Philemon Luhanjo (picha kutoka maktba)
Boniface Meena
BAADA ya kuongezewa mkataba kwa vipindi takriban viwili, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo sasa anatarajiwa kustaafu wadhifa wake huo, ifikapo mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.Taarifa za kukaribia kustaafu kwa Luhanjo zimekuja wakati Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma, akichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge kufuati tuhuma kwamba aliingilia Haki na Mamlala ya Bunge.
Uchunguzi huo unafuatia hatua yake ya kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (alisyesimamishwa), David Jairo anayetuhumiwa kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka katika mashirika yaliyo chini ya wizara yake kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bungeni bajeti ya wizara yake, kinyume cha sheria.
Kamati hiyo inachunguza iwapo hatua ya Luhanjo kutoa “uamuzi wa mwisho” kwa jambo ambalo lilianzia bungeni bila kuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serika bungeni, inaingilia uhuru, haki na madaraka ya bunge.
Kadhalika, Luhanjo katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, alituhumiwa na wabunge kwamba ni chanzo cha uozo na ufisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, tuhuma ambazo hata hivyo, alizikanusha kwamba zilikuwa na lengo la kuchafua rekodi yake ya utumishi mwema serikalini.
Katibu Mkuu Kiongozi aliyeingia Ikulu siku chache baada ya kuapishwa kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete Desemba 2005, alipaswa kustaafu tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini aliongezewa mkataba mwingine.
Sasa imetangazwa rasmi kwamba anastaafu rasmi Desemba 9, mwaka huu, siku ambayo pia ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kauli iliyotolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia.
Ghasia alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jana katika mkutano wake kuhusu kongamano la kumbukumbu ya miaka 12 tangu kifo cha Baba wa Taifa, alikiri kwamba Luhanjo “aliongezewa mkataba wa kazi”.
Ghasi alisema hivi sasa Luhanjo anafanya kazi kwa mkataba, lakini baada ya maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Uhuru, mkataba wake utakwisha na ataachia nafasi hiyo.
“Ule ni uteuzi wa Rais, lakini naweza kujibu kuwa sasa hivi yuko kwenye mkataba na ukiisha atastaafu,”alisema Ghasia.
Ghasia alifafanua kwamba, kufanya kazi kwa mkataba ni utaratibu ambao serikali imejiwekea pale ambapo kuna mahitaji ya watu, hivyo kuruhusu wastaafu kuendelea kufanya kazi.
Wengine wenye mikataba
Mbali na Luhanjo, taarifa zinaonyesha baadhi ya makatibu wakuu wa wizara wamekuwa wakiongezewa mikataba yao ya kazi bila kutolewa kwa maelezo kwa umma.
Miongoni mwao ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbet Mrango na yule wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohamed Muya ambao wameongezewa muda wa kushika nyadhifa zao baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria.
Mrango alipaswa kustaafu mwezi Agosti mwaka huu, lakini aliongezewa mwaka mwingine mmoja, wakati Muya naye ameongezewa muda baada ya umri wake wa kustaafu kisheria.
Uamuzi huo wa kuongezea mikataba makatibu wakuu hao wanaopaswa kustaafu, umekuwa ukiibua manung’uniko kama ilivyotokea kwa baadhi ya watumishi wa wizara ya ujenzi baada ya Mrango kuongezewa muda.
Hata hivyo, Ghasia alitetea hatua hiyo ya Serikali akisema; “Kwa mfano kama ualimu, madaktari kunakuwa na mahitaji hivyo tunawapa mikataba ya kazi na hata ukienda chuo kikuu utakuta kuna wahadhiri wana miaka hadi 70, lakini wanafundisha,”alisema.
Malipo ya watumishi wa Serikali
Kuhusu malipo ya watumishi hewa serikalini, Ghasia alisema wanaendelea kuhakiki watumishi hao kwa kutumia mfumo mpya wizara iliyouanzisha.Alisema suala hilo linashughulikiwa na Takukuru na tayari uchunguzi wa awali umeshakamilika.
Kongamano la Mwalimu Nyerere
Akizungumzia kongamano la kumbukumbu ya miaka 12 tangu kifo cha Mwalimu, alisema madhumuni yake ni kuelimisha na kuikumbusha jamii juu ya mambo muhimu ambayo Nyerere aliyaamini na kuyafanya.
Waziri Ghasia alisema katika kongamano hilo, mada nne zitawasilishwa ambapo tatu kati ya mada hizo zitatolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Kigoda cha taaluma cha Mwalimu Nyerere na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.“Mada hizo zitahusu nafasi na majukumu ya taasisi hizo katika kumuenzi baba wa Taifa,”alisema.
Ghasia alisema mada ya nne ambayo ndiyo kuu itatolewa na mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Palamagamba Kabudi na itahusu miaka 50 ya uhuru, misingi mikuu ya mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika kujenga Taifa hili.
Alisema Rais Mstaafu Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ndiye atakuwa mwenyekiti wa kongamano hilo na litahudhuriwa na viongozi wastaafu mashuhuri waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere, ikiwa ni pamoja na Dk Salim Ahmed Salim, Kingunge Ngombale Mwiru, Joseph Warioba, Jaji Mstaafu Barnabas Samatta na Spika mstaafu, Pius Msekwa.
“Kongamano litafanyika tarehe 15 mwezi huu Ubungo Plaza kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10 jioni,”alisema Ghasia.

Categories: