MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA NDULI ASUSIWA OFISI , WAJUMBE WAKE 16 WANG'ATUKA

Bw. Ayoub Mwenda


SAKATA la uongozi wa kibavu unaofanywa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nduli katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ayubu Mwenda limechukua sura mpya baada ya wajumbe 16 klati ya 25 wa serikali ya kijiji kujiuzulu nafasi zao.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwenyekiti huyo kudaiwa kushindwa kufanya mikutano ya hadhara ikiwemo ile ya kusoma mapato na matumizi ya kijiji hicho toka alipoingia madarakani toka mwaka 2009 ulipofanyika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulimweka madarakani.

Habari za ndani kutoka katika ofisi ya serikali ya kijiji hizo zilizoufikia mtandao huu na kuthibitishwa na afisa mtendaji wa kata ya Nduli Hamidy Mfalingundi zinasema kuwa wajumbea hao tayari wameandika barua za kujiuzulu nafasi zao hizo.

Kwa mujibu wa barua zao za kujiuzulu wajumbea hao wamedai kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kutofautiana na mwenyekiti huyo wa serikali ya kijiji.


Kwa upande wake Mfalingundi alisema kuwa barua za wajumbe hao alizopokea toka jumatatu ya wiki iliyopita na kuwa tayari wajumbe hao wamesimama kujishughulisha na shughuli zote za kijiji hicho.

Alisema kuwa barua ambazo amepokea kuhusu kujiuzulu kwa wajumbe 13 huku mjumbe 1 alifariki dunia na wajumbe wawili walijifuta katika nafasi zao kwa mujibu wa sheria baada ya kushindwa kuhudhuria jumla ya vikao vitatu mfululizo.

Hivyo alisema kuwa hadi sasa nafasi 16 ndizo zilizoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa wajumbe hao 13 kwa mpigo.

Kujiuzulu kwa wajumbe hao kumekuja baada ya wananchi wa kijiji hicho kufikisha malalamiko yao kwa uongozi wa CCM mkoa wa Iringa katika mkutano wao wa hadhara ulioongozwa na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha ambaye alifika miezi zaidi ya mitatu katika kijiji hicho kufanya tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na kupokelewa na malalamiko ya wananchi ya kumkataa mwenyekiti huyo.

Categories: ,