Showing posts with label LOWASSA. Show all posts
Showing posts with label LOWASSA. Show all posts

LOWASSA, SUMAYE WAONGEA CCM


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Andrew Chenge (kushoto) na Edward Lowassa wakipeana mikono baada kutoka katika kikao cha NEC, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi




WALIA KUCHAFULIWA NA MAKADA WENZAO,NEC YARIDHIA GAMBA KUREJESHWA CC
Habari na Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma.
******



MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji.

Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?”Sumaye alinukuliwa akihoji.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: “Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu”.

Richmond yatajwa
Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.

Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC

Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.
Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho.
Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi.

Kujivua gamba
Kufuatia uamuzi huo wa NEC hivi sasa mpango wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho, Aprili mwaka huu unarejeshwa CC ambapo watuhumiwa wote wa makosa mbalimbali watafikishwa mbele ya Kamati za maadili na kuchukuliwa hatua kwa taratibu za chama hicho.

Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho na sasa unarejeshwa Kamati Kuu (CC) ili ichukue hatua zaidi kwa wale waliogoma kujiuzulu.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo ukimya ambao unaashiria kutokuwapo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari yao kama ilivyotarajiwa.

Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa.

Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.

Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: “Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja”.

Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: “Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho”.

Nec yawakaanga kina Jairo
Katika hatua nyingine, NEC imeunga mkono hatua zilizopendekezwa na Bunge dhidi ya watumishi wa umma waliotajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoanika uozo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma ndani ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kamati hiyo katika ripoti yake iliyowasilishwa mwishoni mwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, iliwataja Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyesimamishwa), David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba wanastahili kuchukuliwa hatua.

Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, huku wabunge wakipendekeza pia kuondolewa madarakani kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

NAPE AKISALIMIANA NA WAZEE WA CCM


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC, Bw. Edward Lowassa. wakati wa kikao cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma jana. Kulia kwa Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Fredrick Sumaye na Bw. Kingunge Ngombale Mwiru (kulia)
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

MH. LOWASSA ACHANGISHA MIL 200 UJENZI WA KANISA KATOLIKI NYAKATO,MWANZA


Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa kanisa Katoliki Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu la Mwanza jana kabla ya kuendesha haranbee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kubwa kuliko yote Kanda ya Ziwa ujenzi ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 700.Litakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa wakati.Katika harambee hiyo zilikusanywa shilingi milioni 200 ikiwa ni zaidi ya mahitaji ya shilingi milioni 120.



Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Mara, Mh. Christopher Mwita Gachuma (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa, kushoto ni aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Lawrance Masha.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Mara, Mh. Christopher Mwita Gachuma (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa, kushoto ni aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Lawrance Masha.



[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

LOWASSA ACHANGISHA MIL 126.9 ZA UJENZI WA MABWENI SEKONDARI YA ASKOFU JOHN SEPEKU ILIYOPO BUZA MTONI, DAR ES SALAAM



Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikani Tanzania, Valentino Mokiwa (kushoto) akipokea mchango wa sh. mil 10 kutoka kwa mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (katikati), Regina Lowassa, zilizotolewa na familia ya Lowassa katika harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Askofu John Sepeku iliyopo Buza Mtoni, Dar es Salaam. Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisa la Aglikani Segerea, Dar es Salaam leo, ambapo zaidi ya sh. mil. 126.9 zilichangangwa. Waziri Mkuu mstaafu aliahidi kutoa tena sh. milioni 10. 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikani Tanzania, Valentino Mokiwa (kushoto), akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alichangia sh. mil. 3,katika harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Askofu John Sepeku iliyopo Buza Mtoni, Dar es Salaam.
Mtoto David Gideon (4), akitoa mchango wake wa sh. 1000 kwa Askofu Mkuu Valentino Mokiwa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa mabweni ya shule hiyo.


Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa (kulia) akikumbatiana kwa furaha na mke wa Askofu Mokiwa, Mama Grace Mokiwa,  wakati wa harambee hiyo.

Baadhi ya waumini wakishangilia baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Eward Lowassa kutangaza kuvuka kwa malengo ya harambee hiyo, ambapo malengo yalikuwa kukusanya sh. mil. 100 lakini zilichangwa sh. mil 126.9.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na baadhi ya waumini wa Kanisa la Anglikani, waliochangia fedha katika harambee hiyo.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

HOTUBA YA EDWARD LOWASSA 19.10.2011

HOTUBA YA MBUNGE WA MONDULI, EDWARD LOWASSA
KWA WAANDISHI WA HABARI MONDULI, OKTOBA 19, 2011

NDUGU wana habari nimewaita katika mkutano huu leo kwa sababu moja kubwa, kutoa ufafanuzi kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakitokea huku yakinihusisha mimi binafsi kwa namna ambayo sasa yanatishia ustawi na mshikamano wa kimaadili, kihistoria na kikazi miongoni mwa viongozi na baina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ndugu wana habari, naamini mmkekuwa mkifuatilia kwa karibu habari zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazolihusisha jina langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baada ya kuwa zimesharipotiwa katika vyombo vya habari.

Uamuzi wangu wa kukutana nanyi leo hauna makusudi ya kuzozana na vyombo vya habari wala kwenda kinyume na utamaduni wa kimaadili wa ndani ya chama changu unaotutaka viongozi kujadili masuala yanayokihusu chama chetu ndani ya vikao vyetu rasmi vya kimaamuzi bali kutoa ufafanuzi na angalizo kwa pande zote hizo mbili ambazo zinaguswa na matukio yanayoendelea kutokea leo hii.

Moja ya mambo ambayo yameligusa jina langu kwa namna hiyo ni lile linalonihusisha eti na kundi moja la wanasiasa ambao wamekuwa na mikakati ya kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Hakuna shaka ni madai ya kipuuzi, kizushi na yenye malengo machafu.

Hawakuishia hapo sasa wamefikia hatua ya kuvitumia vyombo hivyo hivyo vya habari kufikia hatua ya kudai kwamba nimeanza kuandaa orodha ya kile wanachokiita madhambi ya Rais Kikwete ambayo wandai nimepanga kuyasoma wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CCM).

Ninaamini kwa dhati kabisa kwamba, waandishi wa habari wanaofuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa masuala ya kisaiasa nchini wanatambua kwamba, watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo kwa malengo ya kufikirika na kujisafishia njia kisiasa.

Ni jambo lisiloingia akilini kunihusisha na kile kinachoitwa mikakati ya kumhujumu rais au chama ambacho mimi ni kada wake wa muda mrefu, mbunge anayetokana na chama hicho hicho na mtu anayeiongoza Kamati nyeti ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na zaidi ya yote kiongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na kiserikali nilizowahi kushikilia.

Kuhusu hili napenda kusema kwa uwazi kwamba, mbali ya ukweli kuwa sijapata kufikiria hata mara moja kuhusu hicho wanachokiita mabaya au madhambi ya rais, sina wala siijui hiyo wanayoitaja kuwa ni orodha ya mabaya ya namna yoyote dhidi ya Rais Kikwete.

Mbali ya ukweli kwamba huo ni uongo wa wazi, silika yangu kama mwanasiasa na mtu mwenye dhamana kubwa kwa watu wa Monduli na kwa taifa langu haiwezi kamwe kunituma nianze kupanga mikakati ya kumhujumu kiongozi wetu mkuu au chama ambacho kimenilea na mimi mwenyewe nikakitumikia kwa uadilifu na kwa juhudi kubwa pengine kuliko ilivyo kwa hao wazushi.

Ndugu wana habari, nitakuwa ni mtu wa mwisho kufikiria au kupanga kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama na rais ambaye nimemuunga mkono kwa dhati kwa muda mrefu na kushirikiana naye katika harakati nyingi za kifikra na za kiuongozi katika ngazi mbalimbali na kwa miaka mingi. Nilipatana kuliesema hili na leo nalirudia tena. Mimi na Rais Kikwete hatukukutana barabarani.

Tangu serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani kuna kundi la watu limekuwa likifanya juhudi kubwa kunigombanisha na Rais wakitumia kila aina ya hoja za kupikwa.

Kundi hilo ambalo sasa limekuja na uzushi mpya, ndilo ambalo mwaka juzi lilipenyeza ndani ya chama chetu na katika jamii hoja kwamba nilikuwa nimejipanga kugombea urais kwa tiketi ya chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, likidai kwamba nilikuwa na mlango ya kumpinga Rais Kikwete ambaye wakati huo alikuwa ndiyo kwanza anaelekea kukamilisha ngwe yake ya kwanza madarakani.

Katika kuthibitisha kwamba watu hao walikuwa na hila, nilipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam miezi kadha kabla ya Uchaguzi Mkuu nilijibu kwa kifupi nikisema, hatukukutana na Rais Kikwete barabarani.

Nayasema haya na kurejea baadhi ya mambo huku nikiwa na imani ya dhati kabisa kwamba, viongozi wenzangu ndani ya CCM na wale walio na nia njema na chama chetu na taifa hili, akiwapo Mwenyekiti wetu wa Taifa, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete hawawezi kamwe kuamini kushawishiwa na propaganda chafu zinazoendeshwa na kikundi kidogo cha wanasiasa hao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ambayo malengo yao ya kisiasa yako wazi na yanayojulikana.

