Na Mwandishi Wetu
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Arusha, Hadija Bambo ametekwa na watu wasiojulikana (maharamia).
Tukio hilo lilitokea Jumatatu, Oktoba 10, 2011, saa 4 asubuhi.
Kwa mujibu wa shemeji wa mwanafunzi huyo, William Joseph, baada ya Hadija kutoonekana kwa muda, mama yake, Asia Gema alijaribu kupiga namba ya simu yake lakini ikapokelewa na mwanaume aliyetoa vitisho.
“Yule mtu aliyepokea simu ya Hadija, alimtahadharisha mama (Asia) asitoe taarifa polisi mpaka watakapoamua kumrudisha,” alisema William.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa Kituo cha Polisi Baraa, Arusha kwa namba BAR/RB/1359/2011 na kwamba polisi wanaendelea na upelelezi.
Mwenye taarifa anaweza kuripoti polisi au kupiga simu namba 0754 277521 na 0715 627585.
Categories:
arusha,
denti,
hadija bambo