Showing posts with label ajali mbeya. Show all posts
Showing posts with label ajali mbeya. Show all posts

MMOJA AFA KWA KUKOSA HEWA SAFI WAKATI AKICHIMBA KISIMA CHA FUTI 96 MKOANI MBEYA.

Wakazi wa kata ya Iyela mtaa wa Airport wakifanya jitihada za kuokoa maisha y
a Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Igale wilayani 
Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa na mauti wakati akichimba kisima 
chenye futi 96 kipenyo cha futi 2.
Dada wa marehemu Fraida Mwashozya akiwa akipewa msaada baada ya kuutambua 
mwili wa marehemu na mmoja wa wakazi wa Iyela waliofika eneo la tukio kuokoa
 maisha ya marehemu aliyefariki wakati akichimba kisima cha futi 96 na kipenyo 
cha futi 2.
Mwili wa marehemu Fraida Mwashozya ambaye amefariki wakati akichimba 
kisima chenye kicha cha futi 96 na kipenyo cha futi mbili,
Bwana Mwanyelele ambaye alizirai wakati alipojaribu kwenda kuokoa mwili wa marehemu Fraida.
Kikosi cha Zima moto mkoani Mbeya kikitumia huduma ya hewa safi, kujaribu
kunusuru kifo cha marehemu Fraida. 
***** 

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Licha ya juhudi za wakazi wa kata ya Iyela mtaa wa Air Port jijini Mbeya kujaribu kuokoa maisha ya Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Igale wilayani Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa na mauti.

Juhudi hizo zilifikia kikomo majira ya saa 11 jioni pale mwli wake ulipoibuliwa kutoka katika kisima hicho akiwa amefariki, juhudi za uokozi zilianza majira ya asubuhi kuanzia saa moja na dakika arobaini na tano ambapo marehemu mbaye alikuwa akichimba kisima chenye urefu wa futi 96 na kipenyo cha mzunguko futi 2 kazi iliyofanyia kwa siku moja wakati akitaka kumridhisha mwajiri wake aliyemwagiza kukichimba kisima hicho.

Inaelezwa kuwa Fraida Mwashozya na mwenzake Nesco Mwamlima mwenye umri wa miaka 23 walipewa ajira ya kuchimba kisima chenye urefu wa futi 96 bwana Piusi Simchimba mwenye umri wa miaka 64 kwa ujira wa shilingi elfu 55 ambapo baada ya kumaliza waliambiwa hawatoweza kulipwa hadi watakapo ongeza urefu wa kisima hicho.

Tukio hilo la kutumbukia kwa Fraida limetokea jana majira ya saa moja za asubuhi lakini Jeshi la polisi, kikosi cha uokoaji na wakazi wa eneo hilo wameshindwa kumuokoa na kwamba jitihada za kutumia watu kuingia kisimani humo zimeshindikana kutokana na kukosekana kwa hewa kisimani humo.

Aidha watu wawili Nesco Mwamlima na Juma Mwanyeyere walipojaribu kuingia kwenye kisima hicho kumuokoa nao walishindwa kutokana na kuhishiwa hewa lakini wao waliokolewa na afya zao zinaendelea vizuri.

Afisa mtenda wa kata ya Iyela Ezekiel Kipako amesema zoezi la uokoaji limemalizika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

HABARI MPYA: Ajali Nyingine Yatokea Mbeya LEO







Maiti ikinasuliwa kutoka kwenye moja ya magari yaliyopata ajali katikaeneo la pipeline mkoani Mbeya, ajali hiyo imetokea hivi punde. Tutawaletea taarifa juu ya chanzo na mengineyo kadiri taarifa zitakavyokua zinatufikia.
Habari kwa hisani ya Mjengwa blog
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WATU 30 WAJERUHIWA NA HAKUNA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSUSHA MAGARI MANNE MKOANI MBEYA


Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika ajali mbaya na hakuna aliyefariki iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Baadhi ya majeruhi kati majeruhi 30 wakiwa wameketi chini, wakiwaweshikwa na butwaa kushindwa kuamini kile kilichotokea baada ya kutoka salama katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo hakuna aliyefariki lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Mashuhuda waliofika eneo la ajali ambapo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Moja kati ya malori matatu yaliyosababisha ajali na kuziba barabara na hali iliyopelekea magari mengine kushindwa kupita  katika ajali mbaya, ambayo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali hiyo iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»