Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange akipokea Kikombe cha ushindi pamoja na Ngao kutoka kwa Meja Jenerali Nicholas Miti ambaye aliongoza msafara wa Jeshi la Tanzania nchini Msumbiji katika kusheherekea miaka 25 ya kuwa kumbuka mashujaa walio pigania uhuru wa Msumbiji. Sherehe hizo ziliambatana na michezo na timu ya miguu ya JWTZ ilishinda na kuzawadiwa kikombe. Kulia ni Mnadhimu wa Michezo Jeshini Luteni Kanali Richard Mwandika. Hafla fupi ya kukabidhi kikombe na ngao ilifanyika Makao Makuu ya Jeshi Dar es salaam. (Picha na Chris Mfinanga) |