Showing posts with label simba. Show all posts
Showing posts with label simba. Show all posts

SIMBA HAINA IMANI NA MWAMUZI ODEN MBAGA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SIMBA SPORTS CLUB (SSC) imetatizwa na hatua ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumteua mwamuzi Oden Mbaga kuchezesha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga Jumamosi ya Oktoba 29 mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa Oden Mbaga ndiye mwamuzi aliyechezesha pambano la mwisho la watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.
Pambano hilo nusura lisababishe vurugu baada ya Mbaga kukataa bao la wazi la Simba lililofungwa na Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 73 ya mchezo huo uliochezwa Machi mwaka jana.

Alibadili maamuzi yake na kukubali baada ya ama kulalamikiwa na washabiki na wachezaji wa Simba au kwa kujionea mwenyewe picha za marudio zilizoonyeshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini zilizothibitisha kuwa goli hilo lilikuwa halali.

Udhaifu huo wa kimaamuzi ungeweza kusababisha maafa makubwa uwanjani.
Ndiyo maana, Simba imetatizwa na uamuzi wa TFF kumteua tena Mbaga kuchezesha mechi hiyo, pamoja na makosa yake ya wazi aliyoyafanya katika mechi hiyo kubwa.

Simba Sports Club haina imani tena na Oden Mbaga kutokana na historia yake katika mapambano yaliyopita dhidi ya timu yetu.

Kwa taarifa hii, Simba SC inapenda kuutangazia umma kuwa japo haina imani na Mbaga, haitasusia pambano hilo kwa namna yoyote ile lakini inapenda kuweka wazi msimamo wake huo kuhusu mwamuzi huyu.

Ni matumaini yetu kuwa ujumbe huu utamfikia Oden Mbaga mwenyewe na wote waliohusika katika kumpanga awe mwamuzi katika pambano hilo.

Tunatanguliza shukrani.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba SC
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

SIMBA YATEMBEZA KICHAPO KATIKA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA: YAIBAMIZA RUVU SHOOTING BAO 2-0


 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Ruvu shooting.
 Wachezaji wakisalimiana kabla ya mchezo.
 Juma Jabu akikontroo mpira ili amtoke beki wa timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Azam jijini Dar.Simba imeshinda bao 2-0 na kujikita kileleni moja kwa moja.
 Moja ya hekaheka zilizotokea katika lango la Ruvu Shooting
 Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Simba, Ulimboka Mwakingwe (shoto) akichuana na beki wa Ruvu Shooting, Paulo Ngalema katika mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Azam huko Chamazi,jijini Dar.Simba imeshinda bao 2-0
 Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akichuana na beki wa Ruvu Shooting, Idd Nyambiso.
 Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi chini wakati wa hekaheka za kuwania mpira na George Michael wa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika leo kwenye uwanja wa Azam,jijini Dar.
 Emmanuel Okwi akichuana na mabeki wa Ruvu Shooting.
 Boban akimiliki mpira.
Mashabiki wa simba wakichagiza ushindi leo katika dimba la Chamazi.
Vuvuzela hazikuwa nyuma.Picha na Francis Dande.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Basena apika dawa ya African Lyon

KOCHA wa Simba, Moses Basena


DORIS MALIYAGA

KOCHA wa Simba, Moses Basena, amewaandaa nyota watatu kwa ajili ya kubeba mikoba ya Victor Costa "Nyumba" wakati timu hiyo itakapoikabili African Lyon katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa Uwanja wa Taifa kesho Jumapili jijini Dar es Salaam.

Kiungo Patrick Mafisango, ambaye ameifungia timu hiyo mabao manne, ni mmoja wa waliotayarishwa kwa ajili ya kazi hiyo maalum. Wengine ni Jerry Santo, ambaye pia ni kiungo na beki Obadia Mungusa aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar.

Watatu hao wamepewa mafunzo maalumu na Basena ili kuziba pengo la Costa, aliyeko nje ya uwanja kutokana na kuumia msuli wa paja, huku kukiwa na pengo pia la Kelvin Yondani aliyeingia mitini na Amir Maftah ambaye ni majeruhi.

Akizungumza kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko Bamba Beach, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Basena hakuweka wazi nani hasa atacheza nafasi ya Costa, lakini alieleza ana imani na wote watatu kwa mbinu na mazoezi aliyowapa.

"Kila mmoja wao yuko katika kiwango cha kufanya kazi nzuri ya kutupatia ushindi," alisema Basena ambaye timu yake yenye pointi 18 inataka kuwapiku vinara JKT Oljoro inayoongoza ligi ikiwa na pointi 19.

"Tuna Mafisango, Santo na Mungusa, wanaoweza kucheza nafasi ya Costa, ninachofanya ni kuwaangalia kujua nani kati yao atafaa zaidi,"alisema Basena, ambaye alitamba kuwa timu yake ipo vizuri kutokana na kuwa katika kambi tulivu na kufanya wachezaji kushika haraka kile anachofundisha tofauti na wakiwa mjini penye vurugu nyingi.

Basena kwa sasa anakuna kichwa kusaka mtu wa kucheza na Juma Nyosso, ambaye ndiye beki pekee mzoefu aliyesalia kufuatia kutoweka kwa Yondani, ambaye katika siku za karibuni hajakuwamo katika mipango ya Basena.

Wakati Nyosso akiwa na Taifa Stars huko Morocco, Basena aliwachezesha kwa vipindi tofauti Mungusa na Shomari Kapombe, Jerry na Mungusa kwa nafasi hiyo ili kuangalia kombinesheni.
Alipofanya hivyo, Mafisango alicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji wakati timu hiyo ilipotoka sare ya bao 1-1 na Azam kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa asubuhi ya Jumatatu iliyopita.

Basena alidokeza pia anawaangalia wachezaji waliokuwa katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja na Nassor Said "Chollo" waliokuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, pamoja na Gervais Kago aliyekuwa na kikosi cha Afrika ya Kati.

Alisema kuwa anawafuatilia wachezaji hao kisaikolijia kuona kama hawajaathirika baada ya timu zao kushindwa kufuzu kutinga fainali hizo zitakazochezwa mwakani huko Gabon na Guinea ya Ikweta.

Akizungumzia mchezo dhidi ya African Lyon, Basena alisema kuwa ana matumaini makubwa ya ushindi kwani ameishaipeleleza timu hiyo, ambayo inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi tisa.
"Si kwamba African Lyon ni mbovu, lakini nilivyoiona inafungika tu," alisema Basena, ambaye alikuwapo uwanja wa Chamazi wakati Lyon ilipofungwa na Kagera Sugar mabao 2-1.

Kuhusiana na majeruhi, Basena alieleza kuwa Salum Machaku na Mwinyi Kazimoto wanakaribia kurejea uwanjani. Ambao hali zao bado ni Costa na beki wa kushoto, Amir Maftah, ambaye pengo lake uwanjani litazibwa na Juma Jabu.

Katika mechi nyingine ya Ligi Kuu leo Jumamosi, Azam itaikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi, ulio nje kidogo ya Dar es Salaam.
Azam inatazamiwa kumrejesha uwanjani raia wa Ivory Coast, Kipre Tchetche, ambaye kwa muda sasa amekuwa majeruhi.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»