Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar leo
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakati wa sherehe za Mapinduzi leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi leo.
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri Kiongozi Mstaafu, Mh. Ramadhani Haji Fakhi wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo
Msafara wa Rais Kikwete ukiwasili katika Uwanja wa Amaan kwa maadhimisho hayo
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Categories: