Showing posts with label mbeya. Show all posts
Showing posts with label mbeya. Show all posts

BARABARA ZA MBEYA ZAFUNGWA NA WANANCHI, JESHI LAINGILIA KATI, RISASI ZASIKIKA MCHANA HUU

 Picha hazipo Clear sana kutokana na Mabomu kuwa Mengi wananchi wanaziba barabara kuzuia Magari yasipite 
 Maeneo ya Ilomba wananchi Bado wanafunga Barabara 
 Wananchi wamechoma matairi kuzuia usafiri wa aina yoyote usiwepo
Hapa ni Mamajoni ambapo Bara bara zimefungwa
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

POLISI WAZIMA MACHAFUKO TUNDUMA MKOANI MBEYA





Na Gordon Kalulunga.
Askali wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania katika mpaka wa Tunduma uliopo kati ya Tanzania na Zambia, wamefanikiwa kuzima machafuko yaliyokuwa yameanza kati ya wasafirishaji wa Tanzania na Zambia.

Sakata hilo lilitokea juzi kuanzia majira ya saa 2 asubuhi na kumalizika majira ya saa 9 alasiri ambapo wasafirishaji wa upande wa Tanzania walikuwa wakinyang’anya funguo za magari ya raia wa Zambia waliokuwa wakivuka mpakani hapo kwa kile walichodai kuwa walichoshwa na manyanyaso.

Walisema kuwa raia wa Zambia wamekuwa wakiwapiga wasafirishaji kutoka upande wa Tanzania hasa wanaosafirisha kwa kutumia Bajaji na pikipiki maarufu kama Bodaboda wanapovuka kwenda eneo la Nakonde kupeleka abiria jambo ambalo walilipeleka polisi mara kadhaa lakini walikuwa wakipuuzwa.

Wasafirishaji hao walisema kuwa tabia hiyo ya wasafirishaji wa upande wa Zambia imedumu kwa takribani muda wa miezi miwili sasa hivyo nao waliamua kujichukulia hatua mikononi ili Serikali za pande zote mbili zichukue hatua kudhibiti maonezi wanayotendewa.

Baada ya hali hiyo kuwa tete, Askari wa Jeshi la polisi katika kituo cha polisi kilichopo Tunduma waliamua kujitokeza na kuwaomba wasafirishaji hao kutoa kero zao na kile kilichosababisha waanze kujichukulia hatua ili kuwadhibiti raia wa Zambia kutoingia na usafiri wao upande wa Tunduma ambapo wasafirishaji hao walitii ombi hilo.
Askari Polisi hao wenye vyeo mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa kituo hicho Aly Wendo waliwasihi wasafirishaji hao kuacha kufanya hivyo kwa kile walichodai kuwa malalamiko yao yalikuwa ya Msingi lakini wakawaonya kuwa ni muhimu wakaheshimu sheria za nchi zingine.

‘’Tunawashukuru kwa uelewa wenu na kutoa malalamiko bila kuficha na sisi kwasababu tunajua maana ya ujirani mwema na askari wa upande wa pili wanauelewa mzuri hivyo mimi ninaenda kule upande wa pili kuwaeleza wenzangu kuwa kuna jambo hilo hivyo atakayepigwa kuanzia sasa aje kwangu tunavuka nae na kuwakamata wale watakao husika’’ alisema Wendo.

Kwa upande wake Inspector Chaburuma na askari wengine ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja waliwafafanulia wasafirishaji hao kuwa sheria za nchi ya Zambia hazitambui usafiri wa Bodaboda na bajaji hivyo ni muhimu wakaheshimu suala hilo licha ya kuwepo mazoea ya ujirani mwema.

Kwa upande wao wasafirishaji hao zaidi ya 100 waliokuwa wametoka eneo la mpaka huo walipokuwa wamezingira na kisha kuelekea katika kituo cha polisi baada ya kuombwa na askari polisi wa Tunduma waliwahakikishia askari hao kuwa wamekubaliana na ushauri huo na hasa kutokana na Mkuu huyo wa kituo kuonesha utu wa kufuatilia upande wa pili ili kumalizwa kwa mgogoro unaoweza ukuathiri uchumi wa watu wanaotegemea mpaka huo.
Msafirishaji Hamad Omary alisema kuwa kutokana na kueleweshwa na askari hao msafirishaji yeyote ambaye atakiuka makubaliano hayo wenzake hawatahusika na lolote.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI MBEYA NA MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro,baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Rukwa, katika hafla iliyofanyika jana, kijiji cha Mkutano wilayani Mbozi.




Askari wa kutuliza ghasia na skauti wakiulinda mwenge wa uhuru baada ya kuwasili viwanja vya Bomani wilayani Mbozi.


