Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akikabidhi pampas kwa ajili ya wodi hiyo maalum kwa watoto wnaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi mmoja,watoto hao ambao wamekuwa wakizaliwa hivyo kutokana na kukumbwa na matatizo mbalimbali.
Miss Tanzania 2011 Salha Esrael wakishirikiana na kipindi cha Njia Panda jioni ya leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye Wodi ya Watoto namba 36 (Neonatal Ward).Pichani Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akiwakabidhi baadhi ya vitu Manesi wa wodi hiyo maalum ya watoto kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili.

Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania 2011,Albert Makoye akiushukuru uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa kile ambacho wamedhamiria kukifanya kwa ajili ya kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi mmoja,kuhakikisha wanawaisaida kwa kila hali na pia kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na suala zima la watoto hao,ambao baadhi yao wazazi wao wamekuwa wakiwatelekeza,ama hata kuwatupa kwenye mapipa ya taka,vicha na vinginevyo,wakati watoto hao wana haki zote za kuishi kama watoto wengine .
Mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda ambao ndio waratibu wa zoezi zima la ushiriki wa Miss Tanzania kutoa msaada kwenye wodi hiyo maalum,Dr Isaac Maro akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo,pichani kati ni Miss Tanzania 2011,Salha Esrael pamoja na mdau Simalenga kutoka Clouds FM akirekodi taarifa muhimu za tukio hilo.
Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania 2011,Albert Makoye akiushukuru uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwapa sapoti ya kutosha kwa kile ambacho wamedhamiria kukifanya kwa ajili ya kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi mmoja,kuhakikisha wanawaisaida kwa kila hali na pia kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na suala zima la watoto hao,ambao baadhi yao wazazi wao wamekuwa wakiwatelekeza,ama hata kuwatupa kwenye mapipa ya taka,vicha na vinginevyo,wakati watoto hao wana haki zote za kuishi kama watoto wengine .
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akimtazama mtoto wake ambaye ameamua"kumuadapti" na kumpachika jina lake la Salha.
Salha akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima aliyezaliwa chini ya umri wa mwezi mmoja na Mama yake kufariki na kuhifadhiwa kwenye chumba maalum cha kuhifadhia watoto hao.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akifafanua jambo kuhusiana na misaada waliotoa leo jioni kwa wodi ya watoto wanaozaliwa chini ya umri wa mwezi mmoja wakishirikiana na kipindi cha Njia Panda.
Posted by newstz.blogspot.com
0
comments»