale, polisi wameniambia kuwa nirudi tena leo kwa kuwa kuna shughuli za mwenge mkoani Arusha,” alisema.

Hata hivyo, alisema hajaelewa chanzo cha kuitwa kwake polisi.Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga alilaani kitendo cha polisi kumsaka Milya na kudai kwamba CCM kinapoteza mwelekeo kutokana na mambo ya chama kufikishwa polisi badala ya kumalizikia ndani ya vikao.

“Chama kinapoteza mwelekeo, hakina msemaji. Mambo ya chama yanafikishwa polisi badala ya kwenye vikao vya chama hii ni ajabu,” alisema Kalanga.

Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM Wilaya ya Arusha, Ally Bananga alipinga kitendo cha polisi kumsaka Milya na kusema kuwa huo ni ukandamizaji wa demokrasia ndani ya chama kwa kuwa mambo ya chama yanapaswa kumalizwa ndani ya chama.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

UVCCM IRINGA VIJIJINI WAADHIMISHA MIAKA 12 YA KIFO CHA NYERERE ,KAMANDA WAO AWATAKA WAFANYE KAZI




Vijana wa Chama cha mapinduzi (UV CCM) wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa Leo wameungana na watanzania katika kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere ambaye ametimiza miaka 12 tok a alipotutoka duniani.

Vijana hao wametembea umbali wa zaidi ya kilometa 35 kutoka Kidamali jimbo la Kalenga hadi KIsing,a jimbo la Isimani na kupokelewa na mgeni rasimi kamanda wa UV CCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri (pichani kulia) ambaye amewataka vijana kuepuka kulia ugumu wa maisha kwa kushinda vijiweni na badala yake amewataka kufanya kazi .

Alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa ambayo serikali ya awamu ya nne imeonyesha kwa kuboresha maisha bora na kuongeza ajira kwa vijana ila bado vijana walio wengi wanashindwa kuchangamkia nafasi mbali mbali za ajira na kuendeelea kushinda vijiweni na kulia maisha magumu.

Hivyo alisema wakati umefika kwa vijana kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili kuweza kujitafutia maisha bora badala ya kutegemea kushushiwa neema ya maisha bora.

katika hatua nyingine kamanda huyo wa vijana amewataka vijana wa UVCCM kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli kwa vijana wengine ikiwa ni pamoja na kujkiepusha na matumizi pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya .

Kwani alisema kuwa jitihada zinazofanywa na serikali katika kupiga vita matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya ni vizuri kuungwa mkono na makundi yote ya kijamii huku akisisitiza kuwa vijana ni moja kati ya makundi ambayo yanaathirika zaidi na matumizi ya dawa za kulevya .

Akielezea kuhusu siku hiyo ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa alisema kuwa mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mchapa kazi na kiongozi wa mfano barani Afrika na dunia kwa ujumla kutokana na utendaji kazi wake.

Hivyo alisema njia pekee ya kuendelea kumuenzi baba wa Taifa ni watanzania kufanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwa na uzalendo na Taifa pamoja na kupiga vita maadui watatu kwa maana ya malazi ,ujinga na umasikini kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alivyojitolea kupambana na maadui hao.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KUMBUKUMBU YA MIAKA 12 YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE


KAMANDA wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, Sharik Choughule, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.


KATIBU wa Siasa na Uenezi tawi la CCM, Mchafukoge, akimkumbuka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Msikilize Ridhwan kikwete Akiongea kuhusu wimbo wa Izzo Bizzness..! wa naongea na Ridhwan

Ridhwan Kikwete

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Makundi ya urais 2015 zaitafuna UVCCM

Mussa Juma, Arusha.
MAKUNDI  ya vigogo wanaowania urais mwaka 2015, ndani ya CCM yamezidi kuugawa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), baada ya Kaimu Mwenyekiti wake, Beno Malisa na viongozi wengine wa kitaifa kujikuta wakikwama kufungua matawi ya umoja huo mjini hapa jana.

Malisa aliyekuwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Jamal Ally, mbunge wa vijana CCM, Catherine Magige pamoja na vigogo kadhaa wa umoja huo,  jana walikuwa wazindue matawi 16 ya vijana katika Manispaa ya Arusha, lakini uongozi wa UVCCM wilaya ukagoma.

Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Godfrey Mwalusamba walipinga ujio wa ghafla wa vigogo hao na kufanya kazi ya kuzindua matawi huku uongozi wa umoja huo  wilaya ukiwa hauna taarifa.

Mwalusamba pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya hiyo, walitoa uamuzi huo katika kikao kilichozua malumbano ambacho kilifanyika juzi, ofisi ya UVCCM Mkoa.

Jana, Mwalusamba alithibitisha kupinga kazi ya ufunguaji matawi hayo ya UVCCM kwa maelezo kwamba, walikuwa hawana taarifa za kazi hiyo.

 "Wanasema mimi natumiwa na kundi moja la wanaogombea urais, hapana labda  wao ndio wanatumiwa, itakuwaje wafike hadi wilayani kwangu na kufanya kazi kwenye kata, bila taarifa hata hizo kata hawana taarifa,"alisema Mwalusamba.Kazi ya uzinduzi wa matawi hayo, ulikuwa umepangwa kufanyika katika Kata za Sokone One,Sombetini, Kaloleni, Sekei na Elerai, lakini haikufanyika licha ya kuwa tayari mabango na baadhi ya vijana walikuwa wamejiandaa.


Kauli ya UVCCM Mkoa Arusha 
Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, Ally Benanga ambaye ni mmoja wa waliokuwa waandalizi wa kazi ya ufunguaji wa matawi, alituhumu baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Arusha kutumiwa kukihujumu chama.

"Hawa ni wasaliti, tulikuwa tayari tumewaandaa vijana, tumetengeneza mabango sasa wamegomea, tunajua wanatumiwa na kundi moja la urais na Chadema kudhoofisha CCM Arusha,"alisema Benanga.

          
Hata hivyo, Katibu wa UVCCM  Mkoa wa Arusha, Abdul Mpokwa alipotakiwa kuelezea mtafaruku huo, licha ya kukiri kuahirisha zoezi hilo, lakini alikataa kufafanua zaidi chanzo chake.

"Ni kweli leo (jana) tulikuwa na kazi hiyo ila tumeahirisha na tutaifanya siku nyingine, "alisema Mpokwa.

Katibu huyo, hata hivyo, alikataa kuelezea ni hatua zipi watachukuliwa viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha ambao waligomea zoezi hilo kwa maelezo kuwa walikuwa hawana taarifa.

“Naomba uwasiliane na Katibu wa Mkoa Mary Chatanda yeye ndiye msemaji wetu katika chama,”alisema Mpokwa.

Malisa akana kutumiwa na makundi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, Malisa alikiri kuahirishwa jana kufanyika kazi ya uzinduzi wa matawi hayo kwa kile kilichoelezwa siyo siku nzuri.


Hata hivyo, alisema taarifa alizopewa na mkoa ni kuwa kazi hiyo itafanyika leo huku akikanusha kutumiwa na makundi. "Sidhani hapa kuna  makundi,  ufunguzi wa matawi ni kuimarisha chama na madai kuwa wilaya haina taarifa sisi haituhusu kwani uongozi wa Taifa unawasiliana na Mkoa,"alisema Malisa.


Tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, CCM Mkoa wa Arusha kimekuwa katika vurugu kubwa za makundi ambayo yanadaiwa kusababisha kuangushwa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha, Dk. Batilda Burian.



CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»