Showing posts with label jakaya kikwete. Show all posts
Showing posts with label jakaya kikwete. Show all posts

JK aonja shubiri ya umeme


Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB Tully Mwambapa picha ya Mwalimu Julius Nyerere iliyonunuliwa na Benki hiyo kwa kiasi cha Sh.milioni 35,wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais kwa ajili ya kukusanya pesa za upanuzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam juzi na kupatikana Sh.722 milion.Fidelis Felix







Na Aziza Masoud

RAIS Jakaya Kikwete juzi usiku alionja adha ya kukatika kwa umeme alipokuwa akiendesha hafla ya kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.  Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5:43 usiku takriban saa nne tangu hafla hiyo ianze.
Rais Kikwete alifika ukumbini hapo saa 2:33 muda mfupi akitanguliwa na viongozi wengine wa Serikali.  Baadhi ya viongozi hao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki.  Kukatika huko kwa umeme, kuliwafanya wageni waliokuwapo ukumbini kuanza kupiga kelele za: “Ngeleja... Dowans... Ngeleja... Dowans... Ngeleja... Dowans.”

Tukio hilo lilidumu kwa dakika mbili kabla uongozi wa Mlimani City kuwasha genereta. Katika hafla hiyo, Rais Kikwete alichangisha Sh720 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho kinachotarajiwa kujengwa katika Kampasi ya Mlimani katika kumbukizi ya Miaka 50 ya Uhuru.  Kituo hicho kitakuwa na maeneo ya kupumzika wanafunzi, hosteli, sehemu za michezo, maktaba, huduma za vyakula, benki, ofisi za serikali ya wanafunzi na kituo cha intaneti.

Akizungumza kabla ya uchangishaji huo, Rais  Kikwete alisema lengo la kuchangisha fedha hizo za kujenga kituo cha wanafunzi ni kuboresha mahitaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambayo kwa sasa  yamekuwa changamoto kubwa inayosababisha wanafunzi kupata elimu katika mazingira magumu.

 “Mara  nyingi ukipita katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unakuta wanafunzi wamezagaa katika maeneo mbalimbali na wengine chini ya miti. Hii yote inatokana na kukosa eneo maalumu la kujisomea na kupumzika mara wanapomaliza au kusubiri kuingia katika vipindi,” alisema Kikwete.

  Alisema kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kimaendeleo, chuo hicho kwa sasa kinakadiriwa kuchukua wanafunzi 20,000 kwa mwaka, tofauti na miaka ya nyuma   kilipokuwa kinachukua wanafunzi 14,000.  Alisema kutokana na hali hiyo, wahitimu wanapaswa kuchangia maendeleo ya chuo hicho kwa kuwapatia wanafunzi nafasi za malazi ambazo kwa sasa hazitoshi na kuwalazimu wengine kulala nje ya eneo la chuo.

Awali, Dk Kawambwa alisema kukutana kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo hicho ni kuendeleza utamaduni unaotumika duniani kote wa kuchangia maendeleo ya shule au vyuo wanavyotoka.  “Jambo tunalolifanya jioni hii lina maana kubwa, tunajenga utamaduni wenye manufaa katika nchi yetu kuendeleza elimu nchini kwa kuchangia maendeleo ya shule au chuo,” alisema.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema kituo hicho kitagharamu Sh17bilioni na hatua ya kwanza ya kupata fedha za ujenzi huo ni kuandaa kampeni hizo za uhamasishaji na uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali.  “Hafla ya uzinduzi wa michango hiyo ilifanyika Januari 27 mwaka jana.

Iliwahusisha wanajumuiya ya chuo na wajumbe wa baraza la chuo na tulibahatika kupata Sh1.2bilioni, nyingi zikiwa ni ahadi za wafanyakazi,” alisema Profesa Mukandala.  Alisema baada ya hafla hiyo, kulifanyika hafla nyingine Ikulu mwezi huohuo iliyokuwa ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete. Katika hafla hiyo jumla ya Sh1.5bilioni zilikusanywa.

Alisema hafla ya tatu ilikusanya Sh658 milioni za ambazo zilitolewa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye naye ni muhitimu wa chuo hicho. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba aliwataka wahitimu waliosoma chuoni hapo kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo yake.

Katika hafla hiyo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) iliahidi kutoa Sh150 milioni, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Sh130 milioni, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sh100 milioni, Mikumi Interprises Sh20 milioni, Benki ya NMB Sh20 milioni.  Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) ilitoa Sh30 milioni, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Sh30 milioni, Mfuko wa Pensheni wa PSPF Sh20 milioni na Mnyika alitoa Sh2milioni na kuahidi kutoa Sh milioni moja kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano.

Benki ya CRDB ilinunua katika mnada wa kuchangisha fedha za ujenzi huo, picha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa Sh35milioni. Rais ndiye aliyeendesha mnada wa picha hiyo.


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rais Jakaya Kikwete Amaliza Ziara Yake Mpanda na Kurejea Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akiwatazama wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mtapenda cha Majimoto wilayani Mpanda(hawapo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam October 18, 2011. Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rais Kikwete afungua Kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika Mpanda


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawekezaji na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi hapa nchini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufungua kongamano la uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika huko Mpanda mkoani Rukwa lao mchana.
(picha na Freddy Maro).
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWASILI MPANDA NA KUZINDUA MKUTANO WA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA


Rais Dk. Jakaya Kikwete akisaliaiana na Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda, mara baada ya kuwasilia katika uwanja wa ndege wa Mpanda leo asubuhi, tayari kwa kufungua mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanzaganyika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma unaohudhuriwa na Mabalozi, maofisa wa serikali na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi, mkutano huo hivi sasa unaendelea kwenye ukumbi wa idara ya maji mjini Mpanda. Mpaka sasa Rais tayari ameshaingia ukumbini na anaendelea na hotuba yake ya ufunguzi matukio zaidi ya ufunguzi wa mkutano huo yatawajia baada ya muda, katika picha kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi pamoja na wawekezaji wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutengwe katikati akiwaelekeza wageni mbalimbali wakati waliposili kwenye uwanja wa ndege mjini mpanda leo asubuhi kwa ajili ya mkutano huo.
Picha na habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

JAJI MKUU AMPONGEZA RAIS KIKWETE




Mhe. Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande akisisitiza jambo wakati alipokuwa akibadilishana mawazo mwishoni mwa wiki na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ubalozi huo upo jijini New York, Marekani. katika mazungumzo yake na maafisa hao, mazungumzo ambayo pia yaliwahusisha maafisa kutoka wizara mbalimbali wanaohudhuria mikutano ya Kamati za Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, pamoja na mambo mengi Mhe. Jaji Mkuu alizungumzia namna ambavyo Muhimili huo wa usimamizi na utoaji wa sheria umejipanga katika kuboresha utendaji kazi. akitumia fursa hiyo kumpongezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba chombo hicho muhimu kinasaidiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

*****


Na Mwandishi Maalum,New York

Jaji Mkuu, Mhe. Mohamed Chande Othman amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutoa kipaumbele uboreshaji na utendaji kazi wa Mahakama nchini Tanzania

Jaji Mkuu ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki, wakati alipoutembelea Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na maafisa wa Ubalozi huo.

Jaji Mkuu Mhe. Chande amesema, uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kuteua majaji wengi katika Mahakama Kuu ni kielelezo cha namna gani anavyojali utawala wa sheria na anastahili kushukuriwa.

Aidha Jaji Mkuu, amesema uamuzi wa serikali wa kuanzisha Mfuko wa Mahakama kama ilivyo kwa muhimili mwingine wa dola yaani Bunge, ni jambo jema kwa kuwa mfuko huo utasaidia sana katika si, tu uboreshaji wa kazi za mahakama lakini pia katika suala zima la kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kupungunza mrundikano wa kesi.

"Mhe. Rais ametusaidia sana, ameteua majaji wengi katika Mahakama Kuu tena wengi wao wakiwa vijana, hawa watadumu kwa muda mrefu. Tunamshukuru sana kwa hili na ni matumaini yangu kuwa ataendelea na hatua hii ya kutuongeza majaji wengi zaidi" amesema.

Katika mazungumzo yake na maafisa hao, mazungumzo ambayo pia yaliwahusisha maafisa kutoka wizara mbalimbali ambao wapo hapa New York kuhudhuria mikutano ya Kamati za Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Jaji Mkuu amebainisha kuwa mahakama nchini bado zinakabiliwa na changamoto nyingi.

Amezitaja baadhi ya changamoto hizo ambazo pia zina kwamisha ufanisi na ambazo baadhi zimeanza kufanyiwa kazi, ni pamoja na ile ya kujaribu kutenganisha kazi za kisheria na kazi za kiutawala.

"Kama nilivyosema, tunakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwamo hizo za upungufu wa majaji na mlundikano wa kesi,lakini kuna hili la mahakimu kufanya kazi za utawala hasa huko mikoani, hili pia ni tatizo kubwa tumeanza kulifanyia kazi"

Amefafanua kwa kusema , mahakimu wengi wamekuwa wakifanya kazi za utawala kwa mazoea tu, na kwamba hiyo si sahihi na inawapunguzia muda wa kushughulikia kesi.

Akasisitiza kwamba kazi za utawala, za mipango, uhasibu, au uratibu wa raslimali watu ni kazi ambazo zina mafunzo yake, ni kazi za kitaalam.

" Katika hili mahakimu wetu wanafanya kazi kwa mazoea tu ni mfumo ambao tumeurithi. Tumejipanga kuubadili utaratibu huu, ili mahakimu wafanye kazi za kisheria na watawala wafanye kazi za utawala na mengineyo.

Aidha ameongeza kuwa uongozi wake wake umejipanga pia katika kuboresha utendaji kazi katika mahakama za mwanzo ambako amesema asilimia zaidi ya 75 ya kesi ndiko ziliko

Akizungumzia kuhusu mlundikano wa kesi, Mhe. Jaji Mkuu amesema ingawa kumekuwapo na uboreshaji katika usikilizaji wa kesi na utoaji wa hukumu. Lakini bado kuna mlundikano mkubwa wa kesi ambazo hazijapata hata nafasi ya kusikilizwa .

Akatoa mfano wa Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi ambako amesema kuna kesi nyingi sana ikilinganishwa na majaji waliopo ambao ni wanne tu.

" Matatizo ya ardhi ni moja ya tatizo kubwa na lenye mlundikano mkubwa wa kesi. Ni kweli kwamba Wizara husika imejitahidi sana katika kupunguza baadhi ya matatizo yakiwamo ugawaji wa viwanja kwa mtu zaidi ya mmoja . Lakini bado mfumo wa wizara hiyo kushughulikia matatizo ya ardhi si mzuri sana. "

Akasema mfumo wa kushughulikia matatizo ya ardhi unatatiza kwa kuwa matatizo hayo yanaanzia katika ngazi za chini kama vile ngazi za vijiji na kuendelea hadi wizarani. Lakini utatuzi wake wa kisheria unaishia mahakamani.



"Tumejipanga kulitatua tatizo hilo, jambo moja tunalotaka kufanya ni kuifanya Mahakama Kuu kitendo cha Ardhi, mfumo wake uwe kama Mahakama ya Biashara. Kwa kutumia mfumo wa Makahama ya Biashara tunaamini kwamba kasi ya kushughulia kesi za ardhi utaboreka na ufanisi utaongezeka". Amesisitiza.

Akijibu swali kuhusu mchakato wa maandalizi ya Katiba mpya pamoja na hukumu ya kuyonga.

Jaji Mkuu alikuwa na haya ya kusema. Kuhusu Katiba, kazi ya maandalizi ikiwamo ya kuratibu ukusanyaji wa maoni, pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi inaendelea vizuri na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia imeshirikishwa kwa asilimia 100.

Akasisitiza kwamba licha ya mkanganyiko uliojitokeza mwanzoni mwa zoezi hilo, ana imani kubwa na serikali kwa kile alichosema imejipanga vizuri.

Kuhusu hukumu ya kunyonga, Jaji Mkuu amesema kwa Tanzania, kuendelea kuwepo au kutokuwapo kwa hukumu ya kunyoga bado ni mjadala unaoendelea.

Akasema huko nyuma iliwahi kufanyika kura ya maoni kuhusu suala hilo. Matokeo ya kura hiyo yalidhihirisha kwamba bado wananchi walio wengi wanataka hukumu hiyo iendelee , huku idadi kubwa pia ikitaka hukumu hiyo ifutwe.

"kwa upande wa Tanzania, uamuzi wa kuwapo au kuto kuwapo kwa hukumu ya kunyonga bado lina mjadala wa aina yake. Na kwa kweli si kazi ya mahakama kuifuta adhabu hiyo, ni jukumu la chombo kingine ambacho ni Bunge. Lakini pia bado kuna mawazo tofauti miongoni mwa wananchi" akasema Jaji Mkuu.

Hata hivyo akasema kutokana na namna ambavyo mwenendo wa kimataifa umekuwa ukiichukulia hukumu hii ya kunyonga kama ukiukwaji wa haki za binadamu.Ana uhakika kwamba baada ya miaka kadhaa nchi nyingi zitakuwa zimeondokana na adhabu hii.

Akasema kuwa ingawa Tanzania inayo na hii ya kunyonga, lakini utekelezaji wake ni mdogo sana. Kwa mfano akasema Rais wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete hawajawahi kusaini hati za watu kunyongwa.

Katika hatua nyingine Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Othman Chande amesifu uhusiano mzuri uliopo baina ya mihimili mitatu yaani, serikali, Bunge na Sheria na kwamba angalau hakuna muingiliano kati ya vyombo hivyo.

Katika mazungumgo yake na Maofisa hao, Mhe. Jaji Mkuu amewapongeza maofisa hao wa Ubalozi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na kwamba utendaji wao wa kazi umeijenga sifa kubwa Tanzania mbele ya Jumuia ya Kimataifa.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Nape Nnauye Azuru Kaburi La Baba Yake, Ateta na Rais Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete akiagana na viongozi wa ngazi za juu wa CCM baada ya mazishi ya Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Uhuru FM Juma Penza, jana katika makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimwagilia maji kwenye kaburi la Baba yake Marehemu Mussa (Mosses) Salum Nnauye kwenye makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam, jana.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye kaburi la Baba yake Marehemu Mussa (Mosses) Salum Nnauye kwenye makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam, jana.Picha Zote na Mdau Picha zote na Bashir Nkoromo-Uenezi CCM
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Mpasuko CCM sasa dhahiri

MWENYEKITI ARUSHA AMSHAMBULIA NAPE,AMWITA MUASI WA KWANZA, WARIOBA AONYA




Waandishi Wetu
HALI imezidi kuwa tete ndani ya CCM na sasa mpasuko ambao umekuwa ukitajwa kukigawa chama hicho kikongwe nchini ni dhahiri. Hali hiyo inatokana na hatua ya makada na viongozi wake waandamizi kurushiana maneno makali nje vikao vyake rasmi kama ambavyo awali kilikuwa kimejenga msingi imara wa taratibu za kumaliza mambo yake ya ndani kimyakimya.

Jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole aliibuka na kumshambulia hadharani Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akimwita: “Muasi namba moja.” Nangole alikuwa akijibu kauli ya Nape aliyoitoa wiki hii akisema ndani ya chama hicho kuna kundi la waasi wanaokihujumu chama na hasa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Akijibu shutuma hizo jana, Nape alisema: “Ukirusha jiwe kwenye giza, halafu ukasikia mtu akiguna ujue huyo ndiye uliyemponda. Sasa mimi kwenye press release (taarifa kwa vyombo vya habari) sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa iweje yeye leo aanze kujibu?”

“Ninamheshimu sana Mzee Nangole lakini sidhani kama waliomshauri kutoka wamemshauri sawasawa, kama anaweza namshauri akasome taarifa yangu halafu aje tena kwenye press (vyombo vya habari), atazungumza vizuri,” alisema Nape.

Malumbano hayo baina ya Nangole na Nape wote wakiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), yamekuja siku moja tu tangu mwanasiasa mkongwe nchini, Jaji Joseph Warioba alipovionya vyama vya siasa nchini hususan chama hicho tawala kutokana na kile alichokiita kuwa ni “kukosekana kwa nidhamu ya kuzungumza.”

Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1), Warioba alisema hali katika vyama vya siasa inasikitisha kwani kumekuwa na malumbano makali baina ya viongozi.

Jaji Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu alisema hali hiyo inakiathiri zaidi CCM ambacho ni chama tawala na akahoji sababu za kuachwa kwa misingi ya mwanzo ya kuzungumza kwa nidhamu mambo yanayokihusu chama hicho.

“CCM kinaathirika zaidi na hali hii ya kutokuwepo kwa nidhamu ya kuzungumza ndani ya vyama, maana chenyewe kiko madarakani, unashangaa kimetokea nini kwa chama ambacho kilikuwa na nidhamu ya hali ya juu ya kuzungumza,” alisema Warioba.

Kauli ya Nangole
Nangole katika mkutano wake na waandishi wa habari jana alimtaka Nape aachane na malumbano yasiyo na tija ndani ya chama na badala yake asisitize utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani malumbano hayo yanaashiria dalili mbaya za anguko la chama hicho siku zijazo.

Alimtaka Nape ajikite kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na chama hicho badala ya kuendeleza malumbano kila kukicha.
“Tufanye shughuli za kukijenga chama. Mimi nilidhani Nape atakuwa akisisitiza utekelezaji wa Ilani za chama lakini yeye kila siku ni 'gamba, gamba tu.' Haya yatatufikisha wapi? Watu wanataka maendeleo,” alisema Ole Nangole. Alisema ndani ya CCM kwa sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ambayo yanasigana bila tija huku akionya kuwa dalili hizo za makundi zitaifikisha pabaya.

Akizungumzia kauli ya Nape kwamba kuna uasi ndani ya CCM, Mwenyekiti huyo wa Mkoa alisema ikiwa ni kweli, basi uasi wa kwanza ulifanywa na Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, kwani aliwahi kutajwa kuwa mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).

Alisema mara kwa mara Nape amekuwa akituhumiwa na baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa Mbunge wa Kishapu, Shinyanga, Fred Mpendazoe kuwa ni miongoni waanzilishi wa CCJ na hivyo kutamka kuwa kama ni suala la uasi basi Nape huenda akawa wa kwanza kuasi CCM.

Ziara ya UVCCM
Mwenyekiti huyo alipongeza ziara iliyofanywa na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) hivi karibuni mkoani Arusha, ambayo kimsingi ndilo chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa.

Alisema ziara hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa ilipaswa kupongezwa kwa kufufua uhai wa chama wilayani Arusha badala ya kubezwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati huu, chama cha upinzani, Chadema kimeweka himaya yake maeneo mengi ya Mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, alisema chanzo cha migogoro hiyo ni chuki mbalimbali ndani ya CCM zinazosababishwa na vita ya urais mwaka 2015 na kwamba huenda ikakimaliza chama hicho kwa kukiweka pabaya kwenye uchaguzi huo.

“Chuki zote za kuchafuana ni maandalizi ya 2015 na hili ndilo linachangia kutumaliza. Hebu tutekeleze Ilani ya chama. Nawapa pole wanaosaka urais kwa sasa kwani bado mbali sana,” alisema.
Kauli ya Nape Kwa upande wake, Nape alikanusha kuzungumzia ziara ya UVCCM Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari: “Naomba nieleweke, sijawahi kuzungumzia ziara ya umoja wa vijana mkoani Arusha, kwa hiyo madai yoyote yanayohusiana na suala hilo si yangu kwa sababu wanataka kunihusisha na jambo ambalo sihusiki nalo.”

“Kama nilivyosema sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa kwa nini leo hii wasijibu wenyeviti wa Mwanza, Shinyanga, Morogoro au kwingineko na ajibu yeye?”

Kuhusu mbio za urais wa 2015, Nape alisema: “Sijui kwa nini haya mageuzi ya kujivua gamba yanapotajwa yanahusishwa na urais. Hili si sahihi hata kidogo. Kwa mfano, unanihusisha mimi Nape na wagombea watano, hata kama ningekuwa nashabikia hili, nitakuwa vipi na wagombea wote hawa?,”

Alisema Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama imekuwa na kazi nyingi za chama na si kutafuta mgombea wa urais wa 2015 na kwamba hao pengine wanaolizungumza kila wakati ndiyo wenye wagombea wao.

Alipoulizwa CCM kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa Nape alijibu: “Sasa ninyi mngekuwa mkinisaidia kuwahoji hao, kwamba wanazungumza kama kina nani, maana utaratibu wa chama unaeleweka na msemaji wa chama anafahamika.”

Kauli nyingine
Oktoba 12 mwaka huu, Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa kumeibuka kundi la watu wenye nguvu ya fedha wanaokisaliti chama kwa kuendesha propaganda za kupotosha dhana ya kujivua gamba.

