Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro jana. Kushoto kwake ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Bw. Ludovick Utouh na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh Joel Bendera.
Rais Jakaya Kikwete akielekea kupanda mti baada ya kuzindua jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro jana. Pamoja naye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Bw Ludovick Utouh.
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi toka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Bw Ludovick Utouh katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro jana. Wengine ni Waziri wa Katiba, Mh Celina Kombani (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh Joel Bendera na mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
PICHA NA IKULU
Categories: