BALOZI JUMA VOLTER MWAPACHU AFIWA NA MWANAE, WENGI WAFIKA MSIBANI KUMPA POLE


Waziri Mkuu Mstaafu Mh Cleopa David Msuya akimpa pole Balozi
Juma Volter Mwapachu kwa kufiwa na mwanae, Harith



Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya akisaini kitabu cha rambirambi ya kufariki kwa Harith Mwapachu, mtoto wa Balozi Juma Volter Mwapachu (kulia) nyumbani wa wafiwa Mikocheni jijini Dar. Karibu yake ni kaka wa Balozi, Mh. Bakari Mwapachu akifuatiwa na Mzee Hashim Mbita


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye ni mtoto wa Juma Mwapachu, aliyefariki dunia leo asubuhi.Kulia ni Balozi Juma Mwapachu.


Balozi Juma Volter Mwapachu akipewa pole na marafiki zake waliokwenda kumpa pole msibani



Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akipokewa na Dkt Hellen Otaru alipowasili msibani


Balozi Juma Volter Mwapachu akifarijiwa na Mh Freeman Mbowe


Mh Bakari Harith Mwapachu akiongea na Mzee Hashim Mbita (kulia) na Mh Freeman Mbowe msibani

Categories: