MAHAKAMA KUU YAFANYA USULUHISHI KATIKA KESI YA GAZETI LA RAI DHIDI YA WAZIRI WA ZAMANI WA UTAWALA BORA WILLSON MASILINGI




Mahakama kuu imefanya usuluhishi katika kesi ambayo gazeti la Rai lilishitakiwa na Waziri wa Zamani wa Utawala Bora Willson Masilingi kwa kumkashifu.

Rai wamekubali kumlipa fidia ya Sh milioni 15 sambamba na hilo Kampuni ya New Habari (2006) inayomiliki gazeti hilo imekubali kuchapisha habari ya kumuomba msamaha Masiringi baada ya kukiri kumchafua.

Habari za kuomba radhi zitachapishwa katika ukurasa wa kwanza na wa pili utekelezaji wake ni ndani ya siku kumi na nne kuanzia leo.

Mbele ya Jaji wa mahakama hiyo, Zainab Mruke kabla ya kuanza kusikiliza kesi hiyo Octoba 24 mwaka huu, wakili wa wadaiwa, Imanuel Makene aliomba kufanya maongezi ya kulipa ili mdai asiendelee na shauri dhidi yake.

Hata hivyo mdaiwa wa tatu Prince Bagenda alidai hayuko tayari kwa siku hiyo kwasababu wakili wake alijitoa na kwamba anahitaji muda apate wakili mwingine anaefaa ili amshauri.

kikao cha Masilingi na Rai nje ya Mahakama kilileta muafaka na kurudi mahakamani kupata baraka mbele ya Jaji Mruke na kupanga namna ya malipo, Rai walikubali kulipa Sh milioni 10 na Bagenda alikubali kulipa Sh milioni tano fedha ambayo Masilingi alisema kuwa hailingani na gharama zake toka mwaka 2005 kesi hiyo alipofungua ikiwa ni pamoja na kulipa mawakili aliowatoa katika makampuni matatu makuu ya uwakili na kusafirisha mashahidi.

Wakili Makene alikiri maridhiano nje ya mahakama ni bora kwasababu yanaokoa muda na uadui kati ya mdai na mdaiwa. Masilingi alisema amewasamehe Rai na Bagenda hataki kuwa na maadui.

Rai katika toleo lake la Juni 2 hadi 8, 2005 liliandika katika ukurasa wa mbele habari iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Waziri Achangisha wapiga kura na kujenga ghorofa. Katika habari hiyo ilimtuhumu Masilingi kwa matumizi mabaya ya madaraka, kutumia fedha za michango ya wananchi na misaada ya maendeleo.

Habari hiyo ilidai kuwa mwaka 1998 aliwachangisha wananchi wa Wilaya ya Muleba Sh milioni 12.3 kwa madai ya kujenga hospitali ya Mhalala lakini baadaye akazitumia kwa kujenga nyumba yake ya ghorofa. 

Alituhumiwa pia kuomba Sh milioni 45 kutoka mashirika ya Japan kwa ajii ya ujenzi wa Zahanati ya Shamba ambazo alizitumia kujenga nyumba yake hiyo, na kwamba aliingilia miradi ya maendeleo ya wananchi inayosimamiwa na Tasaf na kuvunja kamati hizo.

Pia anadaiwa kutumia madaraka yake ya uwaziri kuilazimisha Halmashauri ya Muleba kuipatia zabuni ujenzi wa barabara kampuni ya Kichina bila kufuata tataribu.Bagenda alimtuhumu Masilingi katika makala yake kumfanyia hujuma kwa Rais Jakaya Kikwete wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.

Categories: ,