Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni mbili kwa Shule ya Sekondari Masaki wilayani
Kisarawe mkoani Pwani, kama sehemu ya uwajibikaji kwa kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi, Multichoice Tanzania inaamini umuhimu wa kuwekeza katika elimu kupitia mpango wao wa ubunifu ujulikanao kama kituo cha habari na mawasiliano.
Alisema mpango huo unatekelezwa katika shule 41 katika Tanzania na kwamba
msaada huo ni sehemu ya uwekezaji katika elimu kuhakikisha vizazi vya sasa baadaye vinapata elimu bora na kwamba Kampuni hiyo imeahidi kufungua kituo cha habari na mawasiliano katika shule moja wilayani humo iwapo umeme utapatikana.
Alisema vituo hivyo vitasaidia kutoa habari kwa watoto, kupanua akili zao, maarifa pamoja na kuwapa ufahamu kuhusu masuala mbalimbali yanayowazunguka duniani ikiwemo uchumi.
Alisema wanalenga pia kuhakikisha nchi zinazoendelea kama Tanzania zinaikuka kielimu na kwamba kampuni hiyo imeanzisha vituo zaidi ya 1,000 vya Rasilimali katika nchi 27 barani Afrika.
Alisema kuanzishwa kwa vituo hivyo na nyenzo za kazi ni kutokana na kushirikiana na serikali ili kusaidia kuboresha ubora wa rasilimali za elimu kwa kutumia teknolojia na njia tajiri elimu kutoka DStv.
Categories: