Showing posts with label urais 2015. Show all posts
Showing posts with label urais 2015. Show all posts

CCM wakiri hawakustahili ushindi


NAPE ASEMA WAMEPENYA TUNDU LA SINDANO



Na Efracia masaweCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekiri kuwa hakikustahili kushinda katika uchaguzi mdogo uliomalizika jimboni Igunga mwanzoni mwa mwezi huu.

Badala yake, kilisema waliopaswa kushinda ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kilikuwa kinaungwa mkono na wananchi wengi.
Hata hivyo, CCM imedai kwamba ushindi wake Igunga umetokana na CHADEMA kutumia vitisho, ikiwamo kumkamata na kumwadhibu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, aliyekutwa anakula njama za ushindi wa CCM.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, katika mkutano wa mapokezi ya mbunge aliyechaguliwa, Dk. Peter Kafumu, katika viwanja vya Bakhresa, Manzese, Dar es Salaam.
Dk. Kafumu alishinda kwa tiketi ya CCM kwa kura 26,484 dhidi ya 23,260 za mgombea wa CHADEMA, Joseph Kashindye. Vyama vingine sita, kikiwamo CUF, vilipata kura chache sana ambazo katika jumla yake hazifiki hata 2,800.
Nape alisema: “Kama CHADEMA wasingejihusisha na vitendo vya kikatili, basi leo hii chama hicho kingekuwa madarakani. Nakiri wazi kuwa CHADEMA wangeweza kuchukua kura zaidi ya 5,000 Igunga…
“Tumeshinda kupitia tundu la sindano, hiyo ipo wazi kabisa… CHADEMA waliwateka wananchi kwa asilimia zote. Kosa lao la kwanza waliwakashifu siku moja kabla ya kupiga kura kwa kuwaleta wasomi ili waje wahesabu kura kwa usahihi, hapo ndipo tatizo lilianza.”
Alisema CHADEMA ilikuwa imewateka wananchi wa Igunga, lakini baadaye walikerwa na kitendo cha chama hicho kuingiza walinzi wa kura kutoka nje ya jimbo.
“Nawahakikishieni baadhi ya wanachama waliokerwa na kitendo hicho cha kutokuaminiwa, kiliwafanya kundi kubwa la wanachama hewa wakichague chama cha CCM, tukaongezewa kura, ” alisema Nauye.
Naye Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Kafumu alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote waliomchagua na akaahidi kuwa nao bega kwa bega katika ufanisi wa kazi.
“Nitawatumikia bila ubaguzi wa chama au mtu yeyote. Nawashukuru kwa kila jambo na Mungu awabariki katika shughuli zenu; naomba tuendelee kushikamana,” alisema Kafumu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Makundi ya urais 2015 zaitafuna UVCCM

Mussa Juma, Arusha.
MAKUNDI  ya vigogo wanaowania urais mwaka 2015, ndani ya CCM yamezidi kuugawa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), baada ya Kaimu Mwenyekiti wake, Beno Malisa na viongozi wengine wa kitaifa kujikuta wakikwama kufungua matawi ya umoja huo mjini hapa jana.

Malisa aliyekuwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Jamal Ally, mbunge wa vijana CCM, Catherine Magige pamoja na vigogo kadhaa wa umoja huo,  jana walikuwa wazindue matawi 16 ya vijana katika Manispaa ya Arusha, lakini uongozi wa UVCCM wilaya ukagoma.

Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Godfrey Mwalusamba walipinga ujio wa ghafla wa vigogo hao na kufanya kazi ya kuzindua matawi huku uongozi wa umoja huo  wilaya ukiwa hauna taarifa.

Mwalusamba pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya hiyo, walitoa uamuzi huo katika kikao kilichozua malumbano ambacho kilifanyika juzi, ofisi ya UVCCM Mkoa.

Jana, Mwalusamba alithibitisha kupinga kazi ya ufunguaji matawi hayo ya UVCCM kwa maelezo kwamba, walikuwa hawana taarifa za kazi hiyo.

 "Wanasema mimi natumiwa na kundi moja la wanaogombea urais, hapana labda  wao ndio wanatumiwa, itakuwaje wafike hadi wilayani kwangu na kufanya kazi kwenye kata, bila taarifa hata hizo kata hawana taarifa,"alisema Mwalusamba.Kazi ya uzinduzi wa matawi hayo, ulikuwa umepangwa kufanyika katika Kata za Sokone One,Sombetini, Kaloleni, Sekei na Elerai, lakini haikufanyika licha ya kuwa tayari mabango na baadhi ya vijana walikuwa wamejiandaa.


Kauli ya UVCCM Mkoa Arusha 
Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, Ally Benanga ambaye ni mmoja wa waliokuwa waandalizi wa kazi ya ufunguaji wa matawi, alituhumu baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Arusha kutumiwa kukihujumu chama.

"Hawa ni wasaliti, tulikuwa tayari tumewaandaa vijana, tumetengeneza mabango sasa wamegomea, tunajua wanatumiwa na kundi moja la urais na Chadema kudhoofisha CCM Arusha,"alisema Benanga.

          
Hata hivyo, Katibu wa UVCCM  Mkoa wa Arusha, Abdul Mpokwa alipotakiwa kuelezea mtafaruku huo, licha ya kukiri kuahirisha zoezi hilo, lakini alikataa kufafanua zaidi chanzo chake.

"Ni kweli leo (jana) tulikuwa na kazi hiyo ila tumeahirisha na tutaifanya siku nyingine, "alisema Mpokwa.

Katibu huyo, hata hivyo, alikataa kuelezea ni hatua zipi watachukuliwa viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha ambao waligomea zoezi hilo kwa maelezo kuwa walikuwa hawana taarifa.

“Naomba uwasiliane na Katibu wa Mkoa Mary Chatanda yeye ndiye msemaji wetu katika chama,”alisema Mpokwa.

Malisa akana kutumiwa na makundi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, Malisa alikiri kuahirishwa jana kufanyika kazi ya uzinduzi wa matawi hayo kwa kile kilichoelezwa siyo siku nzuri.


Hata hivyo, alisema taarifa alizopewa na mkoa ni kuwa kazi hiyo itafanyika leo huku akikanusha kutumiwa na makundi. "Sidhani hapa kuna  makundi,  ufunguzi wa matawi ni kuimarisha chama na madai kuwa wilaya haina taarifa sisi haituhusu kwani uongozi wa Taifa unawasiliana na Mkoa,"alisema Malisa.


Tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, CCM Mkoa wa Arusha kimekuwa katika vurugu kubwa za makundi ambayo yanadaiwa kusababisha kuangushwa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha, Dk. Batilda Burian.



CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»