Afisa utumishi wilaya ya Luddewa Bw. Juma Ally
BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe (Iringa) limemsimamisha kazi kuanzia jana afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Juma Ally kutokana na sababu mbali mbali
Uamuzi wa kumsimamisha kazi afisa utumishi huyo ulitolewa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo wakati kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa mbali mbali za robo mwaka tangu madiwani hao walipoingia madarakani mwaka 2010,kilichohudhuriwa na mbunge Filikunjombe.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, amewaonya watumishi wengine wa Halmashauri hiyo ya Ludewa kuacha tabia hiyo mara moja akisema kuwa, “Ludewa sio shamba la bibi” na kuwa wakati umefika kwa watumishi wasiowajibika kuvuliwa magamba kwamba hatapenda kuona wilaya ya Ludewa inakwamishwa kusonga mbele kimaendeleo na watumishi hao.
Kabla ya kusimamishwa kwa afisa utumishi huyo madiwani wote zaidi ya 33 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na diwani mmoja wa Chama cha TLP walipiga kura ya ndio ya kugoma kuendelea na ajenda mpya za kikao wakati zile maagizo na mipango mbali mbali iliyopangwa kufanyika kusimama utekelezaji wake kutokana na ufanisi duni wa wakuu wa idara katika Halmashauri hiyo
Categories: