Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim akisisitiza jambo wakati akizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa kituo cha Clouds Media Group,waliofika ofisini kwake masaki jijini Dar es Salaam leo.katika mazungumzo hayo,Dkt. Salim amesema mahadhimisho haya ya miaka 50 ya uhuru ambayo kilele chake ni tarehe 9 Disemba ni sehemu ya tathmini ya kuoangalia ni wapi Serikali imefanikiwa na kwa kiwango gani na wapi bado haijafikia ili jitihada zaidi zifanyika na kuweza kufanikisha swala hilo.
Muandaaji wa vipindi wa Redio Clouds FM,Simalenga Simon akimuuliza swali Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) akiendelea kuongea na waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim (mwenye suti) akiwa na wanahabari waliomtembelea leo ofisini kwake Masaki,jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo yanayolenga maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.toka kulia ni Saleh Masoud (Clouds TV),Jerome Risasi (Clouds TV),Raymond Mshana (Clouds FM),Simalenga Simon (Clouds FM) pamoja na Othman Michuzi wa Globu ya Jamii.
Categories:
Dk salim ahmed salim,
mahojiano