Showing posts with label zanzibar. Show all posts
Showing posts with label zanzibar. Show all posts

ZANZIBAR YATIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YAKE NA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA NCHINI MAREKANI

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI NA RAIS WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA NCHINI MAREKANI DK.JAMES H. AMMONS WAKITIA SAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO KATI YA CHUO KIKUU CHA FLORIDA ( FAMU ) NA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR ( SUZA ).

MKUFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA ( FAMU ) DR. LEONARD PERRY AKIMUONYESHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI MOJA YA INJINI ILIYOBUNIWA NA WATAALAMU WA CHUO HICHO.


DR. SUBRAMANIAN RAMAKRISHNAN AKIMTEMBEZA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI KATIKA MOJA YA MAABARA KUU YA CHUO KIKUU CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA ( FAMU ).



Na Othman Khamis Ame - OMPRZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Mashirikiano kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini marekani.

Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.

Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hicho cha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha { FAMU } Dr. James ammons.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.

Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.

“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.

Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida

{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida { FAMU -FSU }.

Mkuu wa Kitengom hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.

Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.




[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WAGONJWA WA MOYO 611 KATI YA 1000 ZANZIBAR WANATARAJIWA KWENDA INDIA KWA MATIBABU



Mtoto Zahra Omar Awesu (Miezi 6) anayeugua Ugonjwa wa Moyo ambaye pia ni miongoni mwa watoto wanaotarajiwa kwenda Nchini India kwa matibabu (Picha na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar)


Na Fatma Mzee-Maelezo Zanzibar

Wagonjwa wa Moyo 611 kati ya 1000 wanatarajiwa kuondoka Zanzibar kwenda nchini India kufanyiwa matibabu ambapo kati ya wagonjwa hao wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka kumi na mbili.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Omar Abdalla Ali wakati alipokuwa akimkaribisha Hoyce Temu ambae aliwahi kuwa Mrembo wa Tanzani mwaka 1999 kwa lengo la kuwaona wagonjwa hao ili aweze kuwashawishi watu wenye uwezo kusaidia matibabu ya wagonjwa hao.

Katibu huyo alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanikiwa kuwapeleka wagonjwa 662 nchini Izraeli na wagonjwa 125 kupelekwa India kwa matibabu ya Ugonjwa wa Moyo katika miaka iliyopita.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wenye uwezo kuzidi kulitilia mkazo suala la kuchangi matibabu kwa watu wenye mahitaji ili kuisaidia Serikali katika kukabiliana na matatizo ya kiafya kwa wananchi wake.

Kwa upande wake Mrembo huyo wa Tanzania Hoyce Temu aliwaahidi wazazi wa watoto wenye matatizo ya moyo kuwa atatumia nguvu zake zote kwenda kuwashawishi watu wenye uwezo ili kuhakikisha wanachangia huduma za matibabu kwa wagonjwa hao.

Aidha Hoyce Temu alisema kuwa atarudi Zanzibar baada ya Wiki Moja ili kuleta mchango wowote atakaofanikiwa kuukusanya kutoka kwa wadau mbalimbali ili uweze kusaidia katika Safari ya hiyo ya India.

Amesema atakapo rudi Zanzibar ataanza na safari ya watoto sita ambao watakuwa na hali mbaya zaidi huku wengine wakisubiri kupatikana msaada ili nao wapelekwe huko India.

Aidha Mrembo huyo aliaahidi pia kushirikiana na Madaktari wa Mmanazi Mmoja na wazazi hao ili kuhakikisha tatizo hilo linaweza kupunguwa kwa kiasi kikubwa.
Amewataka Wazanzibari wenye uwezo kulichukulia umuhimu suala hilo ili kuweza kusaidia wanyonge na watu watu wasikuwa na uwezo wa kuwapeleka watoto wao matibabuni.

Nao baadhi ya wazazi wa watoto hao walimshukuru Hoyce Temu kwa ahadi zake na kuwaomba watu wenye uwezo hasa kwa kwa upande wa Zanzibar kusaidia watoto hao kwa hali na mali kwani fungu lao kubwa litabaki kuwa kwa Mungu.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»