Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

PICHA KUTOKA KATIKA AJALI YA UBUNGO JANA




[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

AJALI MBAYA YA MAROLI YAUWA WAWILI BABATI


Fuso ilivyoteketea kabisa na moto.


Watu zaidi ya wawili wanahofiwa kufa katika ajali ya gari iliyotokea usiku majira ya saa 6 katika eneo la kijiji cha Mdori Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo watu wawili walionekana miili yao ikiwa imeungua na moto. Ajali hiyo ililihusisha roli la mizigo lililokuwa limetokea Arusha na Fuso lililokuwa limetokea Singida.Walioteketea kwa moto inadhaniwa kuwa ni dereva na tandiboy wa Fuso ambao walibanwa katika gari hilo baada ya kukatika cabin.


Mafuta ya kupikia ya alizeti yalitapakaa katika eneo hilo.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

AJALI YA ROLI LA MIZIGO MLIMA KITONGA

 Gari lenye no za usajili T 665 AMV,Limepata ajali eneo la mlima kitonga Iringa,na dereva wa gari hilo bw bonventura simo anayeishi mwananyamala amepata majeraha makali na maumivu ya ndani kwa ndani ambapo kwa sasa yupo hospitali ya ilula Lutheran.ambapo pia kondakta wa gari hiloalikimbia baada ya kiwewe na ajali hiyo Picha na  fununu.blogsport.com.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

AJALI MBAYA YADAIWA KUUA MMOJA IRINGA



Wasamaria wema wakisaidia kumtoa dereva wa daladala baada ya ajali


Lori lililosababisha ajali eneo la Mwangata mjini Iringa mchana huu


Na francis Godwin
Dadaldala lagongana na lori katika eneo la kona za Mwangata katika manispaa ya Iringa majira ya 8 mchana na kuna taarifa kuwa mtu mmoja kufariki dunia katika ajali hiyo mbaya.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wameuambia mtandao huu kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Lori lenye namba za usajili T164 BDB kupita upande ambao si wake hivyo kulazimika kulivaa daladala hilo ambalo lilikuwa likishuka mteremko wa Mwangata na lori hilo likipanda mlima.
Walisema kuwa kutokana na kona hizo abiria waliokuwa katika daladala walijikuta wakikutana uso kwa uso na lori hilo.
Hata hivyo walisema zaidi ya abiria watano ndio walijeruhiwa vibaya akiwemo dereva wa daladala yenye namba T 229 BGP anayefahamika kwa jina la kazi la Kizibo.
Majeruhi wote wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi huku dereva wa lori hilo amekimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo japo taarifa zaidi juu ya tukio hilo ameahidi kuzitoa hivi punde.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MAZISHI YA MABAKI YA MIILI YA ABIRIA WA DELUX



Shughuli ya ya kuzika mabaki ya miili ya abiria waliopata ajali walipokuwa wakisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma juzi. Ajali hiyo ilitokea Kibaha, mkoa wa Pwani, baada ya gurudumu la mbele la basi la Delux kupasuka na kusababisha kudondoka na kuwaka moto na kuteketea kabisa pamoja na abiria 12 hapo hapo. Mazishi hayo ya pamoja yamefanyika katika makaburi ya eneo liitwalo Air Msaehapo Kibaha ambako mwaka 1999 ajali ingine ilitokea sehemu hiyo hiyo. Marehemu imebidi wazikwe pamoja baada ya miili yao kuungua vibaya sana kiashi cha kushindwa kutambulika.

Picha na Chris Mfinanga
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Waliokufa ajali ya basi kuzikwa kaburi moja






MIILI ya watu 12 walioteketea kwa moto katika ajali ya basi la Deluxe Coach iliyotokea Misugusugu mkoani Pwani juzi, watazikwa leo na Serikali kwa heshima zote katika kaburi moja katika eneo la Air Msae mjini Kibaha.

Eneo hilo ndipo walipozikwa watu waliopata ajali ya basi la Air Msae lililokuwa likitokea Arusha kuja Dar es Salaam miaka ya 1990.

Uamuzi huo umefikiwa jana katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mwantumu Mahiza kutokana na miili hiyo kuharibika vibaya na kushindwa kutambulika.

Akizungumzia mazishi hayo jana, Mahiza alisema kabla ya maziko, miili ya watu hao itachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili vifanikishe utambuzi wao.

Taarifa kutoka Hosptali Teule ya Tumbi, zilieleza kuwa hata wananchi waliokwenda kujaribu kutambua ndugu zao, walishindwa kufanya hivyo kutokana na kuharibika kwa miili hiyo ambayo baadhi imekuwa majivu.

Kutokana na hali hiyo, Mahiza aliwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha kuwatambua ndugu zao, kwa kupeleka vitu kama nguo ambazo ndugu zao walizitumia siku chache kabla ya ajali hiyo.

"Tunaomba wananchi walioondokewa na ndugu zao katika ajali hii watoe ushirikino kwa kuleta vitu kama soksi, shati, khanga au viatu alivyokuwa anatumia ndugu yao hivi karibuni ambavyo havijafuliwa ili visaidie kutambuliwa baada ya kupimwa kwa njia ya vinasaba,” alisema Mahiza.

Ofisa Habari wa Hosptali Teule ya Tumbi, Rose Mtei alisema kuwa majeruhi waliofikishwa katika hospitali hiyo ni 36 ambapo 35 waliruhusiwa na mmoja aliyelazwa anaendelea vizuri.

"Kutokana na ajali hiyo ndugu wamefika kujaribu kutambua miili hiyo lakini haikuwezekana kutokana na kuharibika vibaya na wengi wamekuwa majivu, kwa sasa tunasubiri tamko la uongozi wa Mkoa ili kujua mazishi yatakuwa wapi,” alisema Mtei kabla ya tamko la Mahiza.

Kati ya miili hiyo 12, ni miili mitano tu ambayo inaonekana kama miili ya watu lakini haitambuliki ya nani na miili mingine imekuwa majivu kabisa.

Mtei aliwataja baadhi ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali hiyo ni Julias Lesiwa, Mary Mbunga, Earnest Kato, Charles Nyaongo, Shukuru Jarious, Daniel Michael, Nestory Mfuse, Benedictory Labure na Jumanne Mjif.

Wengine ni Omary Omary, Fred Sarom, Paschal Amos, Neema Mgomba, Augustine Matei, Omary Jahu, Maburuk Mohamed Cecilia Ngirao, Alfred Semwari, Isack Manyota, Kelvin Ndugu, Jamira Sefu, Veronica Hippill, Tobias Legume, Mashaka Muganyizi, Paschal Lungwa na Amina Michael.

Ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo namba T 334 AAD aina ya Volvo lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, kupasuka tairi la mbele kulia na kupinduka na kushika moto.

Akizungumzia ajali hiyo jana Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema tayari Jeshi la Polisi limepeleka wataalamu wake wa vinasaba kuchunguza majivu na mabaki ya watu waliokufa katika ajali hiyo.

“Kuna wataalamu wetu wamekwenda Kibaha kuchukua majivu ili kupima vinasaba na kubaini ni watu wangapi waliopoteza maisha katika tukio hilo,” alisema.

Alisema mpaka sasa mbali miili hiyo kushindwa kutambuliwa, watu wanane bado hawajatambuliwa wala haijulikani waliko.

Kamanda Mpinga alisema basi hilo liliondoka Dar es Salaam likiwa na abiria 49 na kuwataka madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, ili kuepusha matukio ya ajali.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani salamu za rambirambi na masikitiko makubwa kwa ajali hiyo.

“Hii ni ajali mbaya sana, ni ajali ya kusikitisha sana na ya kuhuzunisha kwa wananchi wote na hasa mimi,” Rais alisema na kusisitiza kuwa ajali kama hizi zinazidi kutoa changamoto kwa Polisi na vyombo vya usalama barabarani.

“Huu ni mtihani zaidi kwa Polisi na vyombo vya usalama barabarani, tunahimiza sheria za barabarani zifuatwe na kuzingatiwa, na hili ni pamoja na usalama wa vyombo hivyo na abiria wao, hii ni changamoto kubwa kwa Polisi katika kulisimamia hili na kuona linatekelezwa,” alisema katika taarifa iliyiotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ikulu.

Rais aliwataka polisi wa usalama barabarani kutokuwa waangalifu tu pale ajali inapotokea na kulegeza kamba baada ya tukio kwisha.

“Hili ni eneo ambalo litazidi kuwa tatizo siku hadi siku, kama hamtakuwa makini na kuonesha ushupavu kwa wanaovunja sheria na kutozingatia mahitaji ya chombo salama cha usafiri wa binadamu na mali zao wakati wote,” alisisitiza.

“Nawapa pole wafiwa wote, nawatakia waliojeruhiwa kupata ahueni haraka iwezekanavyo na kurudi katika shughuli zao za kila siku,” alisema.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

HABARI MPYA: Ajali Nyingine Yatokea Mbeya LEO







Maiti ikinasuliwa kutoka kwenye moja ya magari yaliyopata ajali katikaeneo la pipeline mkoani Mbeya, ajali hiyo imetokea hivi punde. Tutawaletea taarifa juu ya chanzo na mengineyo kadiri taarifa zitakavyokua zinatufikia.
Habari kwa hisani ya Mjengwa blog
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WATU ZAIDI YA 35 WANUSURIKA KUFA BAADA YA BASI LA DELUX WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA NA KUUNGUA ENEO LA KONGOWE!




Watu
zaidi ya 35 wamejeruhiwa katika ajali yak basi iliyotokea maeneo ya
Kongowe mkoani Pwani. Mashuhuda wamelitaja basi hilo kuwa ni DELUX
coach, ambalo lililokuwa linatoka Dar es salaam, kuelekea mkoani Dodoma,
mchana wa jana , ambapo lilipinduka na kuungua huku ndani likiwa na abiria
na hivyo kuzusha hofu kwa ndugu na jamaa ambao wamesafirisha jamaa zao
katika gari hilo.

Afisa habari hospitali ya
Tumbi mkoani Pwani, Bi rose Mtei anaweka wazi idadi hiyo ya majeruhi
waliopokelewa hospitalini hapo na hali za majeruhi.

Hata hivyo ofisa uhusiano
huyo, alikiri kutopokelewa kwa maiti yoyote katika hospitali hiyo, na
jitihada za kutafuta kamanda wa polisi mkoa ili kuzungumzia hilo
hazikufanikiwa baada yak simu yake kuita bila mafanikio.




[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

BASI LA DELUX COACH LILIVYOTEKETEA KWA MOTO


Watu zaidi ya 20 wanahofiwa kufa baada ya basi la Delux Coach lenye namba za usajili T 334 AAD lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kupasuka tairi la mbele kulia, kupinduka na kushika moto kwa zaidi ya saa tatu likiwa eneo la Misugusugu mkoani Pwani jana. Video hapo juu inaonyesha basi hilo likiteketea kwa moto 

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WATU 30 WAJERUHIWA NA HAKUNA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSUSHA MAGARI MANNE MKOANI MBEYA


Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika ajali mbaya na hakuna aliyefariki iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Baadhi ya majeruhi kati majeruhi 30 wakiwa wameketi chini, wakiwaweshikwa na butwaa kushindwa kuamini kile kilichotokea baada ya kutoka salama katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma. Katika ajali hiyo hakuna aliyefariki lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Mashuhuda waliofika eneo la ajali ambapo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma lakini malori hayo yaliziba barabara na hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.
Moja kati ya malori matatu yaliyosababisha ajali na kuziba barabara na hali iliyopelekea magari mengine kushindwa kupita  katika ajali mbaya, ambayo zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na hakuna aliyefariki katika ajali hiyo iliyotokea kwenye mteremko wa mlima Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini, ambapo ajali hii ilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ikihusisha malori matatu yenye matela na gari ya abiria aina Costa moja maarufu kama Half London au Makete inayofanya ruti ya safari kutoka Mbeya mpaka Tunduma.

