Askofu akitoka (mwenye koti la Bluu) kituoni kuripoti kuwa amezuiwa kuingia katika kanisa
Askofu akiwa amepozi mara baada ya kuzuiwa kuingia kanisani
Waandishi wa habari ambao alikuja nao pia walishikwa na mshangao mara baada ya kukuta hali ni tofauti na alivyowaeleza.
Waumini wakimaliza ibada yao kwa amani pasipo uwepo wa askofu
Picha na Habari Kutoka Kwa Mdau Godfrey Isinika
Kabla ya askofu kuzuiwa hii leo asiingie kanisani hivi karibuni waumini hao wa kanisa la Kilimatinde walibandika mabango kanisani ya kumkataa mchungaji wa mtaa na askofu huku wakiandika hoja kadhaa za kuukataa uongozi huo, baadhi ya hoja ni kama
1. Fedha za mnara watigo ambao upo eneo la kanisa hilo
2. Gari la wagonjwa mil5 za matengenezo zimetumika kinyume namatalijio mpaka sas gali haljatengemaa
3. Kesi nyingizenye hasara kwa DRV
4. kufukuza wafanyakaz kwa maslahi yake binafsi
5. kumng'ang'ania mkuu wa chuo cha uuguz kwa maslahi yake bnafsi,wanafnzi hutoa fedha zaukarabat sh elfu 50 lakini haieleweki pesa hizo zinakwenda wapi pia Wakristo wa DRV wamechangia tsh lak 2 kila parish kwa ajili ya ukarabat wa chuo cha nursing lakini kazi ya fedha hiyo haionekani,
6. Kupuuza malalamiko ya Wakristo.
Barua hiyo aliandikiwa Askof mkuu,katibu mkuu na msajili wa jimbo. Nakala Askofu wa Dayosisi ya Rift Valley John Lupaa,mchungaji wa mtaa Samuel Chilewa ,OCD W Manyoni na OCS Kilimatinde)
Hata hivyo katika hali ya kushangaza waumini wawili walitengwa na mchungaji wa kanisa hilo kutokana na wao wanachokieleza kuwa ni kwenda kuhoji kuhusu fedha za mnara. Katika hali ya kushangaza mara baada ya kutaka kumrudisha muumini mmojawapo kanisani, ni pale walipomwita na kufanya makubaliano ya maneno ya kutamka wakati wanamrudisha kundini hivyo aliombwa kukubali kile wanachomuelekeza ili akatamke mbele ya kanisa lakini tofauti na alivyoelekezwa akajikuta anazungumza mbele ya watu tofauti na walivyokubaliana kabla ya siku ya ibada.
Kabla ya kuibuka kwa mgogoro huo pia kanisa la Kintinku ambalo liko chini ya dayosisi ya rift valley ambayo inaongozwa na askofu huyo pia liliibuka na mjadala wa kumkataa askofu huyo
Hivi leo waumini wa kanisa hilo la Kilimatinde wamemzuia Askofu JOHN DAUDI LUPAA kuingia katika kanisa hilo kwa madai kuwa hawamtaki. Hivi juzi pia waliandika barua kwa askofu Mkuu kuwa waumini hao WAMEJITOA katika utawala wa askofu huyo hivyo kila mali ya kanisa itakuwa chini yao mpaka pale atakapo jiuzulu.
Categories: