Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakijiuguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.
*****
Na mwandishi wetu
Watu 26 wamekamatwa kwa kuhusika na matukio ya upigaji Nondo mkoani Mbeya ambapo watuhumiwa wamegawanyika katika makundi matatu huku kila kundi likiwa na watu 4 hadi 15.
Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ameyataja makundi hayo kuwa kundi la kwanza linawahusisha watu wanne ambao ni Herodi Luka, Musa Idi, Fadhili Luvanda na David Jimy waliosababisha vifo vya watu wawili.
Kundi la pili linawatu saba ambao ni Edson Ulendo, Rashidi Mwakyungwe, Elasto Eliasi, Musa Isa, Amosi Mziho, Sifa Jolewa na Frenk Kitonga ambao walisababisha kifo cha Pc Meshaki
Kundi la mwisho linawahusisha watu 15 ambao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba kundi la kwanza na la pili yamekubali kuhusika na matukio ya upigaji nondo.
Wakati huohuo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametoa shukrani kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa matukio ya upigaji nondo na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo vya uhalifu.
[ Read More ]
Posted by newstz.blogspot.com
Majambazi wawili wakiwa na silaha wamemuua kwa risasi mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa amebebwa mgongoni na mama yake baada ya kuvamia gari la abiria lililokuwa likitoka Mbamba Bay kwenda Mbinga mkoani Ruvuma.
Majambazi hayo pia yaliwapora abiria fedha taslim Sh. 930,000.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 asubuhi katika Kijiji cha Ng’ombo Kata ya Kilosa Wilaya ya Nyasa.
Kamanda Kamuhanda alisema gari lililovamiwa na majambazi hayo ni lenye namba za usajili T 554 ASE aina ya Toyota Hilux lililokuwa likiendeshwa na Joseph Hamza (35).
Alisema baada ya gari hilo likiwa na abiria 14 likiwa katikati ya daraja, walitokea majambazi hao waliokuwa wamejifunga vitambaa usoni wakiwa na bunduki mbili moja aina ya Sub Machine Gun (SMG) na nyingine Semi Automatic Rifle (SAR) na kuanza kufyatua risasi hewani.
Kamanda Kamuhanda alisema risasi hizo ziliwajeruhi abiria wawili akiwemo mtoto Rehema Haule, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyejeruhiwa vibaya kwenye mguu wake wa kushoto akiwa amebebwa na mama yake na kukimbizwa hospitali ya Misheni ya Liuli kwa matibabu.
Hata hivyo, alisema mtoto huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.
Majeruhi mwingine katika tukio hilo ni Castory Kinunda (31), mkazi wa Mbamba Bay ambaye pia alijeruhiwa vibaya katika mkono wake wa kushoto ambapo wote anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Serikali ya Mbinga ambapo hali yake imeelezwa kuwa ni mbaya.
Kamanda Kamuhanda alisema baada ya majambazi hayo kufyatua risasi hewani, walianza kuwapekua abiria mmoja hadi mwingine na kufanikiwa kukusanya Sh. 930,000.
CHANZO: NIPASHE
[ Read More ]
Posted by newstz.blogspot.com