Showing posts with label polisi. Show all posts
Showing posts with label polisi. Show all posts

IGP SAID MWEMA AONGELEA UGAIDI AFRIKA MASHARIKI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu matukio ya vikundi vya kigaidi yanayoendelea katika nchi za Afrika mashariki.Kulia ni Kamishna wa Polisi,Utawala na Usimamizi wa Rasilimali za Jeshi Clodwig Mtweve.Picha na Michael Jamson




Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo katika makaomakuu ya Jeshil hilo jijini Dar es salaam.

1. Awali ya yote napenda niwashukuru kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo na hasa suala la kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa nchini. 

2. Nimewaiteni leo kwa ajili ya kutaka kuwapa taarifa za mambo mbalimbali zikiwemo za matishio ya ugaidi yaliyoanza kujitokeza katika nchi ya jirani ya Kenya, Uharamia unaojitokeza katika ukanda wa Bahari ya Hindi na matukio mengine yanayojitokeza yakiwemo ya ajali za barabarani. 

3. Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa wasiwasi wananchi juu ya Ugaidi unaoendelea katika nchi ya jirani ya Kenya, kwamba, tayari tumejipanga vyema kwa kuimarisha ulinzi na hasa maeneo yote ya mipakani na kazi hii inafanyika kwa ushirikiano na vyombo vingine vyote vya ulinzi na usalama. 

4. Vile vile, kuna matukio ya uharamia na uhamiaji haramu ambayo yamekuwa yakijitokeza katika ukanda wa Bahari ya Hindi hususani katika mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi. Katika kipindi cha mwaka huu maharamia wapatao 13 wamekamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani.

 5. Tunatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhali ya watu ama makundi ya watu watakaowatilia mashaka kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa ili hatua za haraka za kiusalama ziweze kuchukuliwa. 
Watumie namba za simu zifuatazo 0787 668306, 0222138177, 111, 112 na namba za Makamanda wa mikoa, wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCDs) na RTOs zilizokwishasambazwa hadi ndani ya mabasi. 

6. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa taarifa ambazo zimefanikisha kukamatwa kwa baadhi ya wahalifu hao. Tunawaomba wananchi wote kuiga mfano huo wa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kufichua uhalifu wa aina yoyote ile na hasa matukio ya kikatili yanayofanyika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na madereva wazembe wanaosababisha ajali barabarani.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KAMANDA SULEIMAN KOVA KUWA MGENI RASMI KTK PAMBANO LA MATUMLA NA MIYEYUSHO DIAMOND JUBILEE


MKUU WA POLISI KANDA MAALUM YA JIJI LA DAR ES SALAAM AMBAYE PIA NI MLEZI WA MCHEZO WA NGUMI TANZANIA KAMANDA SULEIMAN KOVA (PICHANI) ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA PAMBANO LA MASUMBWI LA UBINGWA WA MABARA WA UBO (UBO INTER-CONTINENTAL BANTAM WEIGHT CHAMPIONSHIP) KATI YA BINGWA MBWANA MATUMLA DHIDI YA FRANCIS MIYEYUSHO LITALALOFANYIKA HIVI KARIBUNI SIKU YA JUMAPILI TAREHE 30 MWEZI HUU KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE.


AKIZUNGUMZIA HILO KAMANDA KOVA ALISEMA KUBWA ZAIDI LILILOMFANYA AKUBALI KUWA MGENI RASMI NI KATIKA KUUNYANYUA MCHEZO HUU AMBAO HUWAKUTANISHA VIJANA WA RIKA MBALIMBALI KTK KUJITAFUTIA KIPATO HALALI NA KUEPUKANA NA TABIA ZA UPORAJI,UVUTAJI BANGI NA MADAWA YA KULEVYA PAMOJA NA KUWA KARIBU NA WANANCHI MBALIMBALI KATIKA KUTEKELEZA DHANA YA POLISI JAMII.


AKIZUNGUMZIA ZAIDI JUU YA PAMBANO HILO LITAKALOKUWA LA RAUNDI 12 MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD AMBAO NDIO WAANDAAJI MOHAMED BAWAZIR ALISEMA MAANDALIZI YA PAMBANO HILO AMBALO LIMEANDALIWA KATIKA UTARATIBU MZURI WA KIMATAIFA YANAENDELEA VIZURI NA KUTAKUWA NA MAPAMBANO MENGINE MATANO MAKALI YA UTANGULIZI IKIWEMO LA UBINGWA WA PST KATI YA JUMA FUNDI NA FADHIL MAJIA NA PAMBANO  LINGINE LITAKALOWAKUTANISHA KINA DADA ASHA NGEDERE NA SALMA KIOBWA WA MOROGORO.


 " NAWAHAKIKISHIA WAPENZI WOTE WA MCHEZO HUU HASA KINA MAMA WAJE KWA WINGI KUSHUHUDIA PAMBANO HILI NA KUTAKUWA NA ULINZI NA USALAMA WA HALI YA JUU" MILANGO ITAKUA WAZI KUANZIA SAA 10 ALASIRI.KWA WALE WANAOHITAJI TICKET ZA KUKAA ENEO MAALUM LA PRIMIER KWA 20,000 TU WANAOMBWA KUWASILIANA NA MUANDAAJI KUANZIA SASA KWANI ZIMETENGWA NAFASI CHACHE TU,VIINGILIO VINGINE VITAKUWA 10,000 NA 5000 AMBAPO TICKET ZITAPATIKANA MLANGONI SIKU HIYO.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KUMI NA MOJA MBARONI MKOANI SINGIDA.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Celina Kaluba akitoa taarifa ya kutiwa mbaroni kwa wachimbaji wadogo wa madini wa kijiji cha Sambaru jimbo la Singida mashariki kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha). (Picha na Nathaniel Limu).
                                                                            

                                                                                *******
Jeshi la Polisi mkoani Singida linawashikilia watu 11 kwa tuhuma ya kuingia katika eneo la mgodi wa dhahabu mali ya kampuni ya Shanta Mining uliopo katika kijiji cha Sambaru wilayani Singida bila kuwa na kibali halali cha kuingia humo.


