Showing posts with label NHC. Show all posts
Showing posts with label NHC. Show all posts

TAARIFA: MKURUGENZI MKUU KUONGELEA MIKOPO YA BENKI NA NYUMBA ZA NHC


MIKOPO YA NYUMBA KUPITIA MABENKI
Siku ya ijumaa ya tarehe 11/11/2011 Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Kyando Mchechu akishirikiana na wataalam wa masuala ya mikopo ya nyumba watashiriki katika kipindi cha KIPIMA JOTOsaa 3.00 usiku mpaka 4.00 usiku kinachorushwa na kituo cha ITV.

Kipindi kama hicho pia kitarushwa na TBC1 kwa lugha ya kiingereza kupitia kipindi cha “THIS WEEK IN PERSPECTIVE” siku hiyo hiyi ya Ijuma kuanzia saa 3.00 usiku mpaka 4.00 usiku. Ni matarajio yetu kuwa vipindi hivyo vitatoa elimu ya kutosha kuhusu mikopo ya nyumba ambayo inatolewa na mabenki hapa nchini.

Wote mnakaribishwa kuangalia vipindi hivyo.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

NHC yauza nyumba

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limeanza kuuza nyumba zake likianzia na zilizopo katikati ya Jiji la Arusha. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe alisema nyumba hizo zitauzwa kwa Watanzania wa ndani na nje ya nchi, wenye mahitaji ya nyumba za makazi.

Bei ya chini kabisa ya kila nyumba ni Sh 175,314,366.48 bila kujumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Ukiongeza asilimia 18 ya VAT bei ya chini kwa nyumba yenye vyumba vitatu ni Sh milioni 200. Aidha, baada ya mauzo hayo, kwa mujibu wa Shambwe, mnunuzi atakayekabidhiwa nyumba anaruhusiwa kumpangisha mtu mwingine kwa bei watakayokubaliana, ilimradi tu mpangaji aitumie kwa makazi na sio biashara. Hata hivyo, bei inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo kwa kuwa kwa mujibu wa maelezo ya Shambwe, nyumba hizo zitauzwa kwa wateja 30 tu, watakaotangaza dau kubwa katika maombi yao.

Nyumba hizo zenye ukubwa wa meta za mraba 169.45 ziko katika majengo mawili ya ghorofa tatu kila moja yaliyojengwa katika kiwanja namba 565/1 na kwa pamoja yatakuwa na eneo la kuegesha magari 24. Shambwe alisema kila nyumba ina baraza tatu, tangi la maji la ujazo wa lita 1,000 na kati ya vyumba vitatu vya kulala, chumba kimoja kina choo na bafu ndani.

Sifa nyingine ya nyumba hizo ni kuwa na sebule kubwa, chumba cha kulia, jiko, stoo, bafu na vyoo vya jumuiya. Alisema nyumba hizo zinazotambulika kwa jina la Meru kutokana na uamuzi wa NHC kuuenzi Mlima Meru na zitaanza kutumika ndani ya siku 90 kuanzia Oktoba mosi, mwaka huu.

Mkurugenzi huyo aliwataka Watanzania kuanza kutuma maombi yao leo, ili wanunuzi 30 wapatikane na kukabidhiwa. “Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 31, mwaka huu, saa 04:00 asubuhi. Nyumba zipo 48 katika maghorofa yetu mawili na ni 30 tu zitakazouzwa kwa sababu 18 zitatumika kwa biashara ya kupangisha. “Wanaopenda kuzinunua wachukue fomu za maombi katika ofisi zetu za Arusha na kwingineko
au katika tovuti yetu www.nhctz.com,” Shambwe alisema.

Aliongeza kuwa, fomu ya maombi itakayojazwa na kuwekwa sahihi na mteja mwenye dhamira ya kununua nyumba hizo inatakiwa iambatanishwe na barua inayoonesha kiasi ambacho mhusika anaweza kulipa, pamoja na ushahidi wa malipo yasiyorejeshwa ya Sh 10,000, kama ada ya maombi.

“Pamoja na viambatanisho hivyo, mteja anapaswa pia kuambatanisha ushahidi wa malipo ya awali ya asilimia 10, aliyoyafanya kupitia benki, kulingana na thamani ya nyumba aliyochagua,” alisema. Baada ya malipo hayo ya awali ya asilimia 10, Shambwe alisema mteja atapewa siku 90 kuanzia tarehe ya barua yake ili akamilishe asilimia 90 ya malipo yaliyobaki, vinginevyo, nafasi ya ununuzi atapewa mtu mwingine.

Hata hivyo, alisema wateja watakaoshindwa kukamilisha malipo hayo katika muda uliopangwa, watarudishiwa asilimia nane tu ya malipo walioyafanya awali ya asilimia 10 na asilimia mbili itakayokatwa itatumika kama gharama ya kumhudumia. “Endapo mteja hatahitaji kurejeshewa fedha hizo, anaweza kuomba asilimia 10 yake itumike katika ununuzi wa nyumba katika miradi mingine ya shirika hili ambayo hata hivyo, itakamilika ndani ya miezi mitatu au minne ijayo.

“Tukianzia na ule wa nyumba za makazi kwa watu wa vipato vya kawaida wa Ubungo na Chang’ombe Dar es Salaam, na mwingine wa Arusha, utakaokamilika miezi kadhaa ijayo,” alieleza.

Alisema mradi huo ambao ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa nyumba 1,500 za NHC, uliogharimu Sh bilioni tano na unategemewa kuliingizia shirika hilo Sh bilioni saba au nane. “Faida yoyote itakayopatikana itatumika kujenga nyumba nyingine kwa ajili ya makazi bora ya Watanzania wa kipato cha chini,” alisema Mkurugenzi huyo.

chanzo:habari leo
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rungu la NHC latua Wizara ya Habari


Zaina Malongo
OPERESHENI ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), ya kuwafukuza katika nyumba zake wapangaji sugu jana ilibisha hodi katika Wizara ya Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo baada ya Idara zake za Habari (Maelezo) na Utamaduni kutupiwa nje virago zikidaiwa jumla ya Sh391 milioni. Deni hilo linaelezwa kuwa ni malimbikizo ya kodi ya pango kwa muda wa miaka mitatu mfulululizo.

Mchakato wa idara hizo kufukuzwa katika majengo ya NHC ulianza saa 3.00 asubuhi ukiongozwa na kampuni za udalali ya Mzizima Action Mart and Bedt Collect Ltd. Baada ya kufika katika ofisi hizo walikwenda moja kwa moja katika ofisi za uongozi na kueleza kusudio lao.
Bila kuchelewa wafanyakazi hao ambao walionekana dhahiri kujua walichokifuata, walianza kutoa kifaa kimoja baada ya kingine nje zikiwamo meza, viti, kompyuta, seti za televisheni na makabrasha mengine.

Kwa Maelezo, tukio hilo lilifanyika mbele ya macho ya waandishi wa habari ambao walikuwa katika ofisi hizo wakisubiri kuingia katika mikutano iliyokuwa imepangwa kufanyika. Kutokana na hali hiyo mikutano hiyo ilikwama.
Idara ya Maelezo ina ukumbi ambao hutumika kuendeshea mikutano ya habari ambayo wahusika hulipa kiasi kidogo cha fedha na kupata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati operesheni hiyo ikiendelea katika idara hizo, Meneja wa Kitengo cha Kukusanya Madeni NHC,  Japhet Mwanasenga alisema Idara ya Utamaduni inadaiwa Sh87milioni, Maelezo inadaiwa Sh47 milioni ikiwa ni kodi ya miezi saba na Idara ya Filamu inadaiwa Sh30 milioni ikiwa ni kodi ya miezi minane.

Alisema shirika lake limefikia uamuzi huo baada ya kutenda haki kwa kila mdaiwa. Alisema kwanza lilitoa notisi ya siku 14 ya kumtaka kila mdeni awe ameshalipa deni lake.

Alisema licha ya wizara hiyo kupelekewa notisi hiyo ilishindwa kulipa deni hilo kitendo kilichosababisha wachukue hatua zaidi. “Baada ya kuona wizara inadaiwa, NHC kupitia kitengo chake cha kukusanya madeni ilitoa taarifa katika kuhusiana na deni hilo lakini walijibu kuwa watalipa baada ya Serikali kupitisha Bajeti ya wizara,” alisema Mwanasenga.

Mwanasenga alisema hata hivyo, baada ya Bunge la Bajeti kumalizika, wizara hiyo ilipitishiwa bajeti yake lakini deni hilo halikulipwa ndipo NHC ilipoamua kuwasilisha nakala ya kukumbushia deni hilo.

Huu ni mwendelezo wa shirika hilo kuwatolea vifaa nje wadaiwa wake sugu. Juzi tukio kama hilo lilifanyika katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikidaiwa Sh30 milioni.

 Akizungumzia kuhusu wizara hiyo, Mwanasenga alisema hadi jana wizara hiyo ilikuwa imeshalipa kiasi cha Sh25 milioni hivyo NHC kurudisha vifaa vyake kwa kuwa imeahidi kumalizia deni lililobaki baada  ya wiki moja.

Chanzo: MWANANCHI

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»