Mkimbiza Mwenge Kitaifa,Mtumwa Rashid Halfan, kutoka kaskazini Unguja, akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa Kiume wa Sekondari ya Mwalimu Jk.Nyerere iliyopo Tunduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakisikiliza wimbo wa kupinga Rushwa uliokuwa ukiimbwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihanda iliyopo Mozi wakati wa uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa shuleni hapo.

Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia baada ya mwenge wa uhuru kuwasili katika kijiji cha mkutano ambacho kipo mpakani mwa mkoa wa Rukwa na Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo (kulia), akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Evance Balama, baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake wilayani Mbozi.Makabidhiano hayo yalifanyika Songwe Viwandani mkoani beya.Mwenge huo mkaoni Mbeya utafungua miradi yenye thamani ya sh.bilioni 2.6 na Wilayani Mbozi umefungua miradi mitatu ya sh.milioni 156. 

(PICHA ZOTE NA DOTTO MWAIBALE)


[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WATU 30 WAJERUHIWA NA HAKUNA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSUSHA MAGARI MANNE MKOANI MBEYA


Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika ajali mbaya na hakuna aliyefariki iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Baadhi ya majeruhi kati majeruhi 30 wakiwa wameketi chini, wakiwaweshikwa na butwaa kushindwa kuamini kile kilichotokea baada ya kutoka salama katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo hakuna aliyefariki lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Mashuhuda waliofika eneo la ajali ambapo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Moja kati ya malori matatu yaliyosababisha ajali na kuziba barabara na hali iliyopelekea magari mengine kushindwa kupita  katika ajali mbaya, ambayo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali hiyo iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

AJALI MBAYA MKOANI MBEYA


MAJERUHI WA AJALI HIYO MBAYA ILIYOTOKEA MBEYA JANA.

MWILI WA MAREHEMU YUDA AMBOKILE UKIWA UMENASA KWENYE GARI.


Mmoja wa majeruhi


Na Ezekiel Kamanga.

Jinamizi la ajali mbaya limeendelea kuusakama mkoa wa Mbeya ambapo usiku wa kuamkia jana imetokea eneo la Mlima Nyoka Uyole Jijini humo na kuua watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo dogo Yuda Ambokile Jeshi la Polisi limethibitisha.


Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa anesema Marehemu wengine ni Peter Kishimba mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Tazara Iyunga na Joshua Sanga mwenye umri wa miaka 2 mkazi wa Uyole jijini Mbeya na ajali hiyo ilitokea majira ya saa Moja na nusu kwa kuhusisha gari Nne ambazo zote zilijeruhi watu waliokuwemo ndani yake.

Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuharibika kwa gari aina ya Toyota Dyana yenye namba za usajili T 660 AUX ambayo ilikuwa imeegeshwa katika mlima huo.

Walisema kuwa kutokana na kuharibika kwa gari hiyo ndipo gari dogo aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T 425 BAZ , iliyokuwa ikitokea barabara ya Mbarali kwenda Mbeya mjini ambayo ilikuwa na abiria watano iliigonga gari hiyo na kusababisha kifo cha Dereva wake Yuda Ambokile na wengine kujeruhiwa vibaya na magari mengine Toyota Cheser T 512 BCT na Nissan T 991 BAK.

Baada ya gari hiyo kugonga gari iliyokuwa imeegeshwa na kusababisha madhara hayo ndipo gari nyingine aina ya Baloon ikagongwa na gari hiyo aina ya Escudo kisha Baloon hiyo ikatumbukia korongoni na kusababisha majeruhi wawili waliokuwemo ndani ya gari hiyo ambao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Mmoja wao akaruhusiwa baada ya hali yake Kiafya kuimarika.

Ajali hiyo haikuishia hapo bali gari nyingine aina ya Pickup yenye namba za usajili T 991 BAK nayo ikakumbwa na dhahama hiyo ambapo iliharibika vibaya bila kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwemo ndani yake.

Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutembelewa na waandishi wa habari leo, wengi wao walikutwa wakiwa na hali mbaya na kushindwa kuzungumza chochote bali baadhi yao waliokuwa na nafuu walisema kuwa walikuwa hawakumbuki chochote juu ya ajali hiyo zaidi ya kujikuta wamelazwa wakiwa na majeraha katika miili yao.

Majeruhi hao ambao baadhi yao waliweza kuzungumza na waandishi wa habari ni pamoja na Denis Untwa (24) ambaye ni dereva wa Baloon, Laina John Sanga (35), Michael Mteve (20), Anania Simbeye(35) ambaye ni dereva wa Escudo, Emmanuel Tambikeni na mmoja aliyejitaja kwa shida jina moja la Boniface..
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 2 comments»

Abiria 30 wanusurika Kifo katika ajali mbaya iliyo tokea eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya



 Ajali ya gari ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya mpaka mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini,  ambayo imetokea mteremko wa Mbalizi ambapo zaidi ya abiria Thelathini wamenusurika kifo, baada ya gari kushindwa kupandisha mlima hali iliyopelekea kupinduka. Tukio hili limetokea siku ya Jumapili.
Baada ya kupinduka kwa gari hiyo ambayo hufanya tuti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya hadi Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini hatimaye lilinusurika kutumbukia bonde la mtoni Mbalizi yukio lililotokea siku ya Jumapili.

Jeshi la polisi Usalama barabarani Mbeya mnapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini magari yenye karoso kwa lengo la kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima  
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

RC MBEYA ABAS KANDORO ABAINI KUWEPO KWA KASORO KATIKA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI 2009/2010 ILEJE + MBEYA




Mkuu wa Mkoa Mbeya, Abbas Kandoro

Na mwandishi wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya imebainika kuwa na kasoro kadhaa katika taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2009/2010 licha ya kupata hati safi katika mwaka huo.

Kasoro hizo za mapungufu katika utendaji zinatokana na taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG zilizobainishwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kwenye kikao cha baralaza maalumu la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwa ajili ya kupitia taarifa hiyo.

Akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa Kandoro, amesema pamoja na halmashauri ya Ileje kupata hati safi yapo maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa ujumla na kuwekewa msisitizo ili kuongeza ufanisi.

Ameyataja maapungufu hayo kuwa ni kuhamisha fedha toka akaunti ya maendeleo kwenda akaunti za matumizi ya kawaida za zaidi ya shilingi milioni 99 na laki 9 na zaidi ya shilingi milioni 78 laki 8.

Akijibu hoja hizo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Glads Dyamvunye amesema baadhi ya kasoro zilizobainishwa kwenye taarifa hiyo tayari zimeafanyiwa kazi ikiwemo kurejeshwa kwa kiasi fedha za miradi zilizohamishwa kwenye akaunti yake.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MKAZI WA KIJIJI CHA MPEMBA - MBOZI MKOANI MBEYA AUWAWA KWA KUPINGWA RISASI.

Na mwandishi wetu
Mkazi mmoja wa kijiji cha Mpemba wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya John Mpembela mwenye umri wa miaka 55 ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana usiku

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Anacletus Malindisa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea majira saa moja na nusu usiku marehemu akiwa nje ya mlango wa nyumba yake.

Malindisa amesema marehemu ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kutumia bunduki aina ya shortgun ambapo katika mwili wake yamekutwa majeraha mbalimbali ya risasi na maganda yake.

Aidha Kaimu Kamanda amesema chanzo cha kuuwawa Bw. John hakijajulikana na hakuna aliyekamatwa na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi .
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

26 WAKAMATWA KWA UHALIFU WA UPIGAJI NONDO MKOANI MBEYA



Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakijiuguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.

*****

Na mwandishi wetu
Watu 26 wamekamatwa kwa kuhusika na matukio ya upigaji Nondo mkoani Mbeya ambapo watuhumiwa wamegawanyika katika makundi matatu huku kila kundi likiwa na watu 4 hadi 15.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ameyataja makundi hayo kuwa kundi la kwanza linawahusisha watu wanne ambao ni Herodi Luka, Musa Idi, Fadhili Luvanda na David Jimy waliosababisha vifo vya watu wawili.

Kundi la pili linawatu saba ambao ni Edson Ulendo, Rashidi Mwakyungwe, Elasto Eliasi, Musa Isa, Amosi Mziho, Sifa Jolewa na Frenk Kitonga ambao walisababisha kifo cha Pc Meshaki

Kundi la mwisho linawahusisha watu 15 ambao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba kundi la kwanza na la pili yamekubali kuhusika na matukio ya upigaji nondo.

Wakati huohuo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametoa shukrani kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa matukio ya upigaji nondo na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo vya uhalifu.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAlUMBANO YASABABISHA UKWASI WA MAENDELEO WILAYANI MBARALI.


Daraja la Kijiji cha Ijumbi, kata ya Ruiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya, ambalo hutumiwa na wananchi kuvuka kuelekea kijiji jirani, ambapo wananchi wengi wamekuwa wakifa kutokana na kuteleza. Mradi wa TASAF ulitoa msaada wa ujenzi wa daraja la uhakika lakini mpaka sasa kumekuwa na marumbano baina ya uongozi waHalmashauri ya mbarali, Kata husika na wananchi ya kwamba ni sehemu gani sahihi lapaswa kujengwa.
Serikali ngazi ya Mkoa ingilieni suala hili ili kunusuru madhara ya kifo kutokana na daraja hili marumbano mpaka lini.

Kwa tafti iliyofanywa na mtandao huu (mbeya yetu) umebaini kuwepo kwa marubano baina ya viongozi wa serikali ya kata, vijiji na wananchi, katika meneo ya kijiji cha Kanioga, Ijumbi, Nsonyanga, Mapogolo, Kapunga na Mawindi. Ambapo baadhi ya watendaji hutafuna fedha za miradi lakini hatua za kisheria hazichukuliwi dhidi yao
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»