Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkarisha Prince Alwaleed Bin Talal Bin Abdulaziz Alsaud, Mwenyekiti wa Kingdom Holding Company (KHC), Ikulu Jijini Dar es salaam leo. Prince Alwaleed alikuwa Dar katika ziara ya siku moja na alikutana na Rais pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kuzungumzia mambo kadhaa yakiwemo Shule ya Nakayama Girls High School iliyoko Rufiji katika Mkoa wa Pwani, shule hiyo inaendeshwa na WAMA ambayo iko chini ya Mwenyekiti Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika maongezi na Prince Alwaleed Bin Talal Bin Abdulaazi Alsaud, Mwenyekiti wa Kingdom Holding Company (KHC),ambaye alisindikizwa na mke wake, (kushoto) Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya kikwete akimwonyesha kitu Prince Alwaleed Bin Talal Bin Abdulaziz Alsaud, Mwenyekiti wa Kingdom Holding Company (KHC) na Mke wake wakati akiwaonyesha Mandhari ya Ikulu.