MAFUTA BEI JUU

Mwandishi Wetu   
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya  petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepanda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.

"Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye Soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012," ilieleza taarifa hiyo.

Kaguo katika taarifa hiyo alieleza kuwa bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka,  ambapo Petroli imepanda kwa Sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50; Dizeli Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26; na Mafuta ya Taa Sh 67 kwa sawa na asilimia 3.47.

"Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo: Petroli imeongezeka  kwa Sh 291.54 kwa lita sawa na asilimia 15.07; Dizeli Sh 199.57 kwa lita sawa na asilimia 10.68 na mafuta ya taa kwa Sh 67.29 kwa lita sawa na asilimia 3.63," aliseleza katika taarifa hiyo.

Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni mpya iliyopitishwa na Ewura  na kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la Desemba 23, 2011.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

SIRI NZITO ZAANZA KUJITOKEZA KIFO CHA MWANGOSI

POLISI WALIOTEKELEZA OPERESHENI WADAIWA KUSAFIRISHWA KUTOKA MIKOA MINGINE, WAANDISHI WA HABARI IRINGA WASUSIA MKUTANO WA DCI MANUMBA
 
INADAIWA kwamba askari waliokuwa katika operesheni ya kuzuia mkutano wa Chadema katika eneo la Nyololo wilayani Mufindi, Iringa na ambayo ilisababisha kifo cha Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi walitolewa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Mbeya.


Tayari tukio hilo limeibua mjadala mzito kiasi cha kumfanya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kuunda tume huru kubaini chanzo cha tukio hilo. Marehemu Mwangosi alizikwa juzi nyumbani kwao Tukuyu, mkoani Mbeya.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kuwa polisi hao kutoka mikoa hiyo mitatu wakiwa wamesheheni vifaa mbalimbali likiwamo gari la maji ya kuwasha, walisafiri siku moja kabla ya mkutano huo wa Chadema na baadaye kuzuka vurugu zilizosababisha kifo hicho.
Marehemu Mwangosi aliuawa kwa mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu ambao ulisambaratisha vibaya sehemu kubwa ya mwili wake.


Chanzo cha habari kutoka mkoani Dodoma kilisema: “Hapa kwetu kuna askari 10 na tunawafahamu kwa majina. Waliondoka hapa siku moja kabla ya tukio hilo wakiwa na gari la washawasha.”
Chanzo hicho kilisema kwamba awali, hawakuwa wakifahamu kama baadhi ya wenzao walichukuliwa na kupelekwa Iringa. “Tulikuja kuona kwenye gazeti picha na tulipofuatilia tukaelezwa kuwa ni kweli Dodoma ilitoa askari kwenda Iringa.”


Askari mwingine aliyekuwa katika operesheni hiyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma, alikiri kuwa hadi jana baadhi yao walikuwa bado wako Iringa na kwamba walikwenda kwa agizo la wakubwa wake wa kazi.
“Sisi ni Watanzania, lakini tumelazimika kuyafanya hayo kwa sababu ya mkate (malipo). Kwa kweli haikuwa haki, kuwatoa askari na silaha kutoka mikoa mitatu kana kwamba wanakwenda kupigana vita!”


Alidokeza kwamba, askari wote waliotoka Dodoma walikuwa njiani kurudi mkoani humo, jana lakini gari la maji ya kuwasha liliendelea kubaki huko Iringa likiwa na dereva wake na askari mmoja mwenye cheo cha inspekta. Askari huyo alisema kwamba gari hilo lililazimika kubaki kutokana na hitilafu.

“Wengine wamerudi lakini, kuna wengine wenye gari la kuwasha bado walikuwa Iringa, gari lao limepata hitilafu kidogo,” kilisema chanzo hicho kutoka mjini Dodoma.

Mmoja wa askari hao alidaiwa kwamba hiyo inaweza kuwa moja ya sababu ya askari hao kumshambulia marehemu Mwangosi wakati mwenzao anayemfahamu akijaribu kuwazuia. "Hii inaonyesha kuwa askari hao waliompiga walikuwa hawamjui na huyu aliyekuwa akiwazuia, alimjua.”

Makamanda watupiana mpira

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen hakukubali wala kukanusha na badala yake alisema: “Mambo yote hayo yanatakiwa kujibiwa na Kamanda wa Iringa.”
Aidha, alisema sakata la kifo cha mwandishi huyo kwa sasa liko katika vyombo vya uchunguzi hivyo asingekuwa tayari kulizungumzia.


“Siwezi kusema kama askari wangu walikwenda huko au hawakwenda, isipokuwa ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo lipo katika vyombo husika hivyo waachiwe wao au Kamanda wa Iringa ndiye mwenye majibu.”
Alipotajiwa jina la mmoja wa askari aliyeonekana katika picha za video na magazeti za tukio hilo kwamba anatokea katika moja ya vituo vyake, kamanda huyo alisema: “Mimi yakitokea Dodoma nitazungumza wala siyo mtu mwingine kwa hiyo, mambo ya Iringa siwezi kuyazungumza na kama tutaanza kila Kamanda kuzungumza jambo hilo hamuoni kuwa itakuwa ni kama vurugu?”


Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alipopigiwa simu yake iliita tu bila kupokewa.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alisema kwa kuwa tukio hilo limefanywa na polisi, mambo mengi yatazungumzwa lakini akasisitiza kwamba hajapeleka askari Iringa.

Alisema hakukuwa na agizo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wala ombi kutoka Polisi Iringa kutaka askari wa kuongeza nguvu... “Taarifa hizo ni za uzushi kwani hazina ukweli wowote.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani alikanusha pia kuwapeleka askari wake Iringa akisema: “Hizo taarifa siyo za kweli. Hakuna askari yeyote aliyekwenda Iringa wakati wa vurugu zile.”


Mkutano wa DCI wavunjika

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema: “Hayo yote yameundiwa tume ngoja tuiachie ifanye kazi yake.”
Awali, DCI Manumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari mkoani Iringa, ambao hata hivyo, ulivunjika baada ya kutokea kutoelewana baina yao.


Manumba alitaka kueleza ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, lakini waandishi hao walikataa kumsikiliza wakisema hawauamini uchunguzi huo kwa kuwa ulifanywa na polisi peke yao.

Kabla Manumba, hajaanza kuzungumza, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Iringa (IPC), Frank Leonard alisema kutokana na msimamo wa waandishi wa habari wa mkoa huo hakutakuwa na uhusiano wa kikazi na polisi hadi pale tume zilizoundwa kuchunguza kifo hicho zitakapotoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo.

“Msimamo wetu ni kusitisha uhusiano wa kikazi baina yetu na jeshi la polisi hususan Mkoa wa Iringa, tumekuja hapa kwa sababu DCI umetuita na kama unataka kutupa taarifa ya kifo cha ndugu yetu basi waambie hao maofisa wa jeshi wa Iringa watoke nje,” alisema Leonard.

Akijibu madai hayo Manumba alisema: “Nia yangu ni kutoa taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, ndiyo maana niliwasiliana na mwenzenu ili tuweze kuzungumza, Polisi Iringa wataendelea kuwepo na waandishi wa habari mtaendelea kuwepo, matukio kama haya yapo na yataendelea kuwepo.”
Licha ya maelezo hayo, hakuna mwafaka uliofikiwa na mkutano huo ukavunjika.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili baadaye, DCI Manumba alisema: "Ni vyema wao wangenisikiliza kujua ninataka kuwaambia nini. Lakini, kwa kuwa kuna mkanganyiko, nimeona ni vyema jambo hili lisubiri tume ndipo watakuja kulizungumza.”


Waikataa Tume ya Nchimbi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeiponda tume ya Dk Nchimbi kikieleza kuwa imeundwa ili kurudisha uhusiano kati ya Polisi na waandishi wa habari na si kutafuta chanzo cha tatizo.


Juzi, Dk Nchimbi alitangaza kamati ya kuchunguza mauaji hayo inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Steven Ihema na wajumbe, Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, Mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Mtaalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu.

Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alisema Dar es Salaam jana kwamba: “Hii si tume ya kuchunguza mauaji, bali ina lengo la kurudisha uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari ili kuwasahaulisha wananchi kwa sababu imeundwa na waziri ambaye naye anatakiwa kuhojiwa.” “Tunamwomba Rais Jakaya Kikwete ateue tume kama anavyoelekezwa na Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 1992, ambayo inaruhusu kumhoji yeyote kasoro yeye Rais.”

Lissu alisema Rais Kikwete angeunda tume hiyo na Waziri Nchimbi na IGP Said Mwema wanatakiwa kujiuzulu ili kupisha uchunguzi akidai kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba walitoa amri ya mauaji hayo.
“Dk Nchimbi anatakiwa kumuiga Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye alijiuzulu akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kutokea mauaji, akijiuzulu atajijengea heshima tofauti na sasa kwani wananchi wamesikitishwa na mauaji hayo,” alisema Lissu.


Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando alidai kwamba kuna mkakati uliowekwa na Serikali wa kukidhoofisha Chadema baada ya kuonekana kwamba ni tishio kwa CCM.

Mbali na Chadema, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), pia limesema halina imani na kamati hiyo likisema imekuwa kawaida kwa Serikali kuunda tume ambazo hazileti ripoti kwa wananchi.
“Tume zimekuwa zikiundwa bila faida yoyote, huku zikipewa muda kuchunguza yaliyotokea lakini matokeo yake huwa hakuna ripoti wanayorudisha,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya.


Kaaya alisema tume zimekuwa zikiundwa na kuigharimu Serikali fedha nyingi za walipa kodi, lakini ripoti zake zinaendelea kuwa siri.

Imeandikwa na Habiel Chidawali, Dodoma, Hamida Sharrif Morogoro, na Tumaini Msowoya, Iringa na Lasteck Alfred na Juliana Malondo.

Chanzo -
http://www.mwananchi.co.tz
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MANUMBA ASUSIWA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI IRINGA

Wanahabari wa Iringa Wakitoka nje ya ofisi

Wanahabari wa Iringa mchana wa leo wamegoma kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa kifo cha Mwandishi Daudi Mwangosi, aliyeuawa juzi jumapili katika mkutano wa ndani wa Chadema uliokuwa ufanyike katika kijiji cha Nyololo Iringa. Mkuu huyo alikataa shariti la wandishi la kumtaka atoe taarifa hiyo bila kuwepo kwa polisi yeyote katika mkutano huo. Kitendo hicho cha mkuu huyo kukataa shariti  la wanahabari kikapelekea waandishi kutoka nje ya ukumbi huo.Hivyo zoezi hilo kushindikana.

Picha na habari , Said Ng'amilo. Mjengwablog


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

CCM yapumulia mashine




•  AJALI YA MV SKAGIT, URAIS 2015

VYAITESA

na Mwandishi wetu

UPEPO wa mabadiliko ya kisiasa

uliozikumba nchi nyingi duniani,

unaelekea kukiathiri Chama Cha

Mapinduzi (CCM) ambacho sasa

kinahaha kujinusuru kung’oka

madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa

mwaka 2015.

Chama tawala hivi sasa kina

msuguano mkubwa wa kiuongozi

ambapo baadhi ya viongozi wake

wamekuwa wakimshutumu Katibu

Mkuu, Willison Mukama, kwa

kukwamisha mikakati ya kujiimarisha

na kurejesha matumiani yaliyofifia

miongoni mwa wanachama wake.

Licha ya Katibu wa Itikadi na Uenezi,

Nape Nnauye, wiki hii kukanusha

kutokuwa na msuguano na Mukama,

makada wa chama hicho

wamelidokeza Tanzania Daima

Jumapili, kuwa vita ya makundi ya

kuwania uongozi na ile ya ufisadi

inakitesa chama hicho.

Mnyukano wa kisiasa unaonekana

wazi hivi sasa ni baina ya Waziri wa

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa

Kimataifa, Bernard Membe, dhidi ya

kundi linalomuunga mkono aliyekuwa

Waziri Mkuu, Edward Lowassa,

anayetajwa kutaka kuwania urais

katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka

2015.

Wakati hali ya mambo ikionekana

kutokuwa nzuri ndani ya chama hicho,

nguvu kubwa sasa imehamishiwa

kwenye Bunge kwa lengo la

kuwadhibiti wabunge wa CHADEMA

ambao wanaelezwa kutishia uhai wa

chama hicho.

Makada wa CCM wamedokeza kuwa

wamebaini wabunge wa CHADEMA

mwaka 2005-2010 walilitumia vizuri

Bunge kujenga hoja za msingi ambazo

ziliwasaidia kujijenga na hatimaye

kupata wabunge 22 wa majimbo

kutoka watano.

Waliongeza kuwa kutokana na kubaini

jambo hilo, chama hicho kimeamuap

‘kuzishughulikia’ hoja zinazotolewa na

CHADEMA bila kujali kama zina

masilahi kwa taifa au la.

Inadaiwa kuwa viongozi wa Bunge

nao wamepewa maelekezo ya

kukisaidia chama chao hasa

wanapoona kuna hoja zinazoelekea

kuwapatia umaarufu wabunge wa

CHADEMA.

Tanzania Daima Jumapili,

limedokezwa kuwa pamoja na

maelekezo hayo baadhi ya viongozi

wa Bunge wameonekana kushindwa

kukisaidia chama tawala kwa sababu

ya kutozijua ipasavyo kanuni, hivyo

kutumia ubavu kukataa jambo

linalotolewa na wapinzani, hivyo

kuwaongezea umaarufu.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai,

anatuhumiwa kutoa fursa zaidi kwa

wabunge wa CCM kurudia maneno ya

dharau na lugha ya kuudhi dhidi ya

wapinzani.

Kiongozi huyo pia juzi alionesha

‘ukada’ wake pale alipojifanya kukosea

jina la Mbunge wa Viti Maalumu, Rose

Kamili, kwa kumuita Rose Kamili Slaa,

ilhali akijua mbunge huyo

alishatarikiana na Dk. Slaa.

Hata hivyo CCM hivi sasa pia

kinakabiliana na wakati mgumu wa

kushutumiwa kushindwa

kuwachukulia hatua watendaji wake

wanaobainika kufanya uzembe katika

shughuli zao za kila siku.

Ajali ya mv Spice Islanders iliyotokea

mwaka jana na mv Skagit iliyotokea

wiki iliyopita inadaiwa ilichangiwa na

uzembe wa wataalamu kwa

kushindwa kukagua ubora wake.

Serikali ya CCM pia inalaumiwa kwa

kushindwa kuwa na vifaa vya kisasa

vya uokoaji licha ya kila mara

kukumbwa na matukio ya ajali za

baharini na ziwani.

Katika ajali hizo mbili za majini

zilizopoteza maisha ya Watanzania

zaidi ya 400, serikali ya CCM

inalaumiwa kwa kushindwa

kusimamia sheria za usafiri wa majini

na kuficha taarifa ya uchunguzi wa

ajali ya awali.

Mmoja wa wabunge wa CCM ambaye

jina lake limehifadhiwa, aliilaumu

serikali kwa kuunda tume kuchunguza

ajali ya mv Bukoba na Spice Islanders,

lakini haikutoa matokeo ya uchunguzi

huo.

“Serikali iliunda tume kuchunguza ajali

ya awali ya mv Spice Islanders na mv

Bukoba lakini ikaficha matokeo ya

uchunguzi wake. Leo imetokea ajali

nyingine na binafsi naamini kama

matokeo ya uchunguzi wa awali

yangetolewa, bila shaka ajali ya juzi

ingeepukika,” alisema kada huyo.

Kufichwa kwa matokeo ya uchunguzi

wa ajali za awali za majini,

kumeelezwa kuwa ndiyo sababu ya

Spika wa Bunge, Anne Makinda,

kuzima hoja za wabunge wa kambi ya

upinzani walioungana na wabunge

wote wa Zanzibar kutaka kujadili ajali

ya mv Skagit iliyosababisha vifo vya

zaidi ya watu 150.

Chanzo: FreeMedia
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

UTORO WA WABUNGE WAKWAMISHA BAJETI




•  WAPINZANI WANG’ANG’ANIA

ISIPITISHWE

na Salehe Mohamed, Dodoma

UTORO wa wabunge uliokemewa na

Spika wa Bunge, Anne Makinda, wiki

iliyopita jana ulikwamisha kupitishwa

kwa bajeti ya Wizara ya Kilimo,

Chakula na Ushirika.

Wiki iliyopita Makinda alisema utoro

kwa wabunge hivi sasa umekithiri na

akaonya kuwa kama wataendelea na

tabia hiyo ipo siku watakwamisha

upitishaji wa bajeti ya wizara husika.

Utabiri huo wa Spika Makinda, jana

ulitimia baada ya wabunge hasa wa

kambi ya upinzani kuibua hoja ya

kukwamisha upitishwaji wa bajeti ya

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

kwa mwaka 2012/2013 kutokana na

uchache wa wabunge.

Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia

(NCCR-Mageuzi), ndiye aliyekuwa wa

kwanza kutoa hoja kwa kutumia

kanuni ya 112 ambapo alitaka bajeti

hiyo isipitishwe kwa kuwa wabunge

waliopo hawajafikia nusu ya wabunge

wote.

“Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni

inataka Bajeti ipitishwe ikiwa idadi ya

wabunge waliohudhuria itafikia nusu

ya wabunge wote.

“Hapa tulipo mimi nimeshahesabu

mara mbili wabunge wote hatuzidi

110, na tunajua idadi ya wabunge

wote ni 352 na nusu yake ni wabunge

175, ili tutende haki nakuomba

uhesabu idadi ya wabunge waliopo

kabla ya kupitisha bajeti hii ili

tuwatendee haki Watanzania,”

alisema.

Baada ya hapo alisimama Mbunge wa

Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-

Mageuzi) akitumia kanuni ya 77 (1) na

(2) kuwa wabunge waliopo hawafikii

nusu ya wabunge wote.

“Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni ya

77 (1). Akidi kwa kila kikao cha Bunge

wakati wa kufanya maamuzi itakuwa ni

nusu ya wabunge wote, kama

ilivyofafanuliwa katika ibara ya 94 ya

Katiba, isipokuwa kwamba idadi hiyo

haitahusu hoja kuhusu uamuzi wa

kubadilisha masharti yoyote ya Katiba

kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba.

“Mbunge yeyote aliyehudhuria

anaweza kumjulisha Spika kwamba,

wabunge waliopo ni pungufu ya akidi

inayohitajika kwa ajili ya shughuli

inayoendelea.

“Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Naibu

Spika, nasisitiza kuwa hatufiki nusu

humu ndani,” alisema.

Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses

Machali (NCCR-Mageuzi) naye

alisisitiza kanuni hiyo hiyo kipengele

cha tatu. “Endapo Spika ataridhika

kwamba kweli idadi ya wabunge walio

ndani ya Ukumbi wa Bunge ni

pungufu ya akidi inayohitajika basi

atasimamisha shughuli za Bunge kwa

muda atakaoutaja na atamwagiza

katibu kupiga kengele.”

Naibu Spika Job Ndugai, alisema idadi

hiyo inatakiwa wakati wa kupiga kura

ya mwisho ya kuipitisha bajeti hiyo si

wakati wa hatua za awali za kamati ya

matumizi.

Kauli hiyo ilimfanya Mnadhimu wa

Kambi Rasmi ya Upinzani, Tundu

Lissu, asimame na kutaka kiti cha

Spika kisiliburuze Bunge kwa kukiuka

kanuni na kuliomba Bunge liahirishe

shughuli hiyo.

Hata hivyo Ndugai hakukubaliana na

kauli ya Lissu. Ndugai huku akisema

kuahirisha shughuli za Bunge ni

gharama kubwa, alichukua muda

kuamua jambo hilo.

Ndugai aliamuru Kamati ya matumizi

iendelee huku Waziri wa Nchi Ofisi ya

Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),

William Lukuvi, alitoka nje

kuwahamasisha wabunge warejee

ukumbini. Mbali na juhudi za Waziri

Lukuvi pia kengele ilikuwa ikipigwa nje

ya ukumbi wa Bunge kuwahamasisha

warejee ukumbini.

Juhudi zakwama

Pamoja na jitihada za viongozi

mbalimbali wa serikali na Bunge

kuhakikisha idadi ya wabunge inafika

nusu, jambo hilo lilishindikana na

ndipo Ndugai alipoamua kuahirisha

shughuli za Bunge.

“Ni Vizuri wananchi waelewe kuwa

tuna huu msiba wa kitaifa

unaoendelea Zanzibar kuna wabunge

wenzetu wako kule Zanzibar hasa

kutoka Zanzibar kwa ruhusa ya

Spika…, kuna mawaziri na manaibu

wapo kule na wengine wako kule kwa

shughuli maalumu.

“Kuna wabunge kadhaa ambao mimi

mwenyewe nimewaruhusu wapo

kwenye msiba wa mazishi ya mama

wa mbunge mwenzetu, Mike Lekule

Laizer (CCM).”

Wakati Ndugai akiendelea kutoa

ufafanuzi huo, wabunge wa upinzani

walikuwa wakitoa kauli na kugonga

meza kuonesha kupinga utetezi huo.

Vitendo hivyo vilimfanya Ndugai

kuwataka wamsikilize badala ya kupiga

kelele ambazo haziwasaidii, kwakuwa

kiti cha Spika hakiwezi kumkandamiza

mtu.

“Nawaombeni ndugu zangu

tunaposikilizana kama watu wazima…

tupeane nafasi, mnalolitaka litakuwa

…..mkisema nyinyi nawapa

nafasi….mimi nikisema mnaanza

kupiga kelele.

“Inanisikitisha sana tunapovunjiana

heshima, tunakuwa kama watoto

wadogo, mimi sidhani kama

inatujengea heshima mahali popote

katika nchi yetu, tunafanya jambo la

msingi la taifa,” alisema.

Alisema kwa busara alizonazo

ameamua kuahirisha kikao hicho,

hatua ya kamati ya Bunge zima hadi

Jumatatu (kesho).

Baada ya kauli hiyo wabunge wengi

hasa wa upinzani walikuwa wakipiga

meza kwa kushangilia ‘ushindi’

walioupata.

NCCR-Mageuzi wakomalia

Mara baada ya Bunge kumalizika

wabunge wa NCCR-Mageuzi

walikutana na waandishi wa habari na

kuweka bayana kuwa hivi sasa

wanafanya uchunguzi kujua ni vikao

gani vilifanyika bila idadi ya wabunge

kutimia, baada ya hapo wapeleke hoja

kutaka maamuzi yaliyofikiwa

yatenguliwe.

Mbunge wa Kasulu Kusini, David

Kafulila, alisema maamuzi mengi

yamekuwa yakifanywa bila akidi

kutimia, jambo ambalo ni hatari kwa

maendeleo ya taifa.

“Tutaomba Spika atupe orodha ya

wabunge waliohudhuria katika kikao

hiki cha Bajeti na tukibaini tutaomba

maamuzi yaliyoafikiwa yatenguliwe,”

alisema.

Chanzo FreeMedia
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rais Kikwete Akutana na Kufanya Mazungumzo na Profesa Ntumra Luaba Alphonce, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu wa (International Conference on Great Lakes Region ICGLR) mjini Bujumbura, Burundi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amesema kuwa
hali ya mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC)
inatia wasiwasi na hivyo Tanzania
inafuatilia kwa makini hali
inavyoendelea katika eneo hilo la
nchi hiyo jirani.

Aidha, Rais Kikwete amesema
kuwa Tanzania ingependa kuona
hali ya amani inarejea katika DRC
kwa sababu nchi hiyo inahitaji
kupata muda wa amani ili
waelekeze nguvu zake kwenye
maendeleo badala ya kupigana.
Rais Kikwete amesema hayo jana,
Jumanne, Juni 3, 2012, wakati
alipokutana na kufanya
mazungumzo na Profesa Ntumra
Luaba Alphonce, Katibu Mtendaji
wa Umoja wa Nchi za Maziwa
Makuu wa International
Conference on Great Lakes Region
(ICGLR) kwenye Hoteli ya Roca
Golf mjini Bujumbura, Burundi.
Rais Kikwete akifuatana na Mama
Salma Kikwete alikuwa mjini
Bujumbura kushiriki katika
Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa
Burundi na kurejea nyumbani jana,
3 Juni, 2012. Kabla ya kuja hapa,
Rais Kikwete alikuwa mjini Kigali,
Rwanda, kushiriki katika sherehe
za namna hiyo zilizofanyika Julai
Mosi, mwaka huu. Rwanda na
Burundi zilipata uhuru kutoka kwa
Wabelgiji Julai Mosi na Julai 2,
mwaka 1962.

Rais Kikwete amemwambia Katibu
Mtendaji huyo: “ Kwa hakika hali
mashariki mwa Congo inatutia
wasiwasi mkubwa na Tanzania
inafuatilia kwa makini hali hiyo.
Congo imekuwa katika vita muda
mrefu kupita kiasi kwa sababu
tokea mwaka 1997 imekuwa katika
vita mfululizo.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Wakati
umefika kwa Congo kutulia ili
nguvu inayoingia katika
mapambano na vita ielekezwe
katika maendeleo ya wananchi wa
nchi hiyo.”

Rais Kikwete pia ameunga mkono
wazo la kuitishwa kwa mkutano
wa mawaziri wa nchi wanachama
wa ICGLR ili kujadili hali ilivyo
katika mashariki mwa Congo
kufuatia ombi la DRC kutaka
kuitishwa kwa mkutano huo.
Hali katika mashariki mwa Congo
imeanza kutia wasiwasi baada ya
kikundi cha waasi wa Serikali ya
nchi hiyo wakiongozwa na jambazi
la kivita John Bosco Ntaganda
kuanza tena harakati zake za
kivita dhidi ya Serikali ya Rais
Joseph Kabila.

Usiku wa jana, Jumanne, Julai 3,
2012, alikutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa
DRC,Mheshimiwa Kabila kuhusu
hali ilivyo mashariki mwa DRC.
Wakati akiwa Kigali,
Rwanda,mwishoni mwa wiki, Rais
Kikwete pia alikutana na kufanya
mazungumzo na Rais Paul Kagame
kuhusu hali ilivyo mashariki mwa
DRC.

Aidha, usiku huo huo wa kuamkia
jana, Rais Kikwete alikutana na
kufanya mazungumzo na Naibu
Waziri Mkuu wa Ubelgiji,
Mheshimiwa Didier Reynders
ambaye pia anahusika na masuala
ya nchi za nje, biashara ya nje na
masuala ya Umoja wa Ulaya (EU).
Katika mazungumzo Rais Kikwete
na Mheshimiwa Reynders
walizungumzia hali ya mashariki
mwa Congo pamoja na mchakato
wa ushirikiano ndani ya Jumuia ya
Afrika Mashariki (EAC).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Julai, 2012


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WAZIRI WA USALAMA NA ULINIZI KENYA PROF. GEORGE SAITOTI AFARIKI KWA AJALI YA HELIKOPTER


Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.

Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.


Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika. Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.


Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KIWANDA CHA NYUKI KIBAHA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo baada ya kufunguza kiwanda cha kusindika asali cha  Organic Honey katika kijiji cha Visiga  mkoani Pwani  kinachomilikiwa na Kampuni ya  Boleyn  International, Juni 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»