CHINA YAKABIDHI BAISKELI NA MIPIRA LEO


 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.) akipewa maelezo na Balozi wa China nchini, Bw. Liu Xinsheng  (aliyeinama) kuhusu Baiskeli zilizotolewa kwake na Ubalozi huo.  Ubalozi huo pia umemkabidhi  Waziri mipira 300 kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu. Aidha, Ubalozi wa China umetoa  vifaa vya michezo ya  Kichina kwa Chama cha Wushu Tanzania. Vifaa hivyo vimetolewa leo katika Ubalozi wa China.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.) na Balozi wa China nchini, Bw. Liu Xinsheng, wakipeana hati za makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini leo katika Ubalozi huo. (Picha na Concilia Niyibitanga- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)

Categories: ,