WAKATI UMEFIKA WA KUWA NA CHUO KIKUU CHA WANAWAKE TANZANIA - SPIKA MAKINDA


Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Ludovick Mwananzila (wa pili kushoto) akimkaribisha Spika Bunge Mhe. Anne Makinda kusaini katika kitabu cha wageni mashuhuri aliposimama mkoani hapo wakati akielekea Masasi Mtwara  kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ndwika ambayo imetiza miaka mia moja tangu ianzishwe mwaka 1911.
Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyeibuka kidedea katika masomo yote,Mwajuma Issa, akipongezwa na Mhe. Spika huku Mwenyekiti wa Bodi ya Shule,Juma Satna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima na Mkuu wa wilaya za Nanyumbu na Masasi Mhe Fatma Ally wakishuhudia.
Spika Makinda akiweka jiwe la msingi katika jengo la teknolojia ya maarifa katika shule ya sekondari ya Ndwika ambako aliendesha harambee iliyokusanya shilingi 27,600,000/- ili kukamisha ujenzi wa shule hiyo.
Umaahiri wa ukandarasi wa awali umekwenda wapi?... haya ni majengo ya mabweni ya wanafunzi wa Ndwika yaliyojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Abdallah (kushoto) akimfahamisha jambo Mhe. Spika wakati wa ziara katika shule ya Ndwika. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Husna Mwilima.
Spika Makinda (kushoto) akiwasili katika shule ya sekondari ya wasichana Ndwika ambapo amekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mia moja tangua kuanzishwa kwake na pia mahafali ya kidato cha nne akiongozwa na Mkuu wa Shule Mama Aluna Bakari kulia.
Spika Makinda akiwa na mwanafunzi, Asia Hassan, ambaye kwa sasa anatumia kitanda alichokuwa akitumia Mhe. Spika shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya wasichana ya Masasi,Mama Tesha (kulia) akimpokea Spika Makinda kwenye shule hiyo. Mhe Spika alisoma katika shule hii mwaka 1965-1968 ambapo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU Youth league.
Spika Makinda akiwa na “School mates” wake jana alipotembelea Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi ambapo amesema ni vema kuanza kufikiria kuanzishwa kwa Chuo kikuu cha wanawake Tanzania.

Categories: