SERIKALI mkoani Mwanza imeowaonya wachimbaji wadogo wilayani kuacha mara moja vurugu wanazoendelea kuzifanya, ikiwa ni pamoja na kuharibu mali na kujeruhi watu, huku ikiahidi kwamba kuanzia sasa itawachukulia hatua kali wachimbaji ama watu watakaobainika kuchochea vurugu katika machimbo hayo. Onyo hilo lilitolewa jana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo wakati akizungumza na kundi la wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyaruyeye katika Kata ya Nyarugusu, baada ya wachimbaji hao kufanya vurugu jana ikiwa ni pamoja na kuvamia kituo kidogo cha Polisi cha Nyarugusu.
Akizungumza na wachimbaji hao katika eneo la machimbo hayo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kuwa na subira wakati bado taratibu za kisheria kwa ajili ya wao kuruhusiwa kuchimba katika eneo hilo zikikamilishwa na kwamba kufanya fujo wakati huu kunaweza kuisababisha serikali kusitisha ukamilishaji wa taratibu hizo.
Kutokana na vurugu za wachimbaji hao mmoja wao anadaiwa kuuawa jana na mwingine amejeruhiwa kwa kupigwa risasi wilayani hapa, baada ya kundi la wachimbaji wadogo zaidi ya 5,000 kuvamia kituo cha polisi kwa lengo la kuwateka askari polisi ili kuvamia eneo la machimbo ya dhahabu ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu na risasi.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kijiji na Kata ya Nyarugusu Tarafa ya Busanda wilayani Geita, baada ya kundi hilo la wachimbaji wadogo kuvamia mgodi huo usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kuchimba dhahabu lakini baadaye walishindwa nguvu na askari wanaolinda eneo hilo na kuwaondoa.
Wachimbaji hao waliondolewa katika machimbo ya dhahabu ya Nyaruyeye wiki tatu ilizopita baada ya kuvamia eneo hilo na kuanza kuchimba dhahabu, ambapo wamiliki wa machimbo hayo waliahidi kukamilisha taratibu za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuomba kibali kutoka kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa vile eneo hilo ni la hifadhi ya misitu.
Amri ya kuondolewa kwa wachimbaji hao ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Philemon Shelutete baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kuamuru waondolewe kwenye eneo hilo kwa usalama wao kutoka na wingi waliokuwa nao hali iliyokuwa ikitishia usalama wao, huku mmoja wa wabia katika machimbo hayo, Baraka Nyandu akiahidi kukamilisha masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria ili waruhusiwe kuendelea kuchimba katika eneo hilo kwa utaratibu mzuri.
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida juzi kundi kubwa la wachimbaji liliibuka na kufanya maandamano makubwa hadi nyumbani kwa Baba yake na Mbia huyo (Baraka) ambapo walifanya mashambulizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubomoa nyumba, lakini kabla hawajasababisha majeruhi kwenye familia hiyo polisi waliwasili na kuwatawanya kwa risasi za moto na mabomu.
Habari kutoka katika eneo la tukio zinaeleza kuwa baada ya wachimbaji hao kuondolewa na polisi katika nyumba hiyo walikimbia na kuelekea kusikojulikana, huku askari wakiamini kwamba wametoweka kabisa ghafla saa 10 jioni kundi hilo liliibuka tena na kuvamia kituo cha polisi cha Nyarugusu kwa madai kuwa askari wa kituo hicho pamoja na wengine waliotoka wilayani ndio wanaowazuia kuchimba kwenye eneo hilo.
Wakiwa katika eneo la kituo hicho cha polisi wachimbaji hao walianza kurusha mawe kwa lengo la kubomoa kituo hicho cha polisi, ambapo katika purukushani hizo askari wanne akiwemo Mkuu wa kituo hicho aliyetambuliwa kwa jina moja la Ibra walijeruhiwa vibaya kwa kupigwa mawe sehemu mbalimbali za mwili wao.
Habari zinadai kuwa kutokana na hali hiyo iliwalazimu polisi kujihami kwa kurusha risasi za moto baada ya mabomu ya machozi kuonekana kushindwa kuwadhibiti wachimbaji hao, ambapo katika hali hiyo mtu mmoja ambaye jina lake bado halijatambuliwa alikufa baada ya kupigwa risasi kifuani huku mwingine akiwa amejeruhiwa.

Categories: