VIONGOZI WA DINI YAPEWA SEMINA KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012

 Mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa akisisitiza jambo kuhusu sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu wakati wa semina ya viongozi wa dini jijini Dar es salaam.

 Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhani Khijjah alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi  2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.


Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi  vyenye jumbe mbalimbali  kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchi nzima mwezi  Agosti mwaka huu  baada ya wataalam kutoka  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo .

Categories: