WANAHARAKATI WAFANYA MAANDAMANO DAR, KUSHINIKIZA SERIKALI IZUNGUMZE NA MADAKTARI NA KUMALIZA MGOGORO
Wanaharakati wakiwa na mabango yao leo kwenye maandano eneo la salender brige jijini Dar es Salaam
Mama Kijo Bisimba-Mkurugenzi wa LHRC akiongea na Waandishi wa Habari kwenye Maandamano hayo
Mama Kijo Bisimba-LHRC Mkurugenzi nae akiwa kwenye maadamano hayo ya wanaharakati muda mfupi uliopita jijini Dar es Salaam
Viongozi wa Jeshi la Polisi wakihakikisha hali ya usalama inakuwepo
Jeshi la Polisi likitoa maelekezo ya kutawanya maaandamano hayo ya wanaharakati yaliyofika katika ya jiji la Dar es Salaam Kufwatia Mgomo wa Madaktari unaoendelea Nchini wameandamana na wamekusanyika hapo salender bridge...Kituo Cha Legal and Human Rights Centre, wakishirikiana na asasi nyingine nyingi za kiraia, waliandaa maandamano ya amani Leo saa tisa mchana leo mabapo walianzia Salendar Bridge Wakiwa na mabango kibao wakiishinikiza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Mganga Mkuu Wizara ya Afya wafutwe kazi mara moja; madaktari warudi kazini mara moja; serikali na madaktari wakae meza moja na kujadili masuala muhimu ya afya, na wafikie makubaliano ndani ya miezi mitatu.Picha na Habari na Mdau Fakhi Karume
Categories: