Showing posts with label ccm. Show all posts
Showing posts with label ccm. Show all posts

MAFISADI CCM WAKALIA KUTI KAVU

*Mkakati wa kuwamaliza kidiplomasia yatajwa
*JK alikwepa mtafaruku,kupisha upepo mbaya

Na Mwandishi Wetu

SIKU tatu baada ya kumalizika kwa vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma wiki iliyopita, upepo mbaya umeanza
kuwaelekea watuhumiwa wa ufisadia ndani ya chama hicho wanaotakiwa kujivua magamba kwa kutafakari wenyewe tuhuma zao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Hali hiyo inatokana na siri nzito kutoka ndani ya vikao hivyo kueleza kuwa mbinu iliyotumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, kurudisha suala hilo kuamuliwa na Kamati ya Maadili kisha kuwasilisha maamuzi yake kwa Kamati Kuu unalenga kuwamaliza kabisa watuhumiwa hao.

Imeelezwa kuwa syahili hiyo mpya iliyotumika mjini Dodoma haikulenga kufuta mchakato wa kuwaondoa watuhumiwa haoa kama ilivyodaiwa bali ulilenga kuepusha malumbano ndani ya kikao baada ya kubainika kundi hilo kuandaa watu wao kuwatetea kwanguvu kubwa na kuwa tayari hata kuchafua hali ya hewa.

Taarifa zilizoifikia Majira juzi na jana, vinaeleza kuwa baada ya kundi hilo kudaiwa kuwa na wafuasi wengi ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), washauri wa masuala ya kisiasa ndani ya CCM walitaka Kamati ya Maadili imalize suala hilo kukwepa mjadala mzito kutokana na wahusika kuwa na kundi kubwa la kuwatetea.

"Kilichotakiwa watu waelewe tangu mwanzo ni kwamba CCM kama chama ni wajanja kuliko kundi la mafisadi, wale jamaa walijiandaa na wana wafuasi na kundi kubwa ndani ya NEC, kuwamaliza mle ni tatizo kubwa.

"Njia pekee wa kuwamaliza ni kuwaachia Kamati ya Maadili ambako mle kuna wajumbe wachache na wenye msimamo thabiti na wanaoijua vizuri chama, kama mnafikiri kujivua gamba imefikia mwisho subirini mtaona matokeo, Kamati inakwenda kumaliza kila kitu,"kilisema chanzo chetu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Rais Kikwete baada ya kuona hali halisi na kupewa taarifa za siri za jinsi kundi hilo ilivyojipanga kupambana kufa na kupona alishauriwa na wakongwe mbalimbali wa kisiasa kumaliza suala hilo kwa njia ya diplomasia na kwamba hakuna atayelaumiwa.

"Kamati ya Maadili ikishamaliza itawasilisha maamuzi yake ambayo kwa lugha ya diplomasia ya chama huitwa mapendekezo, Kamati Kuu itabariki maamuzi hayo na hapo ndio mwisho wa hatua hiyo watafuata wengine," kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Majira ilipomtafuta Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, kuthubitisha taarifa hizo alisema yupo kwenye kikao na kuahidi kutoa ufafanuzi baada ya kumaliza. Hata hivyo hadi tunakwenda mtamboni kiongozi huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa maeleoz kuwa bado anaendelea na kikao.

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ni Mwenyekiti wa Taif Rais Jakaya Kikwete, Makamu Bara Bw. Pius Msekwa, Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Iddi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. John Chiligati, Vuai Ali Vuai.


Kwa mujibu wa taratibu za CCM Kamati ya Maadili inaweza kuchukua hatua moja kwa moja au kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu (CC) ambayo pia wajumbe wake karibu wote wanaingia pia kuyabariki.

Katika kikao cha NEC cha wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejizulu Bw. Edward Lowassa, alilalamika kuchafuliwa huku Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumate, alitaka majibu ya sababu zinazofanya wanaochafua Bw. Lowassa kutochukuliwa hatua kama hana kosa.