Alisema kundi hilo linamhujumu pia Rais Kikwete lakini akasema chama kimejipanga kuwashughulikia wanaounda kundi hilo.

Alipotakiwa kutaja hujuma za kundi hilo dhidi ya Mwenyekiti wa CCM, Nape alisema: “Ni nyingi, moja ni kusambaza hoja ya kutaka nafasi ya urais itenganishwe na ile ya mwenyekiti wa chama.”

Nape ilitoa matamshi hayo siku chache tangu Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa atoe kauli ya kukikosoa chama na Serikali yake akiwataka makada wa CCM kuacha kuingilia siasa za Chadema na pia kuitaka itafute suluhu ya matatizo yanayokabili wananchi.

Benno alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara Mjini Arusha, eneo ambalo linaonekana kuwa chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa ndani ya CCM.

Mkutano huo ndiyo pia chimbuko la tukio la Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kusakwa na polisi kwa tuhuma kwamba alitoa matamshi yenye kuchochea vurugu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jeshi hilo linamsaka Ole Millya kuhusu kauli yake kwamba mtoto mmoja wa kigogo alitoa maagizo kwa polisi kuzuia UVCCM wasifanye mkutano siku hiyo.


Msuguano wa ndani
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na misuguano ndani ya chama hicho, huku kukiwa na kundi ambalo linadaiwa kuwa na ajenda dhidi ya utekelezaji wa falsafa kujivua gamba iliyopitishwa na NEC ya CCM ikiwataka watuhumiwa wa ufisadi kuachia nyadhifa zao.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema kundi hilo la waasi linaungwa mkono na wenyeviti wa CCM wa mikoa zaidi ya 10 na kwamba ndilo linalosukuma ajenda ya kutaka kutenganishwa kwa kofia ya Rais na Mwenyekiti wa CCM.

Habari zaidi zinasema kuwa baada ya uchaguzi wa Igunga, kundi hilo lilipata nguvu zaidi kutokana na kuanza kuungwa mkono na mmoja wa makada wa siku nyingi wa chama hicho kutoka moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Miongoni mwa mikakati ya kundi hilo ni kuhakikisha ajenda ya kuteganishwa wa nafasi hizo mbili inafanikiwa, kufutwa kwa mpango wa kujivua gamba na kumng’oa Nape katika nafasi yake ya sasa kwa madai kwamba anakiharibu chama.

Habari hii imeandikwa na Moses Mashalla, Arusha na waandishi wetu Dar
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Ikulu: Siyo JK ni Mkapa


Rais mstaafu Benjamin Mkapa


Waandishi Wetu, Dar na Moshi

IKULU imesema Rais Jakaya Kikwete hahusiki na utoaji wa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyotolewa na Mahakama kwa askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe.Kwa taarifa hiyo ya Ikulu, inamaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Benjamin Mkapa ndiyo iliyohusika na msamaha huo.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi haikumtaja moja kwa moja Mkapa lakini iliweka wazi kuwa uamuzi huo ulifanywa na serikali yake ambayo ilikuwa madarakani wakati polisi hao walipohukumiwa na Mahakama Kuu mwaka 1998. Mkapa alikuwa madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano, kuanzia 1995 na 2000 na kisha 2000-2005.

“Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.

Lengo la taarifa hiyo ya Ikulu ilikuwa ni kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti hili kuhusu polisi hao wawili kuachiwa huru hivi karibuni.Katika taarifa hiyo, Ikulu inapinga habari zilizotolewa na gazeti hili Jumatano na Alhamisi wiki hii zikidai kuwa Rais Kikwete ndiye aliyetoa msamaha huo baada ya kupunguza adhabu yao hadi miaka miwili.

Wakiwa askari wapelelezi, Koplo Juma Muswa na Konstebo Mataba Matiku walihukumiwa kunyongwa hadi kufa mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Luteni Jenerali Kombe Juni 30, 1996.

Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol, mali ya W. Ladwa kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Matiku alidai kuwa walitoka gerezani Mei, mwaka huu walikokuwa wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu yao ya kunyongwa, kabla ya Rais kuwaonea huruma na kuwapunguzia adhabu.

“Unajua baada ya Jaji kutuhukumu kunyongwa tulikata rufaa, Mahakama ya Rufani ambayo iliona ile hukumu ilikuwa ni sahihi ikasema tuendelee nayo hadi tulipoomba huruma ya mheshimiwa Rais,” alisema Matiku.

Matiku alisema jopo lililomshauri Rais lilipendekeza wapunguziwe adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha miaka miwili na kwa kuwa walikuwa mahabusu tangu 1998, kifungo hicho kilitosha.

Wakati hayo yakiendelea, baadhi ya wanasheria, wasomi na watu wa kawaida wametoa maoni tofauti wakishangazwa na uamuzi huo wa Ikulu wakihoji iweje Serikali iliyomtangulia Rais Kikwete itoe uamuzi wake na utekelezaji wake ufanyike miaka saba tangu utawala mwingine uingie madarakani.

“Kauli ya Ikulu si sahihi hata kidogo, nadhani wasaidizi hawakufanya vizuri kwa sababu Urais ni taasisi. Hata asipokuwepo Kikwete leo bado atakayefuata atazungumzia uamuzi uliofanywa naye akiwa Rais na siyo mtu binafsi,” alisema wakili mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Alisema uamuzi wa kuwapunguzia adhabu polisi hao ulifanywa kwa kuzingatia madaraka ya Rais aliyopewa Kikatiba chini ya Ibara ya 45 ya Katiba ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2008.

“Kwa nini Ikulu inapiga danadana wakati ni suala la kikatiba? Ikulu ilitakiwa kusema ni Rais fulani alifanya uamuzi huo kwa sababu umma unataka kujua lakini kutoa statement (taarifa) ambayo inaacha maswali mengi zaidi nalo ni jambo la hatari sana” alisema wakili huyo.

Mkazi mmoja wa Mailisita alikouawa Kombe, alisema jana kuwa anashangazwa na taarifa hiyo ya Ikulu kutoeleza ilivyokuwa akisema kama uamuzi haukufanywa na Rais Kikwete ilikuwaje utekelezwe katika kipindi chake wakati Mkapa alishaondoka madarakani 2005?

Ibara hiyo ya Katiba kifungu kidogo cha 1(a) na (b) kinampa Rais madaraka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama na hata kubadilisha adhabu yeyote kwa kosa lolote ili iwe adhabu tahafifu.

Mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yaliyotokea mkoani Kilimanjaro yaliibua minong’ono mingi kwamba huenda yalitokana na hatua ya marehemu kuonekana kuunga mkono upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 1995.

Kutokana na minong’ono hiyo, Serikali iliunda tume chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Damian Lubuva na Jaji Mussa Kipenka wakati huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali, kuchunguza tukio hilo.Hata hivyo, taarifa ya tume hiyo imeendelea kuwa siri hadi leo.

CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

‘JK hahusiki msamaha wa polisi waliomuua Kombe’

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ( picha kutoka maktaba).

Imeandikwa na Mwandishi Wetu


IKULU imekanusha taarifa kwamba Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha wa adhabu ya kifo iliyowakabili askari Polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumuua aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe, mwaka 1996.

“Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005,” ilisema taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jana kwa vyombo vya habari.

Ikulu ilikuwa ikizungumza taarifa za gazeti la Mwananchi, matoleo ya juzi na jana, zilizodai kuwa Rais Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari Polisi hao
waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.

“Gazeti hili (Mwananchi) limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na
Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungocha miaka miwili.

“Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu
ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani,”ilisema taarifa hiyo.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

JK AONGOZA MAMIA KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU JUMA PENZA


Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Juma Penza, mwandishi mkongwe na kada wa CCM aliefariki dunia Jumatano usiku katika hospitali ya Hindu Mandal baada ya kuugua


Rais Kikwete akiwa na baadhi ya wajukuu wa marehemu


Waombolezaji wakipokezana katika kuzika


Nape Nnauye akiwa mazikoni


Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa akishiriki katika mazishi


Naibu Mwenyekiti wa CCM (bara) Mh John Chiligati akiweka udongo kaburini


Mzee Athumani Janguo akimzika rafiki yake


Rais Kikwete akiweka mchanga kaburini
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Msikilize Ridhwan kikwete Akiongea kuhusu wimbo wa Izzo Bizzness..! wa naongea na Ridhwan

Ridhwan Kikwete

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»