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

AJALI MBAYA MKOANI MBEYA


MAJERUHI WA AJALI HIYO MBAYA ILIYOTOKEA MBEYA JANA.

MWILI WA MAREHEMU YUDA AMBOKILE UKIWA UMENASA KWENYE GARI.


Mmoja wa majeruhi


Na Ezekiel Kamanga.

Jinamizi la ajali mbaya limeendelea kuusakama mkoa wa Mbeya ambapo usiku wa kuamkia jana imetokea eneo la Mlima Nyoka Uyole Jijini humo na kuua watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo dogo Yuda Ambokile Jeshi la Polisi limethibitisha.


Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa anesema Marehemu wengine ni Peter Kishimba mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Tazara Iyunga na Joshua Sanga mwenye umri wa miaka 2 mkazi wa Uyole jijini Mbeya na ajali hiyo ilitokea majira ya saa Moja na nusu kwa kuhusisha gari Nne ambazo zote zilijeruhi watu waliokuwemo ndani yake.

Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuharibika kwa gari aina ya Toyota Dyana yenye namba za usajili T 660 AUX ambayo ilikuwa imeegeshwa katika mlima huo.

Walisema kuwa kutokana na kuharibika kwa gari hiyo ndipo gari dogo aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T 425 BAZ , iliyokuwa ikitokea barabara ya Mbarali kwenda Mbeya mjini ambayo ilikuwa na abiria watano iliigonga gari hiyo na kusababisha kifo cha Dereva wake Yuda Ambokile na wengine kujeruhiwa vibaya na magari mengine Toyota Cheser T 512 BCT na Nissan T 991 BAK.

Baada ya gari hiyo kugonga gari iliyokuwa imeegeshwa na kusababisha madhara hayo ndipo gari nyingine aina ya Baloon ikagongwa na gari hiyo aina ya Escudo kisha Baloon hiyo ikatumbukia korongoni na kusababisha majeruhi wawili waliokuwemo ndani ya gari hiyo ambao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Mmoja wao akaruhusiwa baada ya hali yake Kiafya kuimarika.

Ajali hiyo haikuishia hapo bali gari nyingine aina ya Pickup yenye namba za usajili T 991 BAK nayo ikakumbwa na dhahama hiyo ambapo iliharibika vibaya bila kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwemo ndani yake.

Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutembelewa na waandishi wa habari leo, wengi wao walikutwa wakiwa na hali mbaya na kushindwa kuzungumza chochote bali baadhi yao waliokuwa na nafuu walisema kuwa walikuwa hawakumbuki chochote juu ya ajali hiyo zaidi ya kujikuta wamelazwa wakiwa na majeraha katika miili yao.

Majeruhi hao ambao baadhi yao waliweza kuzungumza na waandishi wa habari ni pamoja na Denis Untwa (24) ambaye ni dereva wa Baloon, Laina John Sanga (35), Michael Mteve (20), Anania Simbeye(35) ambaye ni dereva wa Escudo, Emmanuel Tambikeni na mmoja aliyejitaja kwa shida jina moja la Boniface..
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 2 comments»

Abiria 30 wanusurika Kifo katika ajali mbaya iliyo tokea eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya



 Ajali ya gari ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya mpaka mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini,  ambayo imetokea mteremko wa Mbalizi ambapo zaidi ya abiria Thelathini wamenusurika kifo, baada ya gari kushindwa kupandisha mlima hali iliyopelekea kupinduka. Tukio hili limetokea siku ya Jumapili.
Baada ya kupinduka kwa gari hiyo ambayo hufanya tuti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya hadi Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini hatimaye lilinusurika kutumbukia bonde la mtoni Mbalizi yukio lililotokea siku ya Jumapili.

Jeshi la polisi Usalama barabarani Mbeya mnapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini magari yenye karoso kwa lengo la kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima  
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»