Showing posts with label mwandosya. Show all posts
Showing posts with label mwandosya. Show all posts

WANANCHI WA JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI WAFANYA IBADA YA MAOMBI KUMWOMBEA WAZIRI PROF MWANDOSYA APONE MAPEMA



Prof Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa maji na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.
*****
Na mwandishi wetu
Wananchi wa Jimbo la Rungwe Mashariki wamefanya ibada maalum ya kumwombea Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni  Waziri wa maji Profesa. Mark Mwandosya ili apone haraka.

Baada ya ibada hiyo maalumu mmoja wa wakazi wa jimbo hilo Njwaba Mwakambinda amesema wananchi wa Kijiji hicho wanafarijika wanaposikia taarifa njema kuhusu hali ya afya ya Mbunge wao.

Naye mwenyekiti wa wataalamu mkoa wa Mbeya Prince Mwaihojo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa itikadi zao za kisiasa katika kuleta maendeleo katika Jimbo hilo na kuombeana mema badala ya kutumia siasa kuzushiana vifo.

Akijibu baadhi ya masuala yaliyojitokeza eneo hilo, Msaidizi wa Prof. Mark Mwandosya, Ndigwako Mwasandungila ambaye pia ni diwani wa kata ya Lwangwa amesema mbunge wao anaendelea vizuri na anaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi zake akiwa kwenye matibabu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAlUMBANO YASABABISHA UKWASI WA MAENDELEO WILAYANI MBARALI.


Daraja la Kijiji cha Ijumbi, kata ya Ruiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya, ambalo hutumiwa na wananchi kuvuka kuelekea kijiji jirani, ambapo wananchi wengi wamekuwa wakifa kutokana na kuteleza. Mradi wa TASAF ulitoa msaada wa ujenzi wa daraja la uhakika lakini mpaka sasa kumekuwa na marumbano baina ya uongozi waHalmashauri ya mbarali, Kata husika na wananchi ya kwamba ni sehemu gani sahihi lapaswa kujengwa.
Serikali ngazi ya Mkoa ingilieni suala hili ili kunusuru madhara ya kifo kutokana na daraja hili marumbano mpaka lini.

Kwa tafti iliyofanywa na mtandao huu (mbeya yetu) umebaini kuwepo kwa marubano baina ya viongozi wa serikali ya kata, vijiji na wananchi, katika meneo ya kijiji cha Kanioga, Ijumbi, Nsonyanga, Mapogolo, Kapunga na Mawindi. Ambapo baadhi ya watendaji hutafuna fedha za miradi lakini hatua za kisheria hazichukuliwi dhidi yao
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Dk. Mwakyembe kalishwa sumu?


KUNA taarifa za kutatanisha juu ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, huku baadhi ya vyanzo vikidai amelishwa sumu.
Taarifa zilizozagaa jana kupitia simu na mitandao mingine ya kijamii, zilidai kwamba kutokana na hali tete aliyokuwa nayo jana, mipango ilikuwa inafanyika kumsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Awali, taarifa zilisema amelishwa sumu; baadaye zikaja nyingine kwamba Dk. Mwakyembe amekula chakula kichafu kikamsababishia kuvimba mwili mzima.
Hata hivyo, gazeti hili lilipowasiliana na mmoja wa wadogo zake mkoani Mbeya, alisema taarifa hizo zilikuwa za kuzusha, kwa sababu za kisiasa.
Baadaye zilipatikana taarifa kutoka kwa ndugu zake wa karibu waliosema kwamba mbunge huyo wa Kyela hakulishwa sumu, bali anaumwa tu kawaida, na kwamba anaendelea vizuri.
Gazeti hili halikufika nyumbani kwake, na lilipomtafuta kwa simu iliita bila kupokewa, baadaye ikazimwa kabisa.
Chanzo kimoja cha habari kilichodai kimefika nyumbani kwake Kunduchi Beach, Dar es Salaam, kilisema: “Kwa kweli afya yake ni mbaya sana. Wizara inafanya mipango akachunguzwe nje ya nchi.”
Wakati hayo yakisemwa kuhusu Dk. Mwakyembe, katika hali isiyokuwa ya kiungwana, uvumi mwingine ulizagaa kuhusu afya inayodorora ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya, ambaye yupo India kwa matibabu.
Baada ya kuibuka tetesi kuhusu afya yake, huku nyingine zikienda mbali na kudai huenda amepoteza maisha, Profesa. Mwandosya alisikika akizungumza na mwandishi wa Radio One, akakanusha uvumi huo.
Katika mahojiano hayo ya simu, Profesa Mwandosya alisema uvumi huo unamwongezea maisha. Alisema anaendelea vizuri, akawashukuru wote wanaomwombea.
“Mimi ninaendelea vizuri, ni kwamba ukiona mtu anakutangazia kifo, basi ujue anakutakia maisha marefu… kwa sisi waumini na watu wa dini tunaamini hilo, hivyo ni jambo la heri, tunaomba waendelee kutuombea maisha marefu na hakuna mtu anayejua siku yake ya kufa… nimeshauriwa niwe karibu na wataalamu … vipimo vikikamilika nitatibiwa na kurudi nyumbani muda si mrefu,” alisema Profesa Mwandosya.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»