MAZUNGUMZO KATI YA WAZIRI WA MAMBO YA AFRIKA WA UINGEREZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA





Waziri wa Masuala ya Africa wa Uingereza Bw Henry Belingham amewaambia Watanzania kuwa nchi yake haina fikra za kuacha kuisadia Tanzania.

Bw Bellingham walikuwa akiongea hayo kutokana na ripoti kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa na mpango wa kusitisha misaada kwa nchi zote ambazo hazifuati haki za  binadamu ikiwemo haki ya ushoga.

Akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Jijini Dar es salaam Jana, Bw Bellingham alisema kuwa Uingereza itaendelea kuheshimu milala, jadi na mapenzi ya Watanzania.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Africa zinazo jali haki za binadamu na utawala bora na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayo faidi sana misaada kutoka selikali Uingereza.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa limshukuru Waziri huyo kutembelea Tanzania, na kwa kuihakikishia Tanzania kuwa swala ushoga.

Katika mazungumzo yao waliongelea pia kuhusu swala linalo tia shaka la maharamia na ukuaji wa siasa katika Afrika ya Kaskazini.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri Belingham Alielekea Zambia.