Showing posts with label mbarali. Show all posts
Showing posts with label mbarali. Show all posts

MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI MWALIMU KILUFI AACHIWA KWA DHAMANA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MFAWIDHI WA WILAYA YA MBEYA. JANA


Mbunge wa jimbo la Mbarali(kushoto) Mwalimu Dickson Kilufi akisikiliza jambo kutoka kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima, Bwana Gordon Kalulunga mara baada ya mbunge huyo kuachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.


Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi waliofika mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge huyo, ambaye ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.



Wananchi wakiwa nje ya mahakamani baada ya kumalizika kwa kesi ya Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi aliyeachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.


Baadhi ya Wananchi wakitoka nje ya mahakamani baada ya kumalizika kwa kesi ya Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi aliyeachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.


*****
Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi mwenye umri wa miaka 51 kupitia tiketi ya CCM aliyepandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hii katika Mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya na kunyimwa dhamana amechiwa huru kwa dhamana.

Kilufi aliachiwa kwa dhamana jana asubuhi na mahakama hiyo na kuamuliwa kufika Mahakamani hapo Octoba 24 mwaka huu kuendelea kusikiliza shitaka linalomkabili la kutishia kuua.

Zaidi ya wananchi 25 walijitokeza kwa ajili ya kumdhamini Mbunge huyo lakini mahakama ilihitaji wadhamini wawili tu ambapo baada ya kuachiliwa huru, nje ya mahakama kulitawala shangwe huku wakili wake Simon Mwakolo akikataa kuzungumza na waandishi wa habari na kumkataza mteja wake kuzungumza lolote.

Baada ya hapo Mbunge huyo aliwaeleza wananchi hao na familia yake kuwa alikuwa ameitwa na uongozi wa CCM kauli iliyopingwa vibaya huku baadhi wakisikika kuwa walikuwa wapi kumsaidia tangu awali na walikuwa wanamwitia nini! Hali iliyoonesha kumkatisha tamaa na baadaye alipanda gari yake na kuondoka na kwenda ofisi za chama hicho.

Awali Mbunge huyo alifikishwa mahakanani kwa kosa la kumtishia kumzuru Jordan Masweve March 16 mwaka huu wilayani Mbarali.

Kosa hilo lilielezwa kuwa ni kinyume na kifungu cha sheria 189 cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2002 kifungu kidogo cha 2(a) sura ya 16 ambapo mshitakiwa alikana shitaka.

Kesi hiyo yenye namba CC/158/2011 baada ya mshitakiwa kukana shitaka linalomkabili, ndipo wakili wa Mbunge huyo Simon Mwakolo aliiomba mahakama hiyo dhamana kwa mteja wake lakini Mahakama ilikataa kasha akapelekwa rumande ya gereza la Ruanda ambako amekaa mahabusu kwa muda wa siku tatu.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAlUMBANO YASABABISHA UKWASI WA MAENDELEO WILAYANI MBARALI.


Daraja la Kijiji cha Ijumbi, kata ya Ruiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya, ambalo hutumiwa na wananchi kuvuka kuelekea kijiji jirani, ambapo wananchi wengi wamekuwa wakifa kutokana na kuteleza. Mradi wa TASAF ulitoa msaada wa ujenzi wa daraja la uhakika lakini mpaka sasa kumekuwa na marumbano baina ya uongozi waHalmashauri ya mbarali, Kata husika na wananchi ya kwamba ni sehemu gani sahihi lapaswa kujengwa.
Serikali ngazi ya Mkoa ingilieni suala hili ili kunusuru madhara ya kifo kutokana na daraja hili marumbano mpaka lini.

Kwa tafti iliyofanywa na mtandao huu (mbeya yetu) umebaini kuwepo kwa marubano baina ya viongozi wa serikali ya kata, vijiji na wananchi, katika meneo ya kijiji cha Kanioga, Ijumbi, Nsonyanga, Mapogolo, Kapunga na Mawindi. Ambapo baadhi ya watendaji hutafuna fedha za miradi lakini hatua za kisheria hazichukuliwi dhidi yao
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU.


Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Dickson Kilufi atafikishwa mahakama ya mkoa wa Mbeya siku ya jumatatu tarehe Oktoaba 10, mwaka huu baada ya kudaiwa kutishia kuua kwa maneno Machi 15, mwaka huu katika Ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbarali.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mbunge huyo amedhaminiwa baada ya kukamatwa juzi na kushikiliwa na Jeshi la polisi ambapo Mwanasheria wa serikali alikubali dhamana iliyotolewa jumamosi ya Oktoba 8, mwaka huu.

Mbunge Kilufi anadaiwa kumtishia kumuua Afisa mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bwana Jordan Masweve mbele ya diwani wa kata hiyo Bwana Alex Mndamlage.

Kwa taarifa zinadai kuwa kumekuwa na mvutano wa muda mrefu wa kiutendaji baina ya Mbunge Kilufi na Afisa mtendaji huyo Bwna Masweve hali iliyopelekea kuamishwa kwa Afisa mtendaji huyo kutoka Kata ya Mawimbi na kupelekwa kituo cha sasa anachoendelea kufanya kazi cha Kata ya Ruiwa.

CHANZO: mbeya yetu blog
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»