Showing posts with label igp. Show all posts
Showing posts with label igp. Show all posts

POLISI WAZUIA MAANDAMANO


*Wahofia uvunjifu amani, yalipangwa kufanyika J'mosi
*Wanaharakati kutafuta njia nyingine kufikisha ujumbe
*IGP Mwema asisitiza jeshi hilo halina nia mbaya

Na Benjamin Masese

SIKU moja baada ya wanaharakati kutoka asasi za kiraia zaidi ya 180, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Jukwaa la Katiba Tanzania kutangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima Novemba 26 mwaka huu, Jeshi la Polisi nchini limeyazuia kutokana na hofu ya kuvunjika kwa amani.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, kwa vyombo vya habari, ilisema kutokana na mchakato unaoendelea wa kupitishwa kwa Muswaada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya nchini, amekuwa akipokea maombi ya kufanya maandamano kutoka taasisi mbalimbali nchi nzima yakiwa na malengo tofauti.

Alisema malengo hayo ni pamoja na kupinga muswaada huo na mengine yakiunga mkono jambo linaloashiria kuleta migongano na hatimaye kusababisha uvunjifu wa amani.

Alizitaja taasisi zilizowasilisha maombi hayo kuwa ni pamoja na Jukwaa la Katiba Tanzania ambalo lilitaka kufanya mandamano ya amani nchi nzima kupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya 2011, ambao ulipitishwa na bunge hivi karibuni.

Taasisi zingine ni Asasi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao waliomba kufanya maandamano nchi nzima ili kuwaelimisha wananchi kuhusu upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya vyama vya siasa na washirika ili kuvunja amani ya nchi kupitia mwamvuli wa mchakato wa katiba mpya.

Alisema pamoja na maombi hayo, pia alipokea maombi ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM, ambao walitaka kufanya maandamano Novemba 26 mwaka huu, katika Wilaya na mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

“Lengo la mandamano ya Umoja wa Wanawake wa CCM ni kuipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni, maombi mengine yaliletwa na Taasisi ya Youth Camp, ambao wanapinga mwenendo wa mchakato wa kudai Muswaada wa Katiba na kudai kuwa, hauendani na utaratibu pamoja na utamaduni wa mtanzania,” alisema IGP Mwema.

Aliongeza kuwa kutokana na mwingiliano wa maombi hayo kila taasisi ikitaka kuwasilisha mawazo au hoja zao kwa njia ya maandamano, jeshi hilo limeona kuna kila dalili za kuwepo uvunjifu wa amani.

“Kutokana na hali halisi, tumeona ni vyema tusitishe maandamano yote na kutoa ushauri kwa wahusika watumie njia mbadala ya kufikisha mawazo yao kama walivyopanga jambo ambalo litasaidia kudumisha amani na utulivu wa nchi.

“Uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi umezungumza na taasisi zote zilizowasilisha maombi katika kikao cha pamoja tulichokifanya Makamo Makuu ya Polisi leo (jana0, ambapo taasisi zote zimekubali kuwa, hoja tulizotoa zilikuwa za msingi hivyo wameridhia kusitisha maandamano na kuahidi watamia njia nyingine kuwasilisha mawazo yao ambazo hazitakuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani,” alisema.

Alisema jeshi hilo halina nia mbaya ya kuzuia mikusanyiko au maandamano bali linatekeleza sheria na kanuni zilizopo.

Aliongeza kuwa jeshi hilo linapopata taarifa ya mikusanyiko au maandamano hulazimika kuzingatia mambo mengine muhimu kabla ya kuruhusu mkusanyiko au maandamano husika.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

IGP SAID MWEMA AONGELEA UGAIDI AFRIKA MASHARIKI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu matukio ya vikundi vya kigaidi yanayoendelea katika nchi za Afrika mashariki.Kulia ni Kamishna wa Polisi,Utawala na Usimamizi wa Rasilimali za Jeshi Clodwig Mtweve.Picha na Michael Jamson




Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo katika makaomakuu ya Jeshil hilo jijini Dar es salaam.

1. Awali ya yote napenda niwashukuru kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo na hasa suala la kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa nchini. 

2. Nimewaiteni leo kwa ajili ya kutaka kuwapa taarifa za mambo mbalimbali zikiwemo za matishio ya ugaidi yaliyoanza kujitokeza katika nchi ya jirani ya Kenya, Uharamia unaojitokeza katika ukanda wa Bahari ya Hindi na matukio mengine yanayojitokeza yakiwemo ya ajali za barabarani. 

3. Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa wasiwasi wananchi juu ya Ugaidi unaoendelea katika nchi ya jirani ya Kenya, kwamba, tayari tumejipanga vyema kwa kuimarisha ulinzi na hasa maeneo yote ya mipakani na kazi hii inafanyika kwa ushirikiano na vyombo vingine vyote vya ulinzi na usalama. 

4. Vile vile, kuna matukio ya uharamia na uhamiaji haramu ambayo yamekuwa yakijitokeza katika ukanda wa Bahari ya Hindi hususani katika mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi. Katika kipindi cha mwaka huu maharamia wapatao 13 wamekamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani.

 5. Tunatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhali ya watu ama makundi ya watu watakaowatilia mashaka kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa ili hatua za haraka za kiusalama ziweze kuchukuliwa. 
Watumie namba za simu zifuatazo 0787 668306, 0222138177, 111, 112 na namba za Makamanda wa mikoa, wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCDs) na RTOs zilizokwishasambazwa hadi ndani ya mabasi. 

6. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa taarifa ambazo zimefanikisha kukamatwa kwa baadhi ya wahalifu hao. Tunawaomba wananchi wote kuiga mfano huo wa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kufichua uhalifu wa aina yoyote ile na hasa matukio ya kikatili yanayofanyika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na madereva wazembe wanaosababisha ajali barabarani.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»