![]() |
Linda msanii wa filamu Mbeya film Production. |
MSANII anayekuja juu katika tasnia ya filamu Sofia David ‘Linda’ ameelezea kuwa anaamini kuwa ujio wa filamu ya God is Great utaonyesha kipaji chake, katika filamu hiyo msanii huyu anasema kuwa amefanikiwa kuigiza filamu hiyo katika kiwango cha juu kuliko filamu alizowahi kuigiza.
Msanii huyu anayepatikana katika kundi la Mbeya filamu amekuwa akifanya vizuri katika filamu anazobahatika kuigiza, alianza kuigiza katika filamu ya Linda na kujizolea umaarufu ambao uliazaa jina hilo la Linda na kuwa jina lake hadi leo hii.
“Sisi Mbeya film kwa sasa tumepania kuonyesha uwezo wetu katika kuigiza filamu kwa kiwango cha juu sana, na kuleta upinzani kwa wasanii waliopo juu hasa Dar es Salaam, mara nyingi baadhi ya watu wanaamini kuwa wasanii wazuri wanatokea huko, lakini ukweli ni kwamba hata sisi tunaweza, Filamu ya God is Great itaonyesha kipaji changu,” anasema Linda.
Filamu ya God is Great inatarajia kuingia sokoni hivi karibuni, baada ya kutengenezwa na kampuni ya Mbeya film Production kutoka Jijini Mbeya, katika filamu hiyo kuna wasanii nyota kama vile Jacqueline Wolper, Elia Daniel ‘Elly G’ Daniel Kamwela na wasanii wengine.
Categories: