AJALI MBAYA YA BASI MKOANI IRINGA YASABABISHA VIFO VYA WATU WANNE


Maiti ikiwa imenasa katika basi


Msamaria mwema mkazi wa Nyololo Mufindi akiivuta mmoja kati ya majeruhi aliyenasa katika basi


Wananchi wa Nyololo Mufindi mkoani Iringa wakitazama ajali ya basi ya New Force lililopinduka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa vibaya


Trekta likijaribu kulivuta basi hilo ili kuwavuta majeruhi waliokuwa wamenasa katika basi na maiti


Dereva wa Halmashauri ya Mbozi Mbeya akitazama gari lake lililoharibika vibaya mbele


Gari la Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambalo lilikuwa na wakuu wa Idara akiwemo mwanasheria likiwa limejiingiza nyuma na lori kukwepa kugongwa na basi hilo. Picha na Habari na mdau Francis Godwin









---
IKIWA ni siku Mbili toka msafara wa makamu wa Rais upate ajali mbaya mkoani Tanga na kusababisha kifo cha askari na kujeruhi wengine ,ajali mbaya imetokea wilayani Mufindi mkoani Iringa na kusababisha Vifo vya abiria zaidi ya watatu wa basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T666 BCR lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam Kwenda Mkoani Mbeya.

katika ajali hiyo abiria wengine zaidi ya watano wamevunjika vibaya viungo vyao huku abiria zaidi ya 30 wakinusurika kufa katika ajali hiyo.

Mashuhuda wa ajali hiyo walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 alasiri Leo wakati basi hilo likielekea mkoani Mbeya na kuwa chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.

Akizungumza na mtandao huu mmoja Kati ya walionusurika katika ajali hiyo John Sanga alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha basi kwa mwendo kasi na hata abiria walipojaribu kumkanya alishindwa kusikiliza.

Alisema eneo hilo ambalo ajali imetokea ni eneo ambalo linamteremko na kuwa mbali ya basi hilo kupinduka pia magari mengine Mawili likiwemo gari la serikali lenye namba za usajili STK 2340 na IT yamegongana na Lori katika eneo hilo.

Maiti zilizotolewa katika ajali hiyo hadi saa 2.usiku zilikuwa ni mbili Hadi mwandishi wa habari hii iweka habari hii katika mtandao jitihada za kuzivuta maiti nyingine katika basi zilikuwa zikiendelea huku askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kedmundi Mnubi walikuwa wakiendelea kuvuta maiti zilizonasa katika basi Hilo.

Categories: