Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, James Ole Millya
Filbert Rweyemamu na Happy Lazaro, Arusha
POLISI mkoani hapa inamtafuta Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, James Ole Millya baada ya kutoa matamshi ya kuchochea vurugu.Taarifa za polisi zilibainisha kwamba wanamsaka Ole Millya ili wamuhoji kuhusu kauli yake aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la St.Thomas Jumatatu wiki hii.
Katika mkutano huo, Ole Millya alidai kuwa mtoto mmoja wa kigogo alitoa maagizo kwa polisi Mkoa wa Arusha kuzuia wasifanye mkutano siku hiyo.
“Tumekuwa tukimtafuta tangu siku hiyo, simu zake hazipatikani na wakati mwingine akipatikana hapokei,tutahakikisha tunamkamata athibitishe kauli yake na tumjue huyo mtoto wa kigogo aliyemtaja ni nani.”alisema Kaimu Kamanda wa Polisi, Akili Mpwapwa.
Mpwapwa alisema Oktoba 7, mwaka huu, polisi Wilaya ya Arusha, lilipata barua kutoka UVCCM mkoa wakiomba wapewe kibali cha kuzindua matawi na kufanya mkutano wa hadhara Oktoba 9, wakati maombi yao yanashughulikiwa Katibu wa UVCCM mkoa, Abdalla Mpokwa,alitoa taarifa ya kuahirisha shughuli hiyo.
Alisema katika hatua ya kushangaza UVCCM walizindua matawi manispaa ya Arusha na kufanya mkutano wa hadhara ambao haukuwa na kibali cha polisi.
Alipotakiwa na waandishi wa habari kueleza ni hatua gani polisi itachukua dhidi ya UVCCM kufanya mkutano bila kibali, alitoa onyo kali kwa vyama vya siasa kutii sheria na taratibu na kwamba halitasita kuchukua hatua watu watakaokahidi utaratibu huo.
Katika mkutano huo,viongozi kadhaa wa umoja huo akiwamo Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa,Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Jamal Ally, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa James Ole Millya na Mbunge wa Viti Maalumu (vijana), Catherine Magige walihutubia mkutano huo.
Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa polisi wilaya lilikuwa limejizatiti kuhakisha mkutano huo haufanyiki, huku magari kadhaa ya askari yakirandaranda kabla ya kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo ya kiongozi wa juu wa wizara ya mambo ya ndani kuamuru wasibugudhiwe kwenye mkutano wao.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,James Ole Millya alipotafutwa kueleza juu ya kutakiwa kutoa maelezo polisi, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Chanzo: MWANANCHI

Categories:
ccm,
james ole millya,
polisi