WAZIRI wa Miundo Mbinu na Mawasiliano katika SMZ Hamadi Massoud Hammad
Talib Ussi,Zanzibar
WAZIRI wa Miundo Mbinu na Mawasiliano Hamadi Massoud Hammad ametakiwa kujiuzulu kwa hiari baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake na kusababisha meli ya Mv Spice Islander kuzama.
Hammad anatakiwa ajiuzulu kutokana uzembe na uliosababisha vifo vya watu zaidi ya 200 baada ya meli hiyo kupinduka na kuzama kwenye mkondo wa Nungwi wakati ikielekea Pemba kutoka Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wakilishi la kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa kuhusu tukio la kuzama kwa meli hiyo Hamza Hassan Juma alisema wahusika walishindwa kusimamia idadi ya abiria waliokuwa wakiingia katika meli hiyo.
Alisema meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua abiria 610, lakini chombo hicho kilipakia watu zaidi ya abiria 2,764. Abiria hao ni mara tano zaidi ya uwezo wa meli hiyo.
Alisema waziri husika amekuwa akitoa majibu ya kubahatisha na kuzarau taarifa mbalimbali zinatolewa na wananchi.
Juma alisema waziri huyo alilidanganya baraza hilo na alimnukuu, 'Wizara kupitia mamlaka ya usafiri Baharini, kabla ya vyombo kuondoka inachukua hatua zinazofaa na tutaendelea kuchukua hatua zote za kiusalama kwa vyombo vyote vinavyo fanya safari majini, kwa kuvikagua'.
Alisema kutokana na mamlaka aliyonayo Waziri huyo alikuwa na uwezo waa kuunda tume kabla ya Rais, lakini hakufanya hivyo mpaka Rais alipounda chombo hicho.
“Kwa maana hiyo tuna mtaka Waziri ajiuzulu kwa hiyari yake ili kuonyesha uwajibikaji na asisubuiri kuwajibishwa na Rais kwa uzembe,” alisema Hamza.
Alitoa mfano kwa Serikali ya Brazili kwamba kuazia Januari, mwaka huu, mawaziri wanne wamejuzulu kutokana na makosa mbalimbali na kwamba Rais mstafu wa Zanzbar Ali Hassan Mwinyi pia aliwahi kujiuzulu kutokana na vifo vya wafungwa wakati alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
Alisema kamati ya imegundua kwamba kapteni wa meli hiyo alifanya uzembe baada ya kutotoa taarifa mapema wakati meli hiyo ilipokuwa ikianza kuingia maji.
“Kapteni angelitoa taarifa mapema, abiria wengi wangeokolewa wakiwa hai,” alisema Hamza.
Kuhusu wazamiaji kutoka Afrika ya Kusini, alisema kamati yake haikuridhishwa na taarifa iliyo tolewa na Serikali kuhusu kushindwa kwa wazamiaji wa hao kwa kuwa meli hiyo ilizama kwenye kina kirefu.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alitoa taarifa rasmi ya Serikali katika ukumbi wa Baraza la Wakilishi ambayo iliweka wazi kwamba meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 610.
Lakini meli hiyo ilichukua abiria wengi kinyume na idadi yake.
CHANZO: MWANANCHI

Categories: