Chalz Baba aunguliwa na nyumba





Na Shakoor Jongo

STAGE master wa Bendi ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Baba ‘Chalz Baba’ amepata kisanga kibaya baada kuunguliwa na nyumba anayoishi, maeneo ya Block 41 Kinondoni, Dar es Salaam.

Tukio la kuungua kwa nyumba hiyo lilijiri Jumamosi ya Oktoba 15, mwaka huu ambapo moto huo ulianzia kwenye feni lililofungwa juu ya dari.

“Dah! Tukio hili limeniathiri sana kwani naanza kujipanga tena upya wakati nilikuwa nimeshavuka katika kipengele cha samani za ndani,” alisema Chalz Baba bila kutaja thamani ya mali zilizoteketea.

Hata hivyo, mwanamuziki huyo alisema kuwa kwa msaada na majirani alifanikiwa kuzima moto huo, lakini vitu vyote sebuleni vilikuwa nyang’anyang’a.

PICHA ZOTE NA GLOBAL PUBLISHERS

Categories: ,