Suala la kujivua gamba ndani ya CCM imeleta mwamko mpya wa kimtazama ndani ya CCM huku kundi moja linalojipambanua kuwa na msimamo wa kimaadili ikielezwa kuusimami na upande wa pili ukieleza kuwa ni mchakato unaokivuruga chama hicho kwa madai kuwa hakuna ushaidi wa magamba yanayotakiwa kuvuliwa.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

LOWASSA, SUMAYE WAONGEA CCM


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Andrew Chenge (kushoto) na Edward Lowassa wakipeana mikono baada kutoka katika kikao cha NEC, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi




WALIA KUCHAFULIWA NA MAKADA WENZAO,NEC YARIDHIA GAMBA KUREJESHWA CC
Habari na Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma.
******



MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji.

Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?”Sumaye alinukuliwa akihoji.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: “Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu”.

Richmond yatajwa
Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.

Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC

Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.
Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho.
Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi.

Kujivua gamba
Kufuatia uamuzi huo wa NEC hivi sasa mpango wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho, Aprili mwaka huu unarejeshwa CC ambapo watuhumiwa wote wa makosa mbalimbali watafikishwa mbele ya Kamati za maadili na kuchukuliwa hatua kwa taratibu za chama hicho.

Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho na sasa unarejeshwa Kamati Kuu (CC) ili ichukue hatua zaidi kwa wale waliogoma kujiuzulu.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo ukimya ambao unaashiria kutokuwapo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari yao kama ilivyotarajiwa.

Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa.

Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.

Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: “Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja”.

Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: “Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho”.

Nec yawakaanga kina Jairo
Katika hatua nyingine, NEC imeunga mkono hatua zilizopendekezwa na Bunge dhidi ya watumishi wa umma waliotajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoanika uozo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma ndani ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kamati hiyo katika ripoti yake iliyowasilishwa mwishoni mwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, iliwataja Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyesimamishwa), David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba wanastahili kuchukuliwa hatua.

Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, huku wabunge wakipendekeza pia kuondolewa madarakani kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

NAPE AKISALIMIANA NA WAZEE WA CCM


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC, Bw. Edward Lowassa. wakati wa kikao cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma jana. Kulia kwa Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Fredrick Sumaye na Bw. Kingunge Ngombale Mwiru (kulia)
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JANA MJINI DODOMA

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, kutoka kushoto: Mheshimiwa Sophia Simba,Capt John Chiligati na January Makamba wakiteta jambo ndani ya ukumbi wa CCM wa White House kabla ya kuanza kwa kikao chao jana.


Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa CCM wa White House Mjini Dodoma jana.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

CCM KWACHAFUKA


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa, wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi


UVCCM WAPANGA KUASI, NI HOFU YA KUFUTWA KWA UMOJA WAO

Habari Na Neville Meena, Dodoma

HALI imezidi kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.Hatua ya viongozi wa UVCCM kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini Dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni “kupigania umoja wao na chama chao,” imezidi kuchafua hali ya hewa.

Taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kamati Kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo Rais Kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na Kikwete.

Juzi usiku, wenyeviti wa UVCCM kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la Area D mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa UVCCM utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja Chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM na wale wa Baraza Kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe NEC ya CCM iwapo wataridhia kufanya hivyo.

Kauli za viongozi
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambaye hakupenda kuandikwa jina gazetini alisema hakuna mpango wa kufuta UVCCM na kuziita taarifa hizo kuwa ni za kupika.

Kauli yake iliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema: “Hakuna kitu kama hicho, mimi ni mshiriki wa vikao vyote vya Sekretarieti hakuna ajenda hiyo kwenye vikao vyetu hivi.”

“Ndiyo maana kwenye mkutano na waandishi wa habari nimesema kwamba watu waache kupandikiza vitu ambavyo kimsingi havipo, vikao hivi ni vya kawaida na ajenda zimewekwa wazi, sasa kama kuna watu wanaleta hizi hoja, basi wana malengo yao tu.”

Mapema Nape akizumgunza na waandishi wa habari alisema kumekuwapo na taarifa nyingi zinazowafanya Watanzania kutaharuki kana kwamba kuna vita inayotarajiwa kutokea mjini hapa.

“Naomba wanahabari wenzangu, nisaidieni maana haya yote yanatokana na taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari, lakini ajenda zetu kama nilivyosema jana (juzi) zinafahamika, kubwa ni kupitia utekelezaji wa mabadiliko ndani ya chama chetu,” alisema Nape.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema hana taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa mpango wa kufutwa kwa umoja huo ambao yeye ni mtendaji wake mkuu na kwamba hata katika kikao cha sekretarieti ambacho yeye ni mjumbe hakukuwa na ajenda ya aina hiyo.

Hata hivyo, Shigela hakuwa tayari kuweka bayana iwapo alifahamu mkusanyiko wa viongozi wa UVCCM kutoka mikoani waliopo Dodoma, zaidi ya kusisitiza kwamba kipindi hiki ni cha kutulia kwa wana CCM kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingine ambazo wakati mwingine vyanzo vyake si bayana.

Chimbuko la hisia
Chimbuko la hisia za kufutwa kwa UVCCM ni taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya vikao vya Kamati ya Maadili ambayo katika siku yake ya kwanza iliwahoji baadhi ya viongozi wake akiwamo Kaimu Mwenyekiti, Benno Malisa.

Wengi walihojiwa kuhusu utendaji wa kamati ya kutathmini upya uendeshaji wa UVCCM, ambayo tayari imefanya kazi yake katika mikoa 19 ya Tanzania Bara. Kamati hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Baraza Kuu ya UVCCM, Hussein Bashe, inatuhumiwa kuendesha mikutano iliyotumika kuwakashifu viongozi wa juu wa CCM wakiwamo Mwenyekiti Kikwete na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

“Kuna taarifa za uhakika kwamba ajenda hii haikupitia kwenye sekretarieti, inatoka kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma kwamba eti sehemu kubwa ya UVCCM tuko nyuma ya kundi moja ndani ya chama,” alisema mmoja wa wenyeviti wa umoja huo na kuongeza:

“Sasa mpango wao ni kufuta viongozi wote wa kuchaguliwa na baada ya hapo waandae uchaguzi mwingine ili kuwaweka viongozi wanaowataka, sasa hili sisi tunasema hapana kama ni tatizo litatuliwe lakini wasituulie umoja.”

Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu alisema jana kuwa taarifa kwamba UVCCM inafutwa zimezagaa katika ofisi hizo lakini bado zilikuwa hazijathibitishwa kutokana uamuzi wa vikao vya Kamati ya Maadili kufanywa kwa siri kubwa.

Mkakati wa Kupinga
Taarifa za mpango huo ndizo zilizowatia wazimu UVCCM kiasi cha kuitana Dodoma kwa lengo la kukabiliana na NEC ikiwa ‘itathubutu’ kuubariki.

Habari kutoka ndani ya kikao cha juzi usiku zinasema wenyeviti hao walikubaliana kwa kauli moja kuwaita wenyeviti wa wilaya wa umoja huo wa vijana ili kuongeza nguvu za kuwakabili wakuu wa CCM.

Mmoja wa wenyeviti kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki alisema juzi usiku kwamba: “Katika hili tumejipanga, tunao vijana zaidi ya 300 wapo kambini, tutawaleta hapa, tutaungana nao kupinga uamuzi huu.”

Harakati za UVCCM zinakwenda sambamba na kupinga utekelezaji wa mpango wa kujivua gamba ambao wanasema unatekelezwa kwa upendeleo ukiwalenga baadhi tu ya watu.

Mmoja wa viongozi hao alinukuliwa na chanzo chetu akisema wanaopaswa kufukuzwa au kuchukuliwa kwa hatua na CCM ni makada ambako Rais Kikwete alipata kura chache wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Kwa mantiki hiyo, vijana hao walisema mpango wa kujivua gamba hauna tija kwa sasa kwani unakigawa chama na kwamba CCM kina matatizo makubwa zaidi kinayopaswa kushughulikia badala na siyo kuchochea chuki miongoni mwa wanachama wake.

Maazimio ya NEC
NEC inakutana miezi minne tangu kilipokutana mara ya mwisho na kutoa maazimio ambayo yalisababisha mmoja wa makada wake, Rostam Aziz kujiuzulu ubunge katika Jimbo la Igunga pamoja na ujumbe wa NEC.

Rostam katika kujiuzulu huko aliitupia lawama sekretarieti ya chama hicho kwa kile alichokiita kuwa ni kuendesha siasa chafu dhidi yake na kuwataja kwa majina Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, John Chiligati na Nape kuwa wahusika.

Kujiuzulu kwa Rostam ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi katika mjadala wa CC na NEC.

Katika mazingira hayo, kuna kila uwezekano wa kutathmini jinsi falsafa ya kujivua gamba ilivyotekelezwa. Kuna madai kwamba Sekretarieti inayoongozwa na Mukama nayo imegawanyika katika suala la utekelezaji wa uamuzi wa NEC, hali inayoongeza sintofahamu ndani ya chama hicho.

CHANZO: Mwananchi
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MH. LOWASSA ACHANGISHA MIL 200 UJENZI WA KANISA KATOLIKI NYAKATO,MWANZA


Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa kanisa Katoliki Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu la Mwanza jana kabla ya kuendesha haranbee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kubwa kuliko yote Kanda ya Ziwa ujenzi ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 700.Litakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa wakati.Katika harambee hiyo zilikusanywa shilingi milioni 200 ikiwa ni zaidi ya mahitaji ya shilingi milioni 120.



Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Mara, Mh. Christopher Mwita Gachuma (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa, kushoto ni aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Lawrance Masha.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Mara, Mh. Christopher Mwita Gachuma (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa, kushoto ni aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Lawrance Masha.



[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Profesa Mwandosya kurejea Novemba 8




Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya


Na Mussa Juma, Arusha 

WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kurejea nchini Novemba 8, mwaka huu baada ya hali ya afya yake kuimarika nchini India anakopatiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa kimataifa wa wadau wa Rabobank's mjini hapa jana, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, alisema aliwasiliana na Profesa Mwandosya juzi na kumweleza kuwa, afya yake inaimarika tofauti na uvumi ambao unaendelea.

"Kuna maneno mengi kuhusiana na Profesa Mwandosya na Dk Mwakyembe kutokana na kupata maradhi, lakini kikubwa hapa afya zao zimeimarika na nimewasiliana na Profesa Mwandosya atarejea Novemba 8, kabla ya kurejea tena kwenye matibabu Januari mwakani," alisema Sitta.

Sitta alikuwa akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari kuhusiana na kuonekana kuanza kupungua nguvu kundi la wanachama wa CCM ambao wanapiga vita ufisadi.

Hata hivyo, Waziri Sitta alisema hivi sasa vita dhidi ya ufisadi haipiganwi na viongozi wachache pekee, bali kuna wananchi wengi wakiwamo wanaoishi vijijini.

"Vita hii ya ufisadi hatupigani peke yetu, wapo wengi. Tunawasiliana na ingekuwa tupo wachache tusingefika hapa," alisema Waziri Sitta.

Alisema haiwezekani nchi kuachwa mikononi mwa watu wachache waendelee kubomoa urithi wa taifa kutokana na kutaka kuhodhi utajiri na mamlaka.

Waziri Sitta alisema kama ambavyo amekuwa akunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari, vita dhidi ya ufisadi ni endelevu na itakoma pale watuhumiwa watakapowajibika kwa makosa yao.


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

CCM sasa wahaha kujinusuru

Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) Steven Wassira





Peter Saramba, Arusha

MSUGUANO wa kisiasa ndani ya CCM ambao umekitikisa chama hicho siku chache zilizopita umechukua sura mpya, na sasa chama hicho kinamtumia kada wake mkongwe, Steven Wassira kuanza harakati za kutatua mgogoro huo.Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), yupo Arusha ambako jana alianza mchakato wa vikao vinavyowashirikisha viongozi na baadhi ya makada wa chama hicho wa Wilaya na Mkoa wa Arusha, eneo ambalo limekuwa kitovu cha vurugu zinazoonekana kukitikisa CCM hadi ngazi ya taifa.

Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana, CCM Arusha kimegeuka kuwa kitovu cha vurugu na mpasuko unaotikisa chama hicho na Umoja wake wa Vijana (UVCCM).

Wassira ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha, alifanya kikao na UVCCM mkoani humo ambacho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Shigella.

Vyanzo vya habari vilidokeza kwamba, katika siku yake ya kwanza ya ziara mkoani hapa, Wassira jana alikutana na UVCCM Wilaya ya Arusha ikiwa ni mwanzo wa safari hiyo ya kusaka suluhu.

Wassira aliyewasili Arusha juzi, katika kikao chake hicho alikutana na wajumbe wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arusha katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Youth League eneo la Faya, ambako vijana hao walimtaka kutumia nafasi yake ya ulezi na uwaziri kukutana na pande zote zinazonyukana kutafuta ufumbuzi kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Pamoja na kujadili mgogoro ulioko kati ya makundi ya vijana ambao uongozi wake wilayani Arusha chini ya Godfrey Mwalusamba unadai unachochewa na mwenyekiti aliyepita, Ally Bananga, kikao hicho pia kilijadili ziara ya Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa iliyopingwa na kususiwa uongozi wa Mwalusamba.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa, Wassira alielezwa na vijana hao wakiongozwa na mmoja wa wajumbe aliyetajwa kwa jina la Mussa Daudi Lungo kwamba tatizo la UVCCM na chama hicho kwa ujumla ni harakati za urais 2015 zinazohusisha baadhi ya makada, viongozi na wanachama.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, zaidi ya nusu ya wajumbe wa kikao hicho walimuunga mkono Mwalusamba katika kila hoja aliyotoa.

Kauli ya Wassira
Akihitimisha kikao hicho, Wassira aliahidi kuchukua maelezo yatakayotolewa na pande zote kwa ahadi kwamba atayawasilisha kwenye Kamati Kuu (CC) ya CCM inayotarajiwa kukutana siku chache zijazo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alithibitisha ujio wa Wassira na kwamba ziara hiyo ni ya kawaida katika kuimarisha chama na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Chatanda aliyezungumza kwa simu jana jioni, alisema Wassira alitarajiwa kukutana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya leo asubuhi kukutana na wajumbe wa baraza la vijana mkoa na kuhitimisha kwa kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa mchana.

“Kama mjumbe wa NEC (Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM) na mlezi wa chama mkoa, atafanya (Wassira) vikao na ngazi mbalimbali ya uongozi wa chama na jumuiya zake na kwa sababu hii ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mlezi wetu, tutampa taarifa ya hali ya mkoa kisiasa,” alisema Chatanda.
Ingawa Chatanda hakutaka kuzungumzia kwa undani maudhui ya ziara hiyo iliyokuja kukiwa na fukuto na minyukano kati ya makundi yanayodaiwa kuchochewa na harakati za urais 2015, moja kati ya ajenda muhimu ya vikao vya waziri huyo ni kutafuta chanzo, sababu na ufumbuzi wa migogoro ya mara kwa mara miongoni mwa viongozi na wana CCM Arusha.

Migogoro ilikoanzia
Katika siku za karibuni, Arusha imegeuka kuwa chimbuko la vita ya maneno miongoni mwa makada wa CCM, hulka ambayo imesambaa hadi kwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Tuhuma za hivi karibuni ni zile zinazomtaja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwamba amekuwa akikivuruga chama hicho kutokana na jinsi anavyopigia chapuo utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba.

Wanaopinga falsafa hiyo wanasema inatumika vibaya kuwabana watu wenye nia ya kuwania urais wa 2015 lakini Nape mara kadhaa amekanusha kutokuwa na lengo hilo.

Awali, mgogoro ulikuwa baina ya baadhi ya vijana wilaya na mkoa wa Arusha na katibu wa CCM Mkoa, Chatanda ambaye pamoja na viongozi na makada wengine walituhumiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kusababisha chama hicho kipoteze kiti cha ubunge wa Arusha Mjini.

Katikati ya mwaka huu baada ya kikao cha NEC, mkoa huo ulitoa onyo kali kwa baadhi ya vijana waliohusishwa na mvutano huo, akiwamo Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, James Ole Millya aliyedaiwa kumtolea Chatanda maneno makali.

Wakati hali ikionekana kutulia, mgogoro mwingine mpya umeibuka mwezi huu na safari hii ukitanuka hadi kuhusisha viongozi wa UVCCM Taifa akiwamo Malisa, baada polisi kuwanyima kibali kufungua matawi na kufanya mikutano ya hadhara.
Hata hivyo, vijana hao walikaidi amri ya polisi na kuendelea na ratiba yao ambayo ilihitimishwa kwa mkutano wa hadhara ambao waliutumia kumtuhumu mtu waliyemwita mtoto wa kigogo wa chama na Serikali kwamba ndiye alitoa maelekezo ya wao kunyimwa kibali cha polisi.

Siku chache baadaye, polisi walitangaza kumsaka Ole Millya ili wamhoji juu ya tuhuma hizo lakini tangu alipojisalimisha, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na jeshi hilo kuhusiana na mahojiano hayo.

Wakati polisi wakiwa kimya, Ole Millya alitoa taarifa ndefu yenye kurasa 12 ambayo pamoja na mambo mengine, alirejea na kusisitiza kuwa wapo watoto wa vigogo wa chama na Serikali wanaotumia madaraka ya wazazi wao kuvuruga UVCCM na kuingilia baadhi ya utendaji serikalini.



CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KATIBU MKUU WA UVCCM ALAANI KITENDO CHA KADA WAO KUMWAGIWA TINDIKALI



Kijana Musa Tesha aliemwagiwa tindikali wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkaoni Tabora,akiwasimulia waheshimiwa,Katibu Mkuu wa UVCCM,Martin Shigela (kushoto) na Mbunge wa Viti maalum kupitia UVCCM mkoani Arusha,Catherine Magige (kulia) jinsi tukio halisi lilivyo mtokea.



Na Woinde Shizza,Moshi

BAADHI ya Vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa Mjini Igunga waliohusika na kitendo cha kumwagia tindikali kijana mmoja ambaye ni mfuasi wa chama cha mapinduzi wamelaaniwa vikali na katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM(UVCCM) Taifa Martine Shigela kwa kufanya kitendo hicho cha kinyama na chakiuuwaji na kusema kuwa kufanya hivyo sio siasa bali ni upuuzi .


Katibu Mkuu huyo alilaani kitendo hicho mara baada ya kumuona kijana huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu ya jeraha hilo ambalo analo katika paji lake la uso pamoja na mkono na kusema kuwa waliousika na tukio hilo wamelaaniwa hadi kwa mungu.

Katibu huyo aliyasema hayo jana mjini hapa wakati alipomtembelea Musa Tesha(24) mkazi wa Igunga ambaye alikuwa anapatiwa Matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kumwagiwa tindikali na wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),kwenye uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi huo.

“Kwakweli nimehuzunishwa sana na vijana hawa waliohusika na kitendo hiki kwani ni cha kinyama kabisa,kweli unamwagia binadamu mwenzako tindikali unamuaribu kisa chama jamani mbona waliohusika na kitendo hichi wamekosa ubinadamu sasa kama wameanza kufanya siasa za hivi mapema hii huko tunapoenda sindio balaa"alisema Shigela

Alibainisha kuwa ni jambo la kulaani kwa yeyote mpenda amani,inasikitisha pale ambapo vijana wanatumika na vyama vya siasa kuharibu maisha ya wenzao.

Shigela aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanashirikiana katika mambo ya msingi na kuwa na ushirikiano ili kuweza kujenga taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya ambaye alikuwa ameongozana na Katibu huyo akizungumzia tukio hilo akisema kuwa kitendo hicho ni cha unyama na sio kizuri kwani watu wanakosa ubinadamu kwa sababu ya chama alisema kuwa Tanzania nchi ambayo inaamani haitakiwi kuwa hivyo kwani hata katika historia yake uko nyuma haikua hivyo.

"huu ni unyama usiovumilika siasa zisitufikishe mahali ambapo mtu anaweza kutoa roho ya mwenzake kwa sababu ya siasa,wanasiasa tunatakiwa kushawishiana kwa hoja,hatuwezi tukagombania fito moja wakati sisi wote ni Watanzania na tunajenga nyumba moja”alisema Millya

Akizungumzia tukio hilo Musa ambaye ni Mkazi wa wilayani Igunga mkoani Tabora,alisema kuwa siku ya tukio akiwa anabandika mabango ya Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM,ghafla walitokea wafuasi wa Chadema na kumkamata wakidai kuwa wanampeleka polisi.

Alidai kuwa siku ya tukio Sepemba 6 mwaka huu,vijana hao ambao walikuwa ni wa Igunga Mjini,badala ya kumpeleka polisi kama walivyokuwa wamemweleza,walimpeleka katika kichaka kidogo ambapo walimvamia na kummwagia tindikali usoni na katika mkono wake wa kulia.

"walinipeleka porini kisha wakanimwagia tindikali na kunipiga sasa baada ya kufanya vile nilijitaidi kujisogeza hadi eneo la nyumba za watu na kwa bahati nzuri nikakuta nyumba moja karibu na pale nikagonga nao wakanisaidi wakatoa taarifa na nikasaidiwa kwakweli nawashukuru sana wale ambao wamenisaidia mpaka sasa na pia nashukuru sana chama kinavyonisaidia na pia nyie mliokuja kunitembelea nawashukuru kwani jinsi mnavyokuaja mnazidi kunitia moyo"alisema Musa

Aidha baada ya kijana huyo kumwagiwa tindikali alipatiwa msaada na wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo,ambapo aliletwa mjini hapa kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC,ambapo CCM inagharamia gharama za matibabu yake.

Kwa sasa hali ya kijana huyo inaendelea vizuri ambapo jana aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo huku akiendelea kupatiwa matibabu nyumbani kwa baba yake mdogo huku jicho la kulia likiwa halijafunguka huku lakushoto likiwa limefunguka na linaona kidogo japo kuwa bado linatiririsha machozi.

Naye Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Arusha kupitia umoja wa vijana (UVCCM) Catherini Magige alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio hilo la kijana huyo aliyemwagiwa tindikali.

"unajua sisi ni watu wa baba mmoja kama ni mafundi tunajenga nyumba moja sasa kama tunajenga nyumba moja yanini kugombania fito za kujengea wakati nyumba ni moja tunajenga eeh jamani vijana wa kitanzania hatutakiwi kugombana hatutakiwi kutoana roho kwa ajili ya chama kimoja au kingine tunachotakiwa kufanya ni kukaa na kujadiliana na kuelimishana jinsi ya kujenga nchi yetu na sio kuvurugana"alisema Magige.

Kufuatia tukio hilo Katibu wa UVCCM taifa aliahidi kiasi cha shilingi milioni 5 kutoka katika Jumuiya hiyo pamoja na kumpatia mtaji wa biashara kijana huyo pindi atakapo pona na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha kupitia(UVCCM) alimuahaidi kumpatia shilingi milioni moja za kumsogeza na kumsaidia pindi atakapo pona.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Nape Nnauye atinga Ukerewe


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Getrude Mongela mjini Nansio, Ukerewe mkoani Mwanza
Sehmu ya Umati Mkubwa wa Wanaccm Ukerewe Wakimsiliza Nape Nnauye
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Queen Mlozi (kulia) akimpa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape alipofika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, jana. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Queen Mlozi baada ya kuwasili jana kwenye Kivuko cha Nansio Ukwewe kwa ajili ya ziara ya siku moja wikayani humo.
Nape akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM baada ya msafara wake kuwasili Kivuko cha Nanisio, jana.
Nape akipinga ngoma kuunga mkono kikundi kilichokuwa kikitumbuiza kwenye mkutano huo.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»