SERIKALI KUTANGAZA KURUDIA MTIHANI WA DARASA LA SABA

Habari Na Flora Amon

Wanafunzi waliofutiwa matokeo 2011 na wadau wa elimu wamepinga vikali kufutwa mitihani hiyo kwa madai kuwa kwa kufunya hivyo ni kuwaathiri kisailojia wanafunzi hao.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mgulani,Bw Kadawi Limbu alisema kuwa Serikali bado inafanya mambo kwa kukurupuka.

Alisema kuwa ni bora Serikali ikasema wamekosa nafasi ya kuwapeleka watoto hao kwa kuwa wamefaulu kwa wingi mwaka huu.

"Hii ni mbinu ya kuwachelewesha ili watoto wengine waolewe na wengine waende mtaani kuwa majambazi"Alisema Bw.Kadawi.

Alisema kuwa kama Serikali imewabaini kuwa wanafunzi waliofanya udanganyifu ni 107 kuliwa na haja gani ya wengine kuwaambia wafanye mtihani tena na kwakukaa darasani mpaka mwezi Septemba.

"Mimi nahisi hii itakuwa njama kati ya Serikali na shule za binafsi ili wanafunzi watakaokuwa na uwezo waende kusoma shule za watu binafsi"Alisema.

Aliongeza kuwa yeye haoni sababu ya wanafunzi hao kufanya mtihani mwezi huo badala yake wapewe mtihani hata mwezi huu hata kwakuchangi gharama na wazazi ili waanza kitadato cha kwanza mwaka huu kama wenzao.

Alibainisha kuwa endapo wanafunzi hao watatakiwa kufundishwa walimu watapatika kutoka wapi wakati hata waliopo awatoshelezi kwa mahitaji.

"Baraza la Mtihani limejichanganya na hawana nia njema ,kama kweli wana nia njema wawape wanafunzi hao mtihani mwezi huu na waliopewa majibu wa wataonekana .

Alisema kuwa mwanafunzi anafundishwa na mwalimu darasa na kuolewa na siku ya mtihani anajibu alichofundishwa,sasa kama mtihani ulikuwa na majibu ya kuchagua mpaka hisabati watasemaje wafanya udanganyifu.

"Hawa wanafunzi waliomaliza washapewa vyeti kwa hiyo wakimaliza tena wapewa vyeti au watakuwa wahitimu wa darasa la saba mara mbili"alihoji.

Kwa upande wa Rais wa Chama Walimu Tanzania (CWT),Bw.Gratia Mukoba Alisema kuwa,si sahihi wanafunzi hao kufanya mtihani mwezi Septemba badala yake wapewe hata mwezi huu warudie.

"Kama hakuna aliyetiwa hatiani ni vema wakatungiwa mtihani upya wakapewa mana wasimamizi wapo na wahihishaji wapo watasahihisha na watoto wakaendelea na kitado cha kwanza"alisema Bw.Mukoba.

Alisema ili kuthibitisha kama kuna udanganyifu uluofanyika wapewe mtihani na waliofanya udanganyifu watapatikana tuu.

Naye Mbunge wa Musoma Mjini Bw.Vincent Nyerere akiongea na Majiora kwa njia ya simu alisema kuwa,mwanafunzi anaingia kidato cha kwanza siyo kwa ukubwa bali kufanya vizuri katika mitihani yake lakini siyo sahihi wanafunzi hao kukaa muda mrefu wakiwa wanasuburi kufanya mtihani badala yake wangepewa mtihani wakafanya upya.

"Unajuwa wakisema warudie mtihani watawanyima wenzao fursa ya ufaulu na ushindani hautakuwa sawa kwani watakuwa wanafunzi wengi"alisema.

Alisema kuwa ni kweli vizuri kurudia mtihani lakini si kwa mwezi Septemba kama Serikali ilivyosema kwani wanafunzi hao watakuwa wanasoma darasa moja mara mbili na sijuwi kama watakuwa makini katika kufatilia masomo pindi wanapofundishwa tena.

Mmoja wa wazazi wanafunzi hao Bi.Asia Sizya alisema kuwa yeye binafsi halifiki swala hilo sababu watoto hao wahasirika kisaikolojia kwakuwaona wenzao waliza nao wapo sekondari na hao wapo shule ya msingi wanasubiri kufanya mtihani.

"Unajuwa Serikali inatoa adhabu kubwa kwa watoto wadogo ambao wengine bado huelewa wao ni mdogo ni vema wawape mtihani hata mwezi huu wafanye ili linapokuja chaguo la pili nao waenda madarasani."alise,a Bi. Sinzya .

"Unajuwa siyo wanafunzi wote watakao weza kusubiria mwezi Septemba wengine wataka tamaa matokeo yake kuingia katika wimbi la ujambazi na wengine kupata mimba za utotoni"aliongeza.

Aidha ameita Serikali kufanya kazi katika utaratibu unaoeleweka na siyo kukurupuka katika maamuzi.

Kwa upande wa mdau mwingine kutoka mkoani Mbeya Bw. Agustino Nchimbi alisema Serikali ingewaruhusu wanafunzi hao kufanya mtihani ili iwe fundisho kwa wazazi na walimu wenye tabia kama hizo.

"Serikali ingewaruhusu wanafunzi hao kurudi mtihani kwani itakuwa kawaida kwamba watu wanafanya udanganyifu ili walalamike na kuruhusiwa kufanya mtihani upya.

Categories: