'Bifu' la C-Pwaa, Suma Lee laendelea


CPWAA


SUMA LEE

Imeandikwa na Evance Ng’ingo;


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Alfan Ilunga (C-PWAA) amesisitiza kuwa hayupo tayari kufanya kazi tena na msanii rafiki yake wa siku nyingi, Ismail Sadiki (Suma Lee).

C-Pwaa aliliambia gazeti hili kuwa, Suma Lee ni rafiki yake na wametoka wote kimuziki tangu wakiwa na kundi la ParkLane mwaka 2003 mpaka 2006.

Alisema, hali hiyo ya kutokuelewana mpaka kufikia uamuzi huo imekuja kufuatia kumsikia Suma Lee akizungumza maneno ya kejeli katika kituo kimoja cha Redio.

Alisema, licha ya kutoimba pamoja kwa takribani miaka mitano sasa lakini yeye kama C-Pwaa alikuwa na nia ya kurudisha umoja wa kundi lao hilo.

C-Pwaa kwa sasa yupo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za muziki za Chanel O, anawania kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki.

Wakati C-Pwaa akiwa amefikia mafanikio hayo msanii Suma Lee kwa sasa anatamba na kibao chake cha Hakunaga.

Kibao hicho cha Hakunaga kimeweza kushika chati katika vituo mbalimbali vya radio na runinga ambapo msanii huyo amekuwa kivutio na ameweza kurudi kwa kasi katika medani ya muziki.

Aliwahi pia kutamba na kibao cha Chungwa na pia wimbo wa Ice-Crean alioshirikishwa na Noorah mwaka 2005 na 2007.

Chanzo: Habari Leo

Categories: , ,