Showing posts with label shule ya msingi mpakani. Show all posts
Showing posts with label shule ya msingi mpakani. Show all posts

SHULE YAKOSA CHOO MAGONJWA YA MLIPUKO YATISHIA, NA WATOTO WAKETI SAKAFUNI WAKIHITAJI ELIMU BORA.


Hiki ndicho choo wanachotumia wanafunzi wa shule ya msingi Mpakani iliyopo mjini Tunduma majaaliwa yao yakoje? wanasoma wakiwa wameketi sakafuni, Tunduma ni moja ya miji maarufu nchini kwa biashara kati ya Tanzania na nchi zilizopo kusini mwa Afrika, ni mji wenye msongamano mkubwa wa biashara.


Jamani haiwezekani kwa hili pia magonjwa ya Mlipuko kutishia eneo hili, Wizara husika tazameni kwa macho ya huruma na kutekeleza pia ahadi Mashuleni.


Huenda watoto hawa ni wa wafanyabiashara wanasoma kwa kuketi chini,wanaweza kuwa wazazi wao ndio wamiliki wa maduka yanayozunguka katika mji maarufu wa Tunduma, wametelekezwa?serikali iko wapi mbona imewatelekeza watoto hawa?

Chanzo: Mbeya yetu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»