Washiriki wa Miss Utalii mkoa wa Mara wakiwa jukwaani |
Fainali za kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2011/12 zimeanza kupamba moto, katika ngazi mbalimbali ikiwemo ngazi za Mikoa ambapo hivi karibuni mkoa wa Mara ulipata mshindi wa Taji la Miss Utalii Mara 2011/12 katika fainali zilizo fanyika katika ukumbi wa Bwalo la Magereza Musoma,na kushirikisha jumla ya warembo 12. Katika fainali hizo ambazo zilitumbuizwa na wanamuziki nguli wa THT Lina Sanga na Ditto.
Katika shindano hilo ambalo lilihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mara na maeneo ya jirani,mshindi alizawadiwa sh.1,000,000/=,wa pili Sh 800,000/= na wa tatu sh 500,000/= huku walio bali wakipewa kila mmoja sh 100,000/=
Categories:
gaudensia joseph,
Miss utalii mara