Kama hiyo haitoshi, wanasiasa hao hao baada ya kulitumia jina langu kama ajenda yao ya uzushi wa kila namna, sasa wameanza kunihusisha hata na matukio ya kisiasa kama yale yaliyotokea majuzi tu hapa Arusha.

Ndugu wana habari baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa, nimeamua kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kisiasa na kisheria ambazo namini zitatoa majibu sahihi dhidi ya wale wote walio nyuma ya ajenda hizi chafu kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawia ndani ya chama changu na kwa jamii nzima ya Watanzania ambao kwa muda mrefu wamelishwa mambo mengi ya kizushi na wakati mwingine ya hatari dhidi yangu.

Tayari nimepanga kuanza kuwasiliana na kuwasilisha malalamiko yangu kwa mamlaka husika zinazosimamia mienendo ya kimaadili na weledi wa kitaaluma wa vyombo vya habari kama vile Msajili wa Magazeti na Baraza la Habari Tanzania.

Kama hiyo haitoshi, baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu nimeshaanza kufikiria na kujipanga kuanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa habari na wahariri ambao kwa makusudi wameamua kutumia vibaya uhuru wa habari ambao serikali imeutoa. Naamini sote tunakubaliana kuwa; ‘UHURU USIO NA NIDHAMU NI FUJO.’

Ndugu zangu wana habari napenda kutumia furasa hii kutoa wito kwa viongozi wa chama na wale wa serikali kumsaidia rais na chma chetu kwa kutimiza ipasavyo wajibu wao badala ya baadhi yao tena wakiwamo wale wenye dhamana nyeti kuwa vinara wa kutunga mambo ya kufikirika kama haya wanayofanya leo.

Viongozi wenye mawazo ya namna hiyo wanapaswa kutambua kwamba, muda adhimu wanaoutumia kubuni na kuzusha uongo kila kukicha mbali ya kuwavunjia heshima wao weneywe unavidhalilisha vyombo vya dola ambavyo vinafanya kazi kubwa kuhakikisha hujuma za namna yoyote dhidi ya viongozi na taifa zinadhibitiwa.

Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge na mtu aliyepata kuwa Waziri Mkuu ninatambua na kuiheshimu kwa dhati kazi hiyo kubwa inayofanywa kwa weledi mkubwa na taasisi mbalimbali za dola zenye wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wa viongozi wetu na taifa kwa ujumla.

Ndugu wanahabari nazungumza nanyi baada ya kurejea nikitokea katika nchi za Nigeria, Malaysia, Singapore, India, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambako nilipata fursa ya kujifunza mambo mengi lakini moja muhimu likiwa ni namba vyombo vya habari (kwa maana ya waandishi wa habari) na wanasiasa wanavyotumia muda wao mweingi kujadili amasuala yanayogusa maisha na maendeleo ya watu wao.

Tofauti na kile wanachofanya wenzetu hapa nyumbani, ninyi wanahabari na sisi wanasiasa tumekuwa tukitumia muda wetu mwingi kujadili watu na propaganda za kisiasa zisizo na tija wakati tukitambua kwamba, taifa linakabiliwa na changamoto nyingi kama zile za kuhamasisha uwezekazji wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha mifumo ya utawala bora, kuporomka kwa thamani ya shilingi kila kukicha, mdororo wa uchumi, tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kushuka kwa kiwango cha elimu na ugumu wa maisha kwa ujumla. TUNAPASWA KUJISAHIHISHA.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

LOWASSA NDANI YA KANISA LA NABII TB JOSHUA NCHINI NIGERIA


BAADA ya kuandamwa na ‘kashikashi’ za kisiasa kwa muda mrefu, Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa (CCM), ameonekana ‘laivu’ runingani akifuatilia kwa karibu ibada ya Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Kikristo ya Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Mtume na Nabii Temitope Balogun Joshua ‘T.B Joshua’ huko Lagos, Nigeria.

Ishu hiyo ambayo imekuwa gumzo katika mitandao fulani fulani ilijiri hivi karibuni ambapo waziri mkuu huyo mstaafu alionekana kupitia Runinga ya Emmanuel TV.

Katika ibada hiyo iliyokuwa na ‘taito’ ya Sunday Live Service, ujumbe wa siku hiyo ulikuwa ni kushinda woga katika kujaribu kutenda jambo lolote.

T.B Joshua ni mmoja wa viongozi wenye heshima duniani aliyejipatia umaarufu kutokana na unabii anaoutoa kuhusu masuala mbalimbali, uponyaji kwa njia ya maombi na maombezi ya kawaida.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»