Showing posts with label spika anna makinda. Show all posts
Showing posts with label spika anna makinda. Show all posts

WAKATI UMEFIKA WA KUWA NA CHUO KIKUU CHA WANAWAKE TANZANIA - SPIKA MAKINDA


Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Ludovick Mwananzila (wa pili kushoto) akimkaribisha Spika Bunge Mhe. Anne Makinda kusaini katika kitabu cha wageni mashuhuri aliposimama mkoani hapo wakati akielekea Masasi Mtwara  kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ndwika ambayo imetiza miaka mia moja tangu ianzishwe mwaka 1911.
Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyeibuka kidedea katika masomo yote,Mwajuma Issa, akipongezwa na Mhe. Spika huku Mwenyekiti wa Bodi ya Shule,Juma Satna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima na Mkuu wa wilaya za Nanyumbu na Masasi Mhe Fatma Ally wakishuhudia.
Spika Makinda akiweka jiwe la msingi katika jengo la teknolojia ya maarifa katika shule ya sekondari ya Ndwika ambako aliendesha harambee iliyokusanya shilingi 27,600,000/- ili kukamisha ujenzi wa shule hiyo.
Umaahiri wa ukandarasi wa awali umekwenda wapi?... haya ni majengo ya mabweni ya wanafunzi wa Ndwika yaliyojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Abdallah (kushoto) akimfahamisha jambo Mhe. Spika wakati wa ziara katika shule ya Ndwika. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima.
Spika Makinda (kushoto) akiwasili katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambapo amekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mia moja tangua kuanzishwa kwake na pia mahafali ya kidato cha nne akiongozwa na Mkuu wa Shule Mama Aluna Bakari kulia.
Spika Makinda akiwa na mwanafunzi, Asia Hassan, ambaye kwa sasa anatumia kitanda alichokuwa akitumia Mhe. Spika shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya wasichana ya Masasi,Mama Tesha (kulia) akimpokea Spika Makinda kwenye shule hiyo. Mhe Spika alisoma katika shule hii mwaka 1965-1968 ambapo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU Youth league.
Spika Makinda akiwa na “School mates” wake jana alipotembelea Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi ambapo amesema ni vema kuanza kufikiria kuanzishwa kwa Chuo kikuu cha wanawake Tanzania.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

TANZANIA YAPATA NAFASI NYINGINE IPU


Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 125 wa IPU chini ya uongozi wa Spika Makinda (katikati) ukijadili jambo kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais wa IPU. Kulia kwake ni Mhe. Angela Kairuki na Kushoto ni Mhe Suzan Lyimo. Mhe. Kairuki amechaguliwa kuziwakilisha nchi za Afrika katika Kamati ya Bunge la Dunia inayoshughulikia Haki za Binadamu na Wabunge. Mhe. Hamadi Rashid ni Makamu wa Rais wa Kamati ya Bunge la Dunia inayoshughulikia Maendeleo endelevu, Fedha na Biashara.
Mhe. David Kafulila akitimiza haki yake ya kidemokrasia kwa kupiga kura ya kumchagua Rais wa IPU.
Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebecca Kadaga (kushoto) akimpongeza Spika wa Morocco Bwa. Radi A. kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa IPU.Picha na Prosper Minja.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»