Vijana wa Chama cha mapinduzi (UV CCM) wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa Leo wameungana na watanzania katika kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere ambaye ametimiza miaka 12 tok a alipotutoka duniani.
Vijana hao wametembea umbali wa zaidi ya kilometa 35 kutoka Kidamali jimbo la Kalenga hadi KIsing,a jimbo la Isimani na kupokelewa na mgeni rasimi kamanda wa UV CCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri (pichani kulia) ambaye amewataka vijana kuepuka kulia ugumu wa maisha kwa kushinda vijiweni na badala yake amewataka kufanya kazi .
Alisema kuwa pamoja na mafanikio makubwa ambayo serikali ya awamu ya nne imeonyesha kwa kuboresha maisha bora na kuongeza ajira kwa vijana ila bado vijana walio wengi wanashindwa kuchangamkia nafasi mbali mbali za ajira na kuendeelea kushinda vijiweni na kulia maisha magumu.
Hivyo alisema wakati umefika kwa vijana kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili kuweza kujitafutia maisha bora badala ya kutegemea kushushiwa neema ya maisha bora.
katika hatua nyingine kamanda huyo wa vijana amewataka vijana wa UVCCM kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli kwa vijana wengine ikiwa ni pamoja na kujkiepusha na matumizi pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya .
Kwani alisema kuwa jitihada zinazofanywa na serikali katika kupiga vita matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya ni vizuri kuungwa mkono na makundi yote ya kijamii huku akisisitiza kuwa vijana ni moja kati ya makundi ambayo yanaathirika zaidi na matumizi ya dawa za kulevya .
Akielezea kuhusu siku hiyo ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa alisema kuwa mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mchapa kazi na kiongozi wa mfano barani Afrika na dunia kwa ujumla kutokana na utendaji kazi wake.
Hivyo alisema njia pekee ya kuendelea kumuenzi baba wa Taifa ni watanzania kufanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwa na uzalendo na Taifa pamoja na kupiga vita maadui watatu kwa maana ya malazi ,ujinga na umasikini kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alivyojitolea kupambana na maadui hao.
Categories:
BENO MALISA,
ccm,
uvccm