Kamanda wa polisi mkoani Singida Celina Kaluba amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Oktoba 9 mwaka huu.


Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Gulas Mahiga(29) mkazi wa Bariadi, Mohamed Saidi (34) mkazi wa Mang’onyi, Maduhu Luhende (39) mkazi wa Bariadi, Steven Wambura (32) mkazi wa Bunda na Boniface Mbola (27) mkazi wa Misughaa.


Kaluba amewataja wengine kuwa ni Emannuel Lugumbika (31) mkazi wa Bariadi, Mwita Mtatiro (31) mkazi wa Musoma, Joseph Mtuti (27), Makenga Mduhu( 27) Emannuel Sawa (53) wote wawili ni wakazi wa Mwanza na Dotto Petero (28) mkazi wa Misigiri.


Akifafanua amesema Oktoba 8 mwaka huu walipata taarifa kwamba kuna kundi la watu limevamia eneo la mgodi wa dhahabu mali ya Kampuni ya Shanta Mining.


Amesema Polisi walipofika eneo hilo , waliwakuta wananchi hao wakiendelea kuchimba dhahabu na walipowataka waache kuchimba katika eneo hilo ambalo sio lao, wananchi hao walianza kufanya vurugu na kuanza kurusha mawe.


“Kitendo cha wananchi hao kurusha mawe, kilisababisha askari D.9800 Sajenti Ally kujeruhiwa mkono wa kushoto. Vurugu hizo zilidhibitiwa na polisi lakini mara kwa mara zilionekana kujirudia kutokana na wananchi hao kutokubali kuondoka katika eneo hilo ”amesema.


Kaluba amesema Oktoba 9 mwaka huu saa mbili asubuhi, kundi hilo la watu lilirudi tena katika mgodi wa Shanta Mining huku likihamasishana kwa kupiga kelele na kuanza kuwatupia mawe askari polisi.


“Kulikuwa hakuna namna nyingine isipokuwa polisi kuwarushia bomu la machozi na kufyetua risasi za moto hewani ili kuwatanya. Baada ya hapo, ndipo watuhumiwa 11 waliweza kukamatwa”,amesema Kaluba.


Kamanda Kaluba amesema baada ya upelelezi kukamilika, watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Polisi yamska kiongozi wa CCM Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, James Ole Millya

Filbert Rweyemamu na Happy Lazaro, Arusha
POLISI mkoani hapa inamtafuta Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, James Ole Millya baada ya kutoa matamshi ya kuchochea vurugu.Taarifa za polisi zilibainisha kwamba wanamsaka Ole Millya ili wamuhoji kuhusu kauli yake aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la St.Thomas Jumatatu wiki hii.

Katika mkutano huo, Ole Millya alidai kuwa mtoto mmoja wa kigogo alitoa maagizo kwa polisi Mkoa wa Arusha kuzuia wasifanye mkutano siku hiyo.

“Tumekuwa tukimtafuta tangu siku hiyo, simu zake hazipatikani na wakati mwingine akipatikana hapokei,tutahakikisha tunamkamata athibitishe kauli yake na tumjue huyo mtoto wa kigogo aliyemtaja ni nani.”alisema Kaimu Kamanda wa Polisi, Akili Mpwapwa.


Mpwapwa alisema Oktoba 7, mwaka huu, polisi Wilaya ya Arusha, lilipata barua kutoka UVCCM mkoa wakiomba wapewe kibali cha kuzindua matawi na kufanya mkutano wa hadhara Oktoba 9, wakati maombi yao yanashughulikiwa Katibu wa UVCCM mkoa, Abdalla Mpokwa,alitoa taarifa ya kuahirisha shughuli hiyo.

Alisema katika hatua ya kushangaza UVCCM walizindua matawi manispaa ya Arusha na kufanya mkutano wa hadhara ambao haukuwa na kibali cha polisi.

Alipotakiwa na waandishi wa habari kueleza ni hatua gani polisi itachukua dhidi ya UVCCM kufanya mkutano bila kibali, alitoa onyo kali kwa vyama vya siasa kutii sheria na taratibu na kwamba halitasita kuchukua hatua watu watakaokahidi utaratibu huo.

Katika mkutano huo,viongozi kadhaa wa umoja huo akiwamo Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa,Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Jamal Ally, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa James Ole Millya na Mbunge wa Viti Maalumu (vijana), Catherine Magige walihutubia mkutano huo.

Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa polisi wilaya lilikuwa limejizatiti kuhakisha mkutano huo haufanyiki, huku magari kadhaa ya askari yakirandaranda kabla ya kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo ya kiongozi wa juu wa wizara ya mambo ya ndani kuamuru wasibugudhiwe kwenye mkutano wao.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,James Ole Millya alipotafutwa kueleza juu ya kutakiwa kutoa maelezo polisi, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Chanzo: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»